Natafuta Rafiki, Mchumba

Mimi nitaenda nje kidogo ya mada. Nimeoa nakaa dar. Hivi kwa wenzangu walio oa ni kawaida kwa mwanaume kumpa hela mkewe kila mwezi? Mimi ninafanya hivyo kila mwanzo wa mwezi (200,000) sasa juzi juzi hapa (miezi 3 imepita) kaanza kulalamika eti haitoshi nimuongezee. Yeye ana kazi yake mwenyewe ila ukweli ni kuwa mshahara wake kwa mwezi hata robo tu hauufikii wangu.Hili suala limeshakuwa kero kwangu. Ninafikiria kuacha kumpa kabisa. Kaja na historia ya akina mama wenziwe ninaowajua wanapewa 400,000 au zaidi. Mfumo huu niliuanzisha mwenyewe kwa kuwa wakati nakua baba yangu mzazi alikuwa anafanya hivyo. Je ni mimi tu nimekuzwa hivyo au ni kawaida kabisa kwa waliooa kufanya hivyo? Naweza kumwambia bila matatizo kuanzia leo upati kitu fanya utakalo.

Usiache kumpa kama kipato chako kinakuruhusu. Naona scenarios 2 hapa. Kwanza ni tamaa. Asijilinganishe na wanawake wengine, huo ndio mwanzo wa tamaa, tunatofautiana vipato hivyo si rahisi kila mwanamke kupata kile ambacho mwanamke mwenzie anapata: kuna wengine hawapati kabisa... je anaweza kukuambia naomba usinipe pesa kwa vile mama fulani hapewi pesa na mumewe?

Pili, Pengine anavyokueleza kuwa wanawake wengine wanapewa 400,000 hamaanishi wanawake...je kama kuna jibaba limemwahidi kumpa hizo lakini inaonyesha kuwa anakupenda so kuliko kupata hizo lakini 400,000 toka nje, ni bora apate hata kama ni 250,000 au 300,000 toka kwako.

Kwa swali lako kama ni kawaida kupewa pesa kila mwezi naona umewalenga zaidi wanaume. Ila kukupa mfano wangu ni kwamba napewa 2/3 ya mshahara wa mume wangu kila mwisho wa mwezi. Tulikaa chini tukapiga hesabu kutokana na mshahara wake na wangu na ukubwa wa familia yetu.
 
pole kwa yaliyokukuta huyo mwanamke kwa kifupi hyakufai but kama anataka hivyo lazima kuna wenzake wanamshauri afanye hivyo
Jaribu kukaa nae na umuulize hizo fedha anazozitaka sasa hivi umuongezee anafanyia nini?
Na wewe pia jaribu kufuatilia au kufahamu kama kuna watu wameongezeka katika familia yako au kuna kitu gani? ambacho anataka kukifanyia mabadiliko yoyote
Maranyingi wanawake hao huwa wanapenda kuiga kutoka katika familia nyingine jaribu kumwambia abadilike
 
pole kwa yaliyokukuta huyo mwanamke kwa kifupi hyakufai but kama anataka hivyo lazima kuna wenzake wanamshauri afanye hivyo
Jaribu kukaa nae na umuulize hizo fedha anazozitaka sasa hivi umuongezee anafanyia nini?
Na wewe pia jaribu kufuatilia au kufahamu kama kuna watu wameongezeka katika familia yako au kuna kitu gani? ambacho anataka kukifanyia mabadiliko yoyote
Maranyingi wanawake hao huwa wanapenda kuiga kutoka katika familia nyingine jaribu kumwambia abadilike
 
Mimi nitaenda nje kidogo ya mada. Nimeoa nakaa dar. Hivi kwa wenzangu walio oa ni kawaida kwa mwanaume kumpa hela mkewe kila mwezi? Mimi ninafanya hivyo kila mwanzo wa mwezi (200,000) sasa juzi juzi hapa (miezi 3 imepita) kaanza kulalamika eti haitoshi nimuongezee. Yeye ana kazi yake mwenyewe ila ukweli ni kuwa mshahara wake kwa mwezi hata robo tu hauufikii wangu.Hili suala limeshakuwa kero kwangu. Ninafikiria kuacha kumpa kabisa. Kaja na historia ya akina mama wenziwe ninaowajua wanapewa 400,000 au zaidi. Mfumo huu niliuanzisha mwenyewe kwa kuwa wakati nakua baba yangu mzazi alikuwa anafanya hivyo. Je ni mimi tu nimekuzwa hivyo au ni kawaida kabisa kwa waliooa kufanya hivyo? Naweza kumwambia bila matatizo kuanzia leo upati kitu fanya utakalo.

To be fair kwake pia ana majukumu home kama kununua chai na kitafunio mwezi mzima kila siku, bili ya maji, etc

Pole sana kwa masahibu hayo mwenzangu.
Si uwongo kwamba gharama za maisha Tanzania ziko juu kwa sasa, ukilinganisha na miaka kadhaa hapo nyuma. Huenda ndio sababu kama hizi na nyingine ambazo zimemfanya mkeo aone kwamba pesa unazompa hazimtoshi. Suala la kujilinganisha yeye na wanawake wenzake kwa kipato nadhani hatendi haki hata kidogo. Kulinganisha kipato cha familia yenu na za wenzake na kudai cha juu sio haki kwa sababu huenda mishahara ya waume wa wenzake ni tofauti kabisa na wa kwako, huenda wao wakuzidi sana.
Kaa chini, ongea nae kwa upole, mkae mjadili bajeti ya nyumba yenu kwa mwezi mzima na kuangalia hizo gharama za juu zinazozidi. Nadhani mpaka hapo mnaweza kudodosa chanzo cha ongezeko la gharama anazodai mkeo.
Tuendelee kuelimishana.
 
Mimi nitaenda nje kidogo ya mada. Nimeoa nakaa dar. Hivi kwa wenzangu walio oa ni kawaida kwa mwanaume kumpa hela mkewe kila mwezi? Mimi ninafanya hivyo kila mwanzo wa mwezi (200,000) sasa juzi juzi hapa (miezi 3 imepita) kaanza kulalamika eti haitoshi nimuongezee. Yeye ana kazi yake mwenyewe ila ukweli ni kuwa mshahara wake kwa mwezi hata robo tu hauufikii wangu.Hili suala limeshakuwa kero kwangu. Ninafikiria kuacha kumpa kabisa. Kaja na historia ya akina mama wenziwe ninaowajua wanapewa 400,000 au zaidi. Mfumo huu niliuanzisha mwenyewe kwa kuwa wakati nakua baba yangu mzazi alikuwa anafanya hivyo. Je ni mimi tu nimekuzwa hivyo au ni kawaida kabisa kwa waliooa kufanya hivyo? Naweza kumwambia bila matatizo kuanzia leo upati kitu fanya utakalo.

To be fair kwake pia ana majukumu home kama kununua chai na kitafunio mwezi mzima kila siku, bili ya maji, etc

Pole sana kwa msongo wa mawazo usiwe na shaka hapa JF utapata kila aina ya jibu ila akili kichwani kwako kuyachambua.

Katika maelezo yako umetoa general hesabu ambayo mimi kwa binfasi naona haitupi mwanga wa kuelewa kwa kina tatizo liko wapi wapo wengi wataweza sema ni hela nyingi wapo watakaosema ni chache kwa hiyo ni vem utuambie hiyo hesabu ni relative to what.

pili hujatueleza ktk nyumba yako hiyo hela inatumika kwa kitu ganina inatakiwa kuwahudumia watu wangapi kwa muda wa mwezi mmoja. Maana wapo ambao watakwambia zinatosha kabisa maana ana tumbo moja tu la kulisha na wapo watakwambia hazitoshi kwa kuwa ana matumbo mengi ya kulisha.

tatu, nadhani haitokuwa vema kwa watu kumwita mkeo kuwa ana tamaa maana hatujui yeye ni mtu wa aina gani hadi aamue kutumia mfano wa watu wengine ili kuweza kukushawishi kumuongezea hela. kwangu binafsi naona ni gross judgement kwa kitu ambacho hatukielewi kiundani kimeanzia wapi. Maana wapo watu wengine hadi wapewe mifano halisi ndio wanaamua kukubali na kushawishika kuyakubali mawazo ya wenzi wao. Maana ninafahamu hata wanaume wanatumia mifano ya marafiki na watu wanaowajua ili kushawishi wake zao wanahitaji gari jipya au kiwanja kipya au hata mavazi mapya kisa fulani naona anayo. Je tumwite mwanaume kama huyo kuwa ana tamaa?

Ushauri wangu kwako ni huu:

1. Inaelekea wewe na mkeo mna mapatano ya nani ana jukumu lipi na kwa kutmia kipato kipi. Sidhani ni haki kwako kuchukulia kuwa kwa kumpa mkeo laki 2 ndo umetatua mahitaji yote ndani ya nyumba. je umewahi fikiria yanaweza yakatokea mahitaji ambayo hamkuyapangia na yakahitaji pesa nje ya hizo? Binafsi nafikiri inakupasa wewe na mkeo mkae chini muiangalie upya mahitaji yenu na matumizi yenu ili na wewe uelewe hela inatumikaje. Nisikudanganye, I am not spendthrift ila kwa hela hizo ulizotaja hapo, nyumbani kwangu zinatosha kununua sun dries (vitu kama toiletries,soap, rice, beans, unga, mafuta etc etc.) pekee yake ya mwezi mzima hapo bado sijapangia mshahara wa HG, na ununuaji wa mboga kila siku, ununuaji wa vitafunio vya chai, entertainment needs kwa watoto na ndugu wakija, usafiri wa kwenda kazini, usafiri wa watoto, magonjwa na dawa n.k nk. na mara zote haya mahitaji mengine huzidi hata hiyo laki 2 unayotoa. Ila yanazidi kutokana na kwamba nina familia kubwa. Je swali kwako na wewe una familia kubwa? Na ndio maana ninaona si haki kutoa comments bila kuelewa where you are coming from with this.

2.Solution kwako nyingine ni participation katika kila linalowezekana ndani ya nyumba yako. wanaume wengi TZ wana stereotypic values ambazo zinasababisha wake zao kuanza tabia za kuwadanganya na kuwaibia fedha. Najua wengi tunatumia mifano ya wazazi wetu ila yatupasa pia kujua huu ni wakati tofauti na sio kwamba mkeo atakuwa na uwezo sawa na mama yako ambayo ilimridhisha baba yako) I think you have the right to know where your money is going and what it is being used for. Usiwe a patronizing husband, mwenye kudai kuwa umetoa pesa unahitaji kuona unalishwa vizuri na kuangaliwa na mke hali hujui efforts zinazotumika kukuweka katika hali hiyo. Matokeo yake unaenda kwa nyumba ndogo na unafikiri analolifanya ni vema kuliko mkeo wakati yeye ana tumbo lako na lake na ni mara moja moja anahitaji kukuandalia kwa hiyo deinitely atakuandalia vizuri kuliko nyumbani kwako ambapo wewe hukutaka kujishirikisha kufahamu uwezo wa uendeshaji wa mkeo.

Nadhani mkeo will appreciate it ukitaka kujua na kumsaidia katika kupanga mahesabu kama she is genuine in her needs. Kama alikuwa anatafuta mbinu za kununua gold na wax lazima atakataa kukushirikisha.

all the best ktk kuweka mambo yako sawa.
 
Ushirombo hilo neno kaka....hawa wenye ma-degree hawaeleweki mkuu hata kama unaishi ughaibuni sio issue sana mbona ni vitu vinavyoweza kurekebishika nadhani huyo binti wa kisukuma mwenye diploma ya ualimu ni mwake mwake kabisa...Kwanza mwalimu (lazima discipline itakuwepo) pili msukuma niwajuavyo wasukuma hata kama alizaliwa Agakhan Hospit na kukulia masaki wengi si vicheche...baba H kwani kama ni mayai ya huko ughaibuni unampeleka tuition tu mambo yatakuwa sawa na kwa level ya diploma mzee mbona kianzio unacho kaka shaka ondoa.

Kwani lazima akaajiriwe??? Aweza kuwa mjasiriamali vilevile au ughaibuni imekatazwa nakuhurumia mzee na hao wadada wenye degeree wengi wao utulivu 000 angalia mambo ya msingi kwanza especially true love vinginevyo anaweza kufika huko ukapigwa kibuti vilevile mifano tunayo mzee.
 
Widen your search kaka, toa vigezo visivyo na umuhimu such as nationality na degree priority, pia umri anzia 19 to 26!! then utafanya filtering mwenyewe!! Good luck!!
 
Widen your search kaka, toa vigezo visivyo na umuhimu such as nationality na degree priority, pia umri anzia 19 to 26!! then utafanya filtering mwenyewe!! Good luck!!

I like your name coz i used to call my self Makaveli when I was young,,hope you understand what I mean dawg!!?!!,,anyway huyo mshikaji vigezo vinamkosehsa ngoja amalize na mie niende hewani maana nataka kuondokana na ukapela kupitia JF
 
Naona wale wadau wote mliokuwa mnatafuta wenza kupitia baraza hili mmekaa kimya, pasi na shaka mmeshawapata wale mliokuwa mnawatafuta.
Invisible ushapata?
Kila la kheri
 
haya mambo ya mikwanja ni tabu sana...Ndugu yangu hayo mambo katika familia nyingi za wanawake kudai kuongezewa dau from time to time lakini kama alivyo-comment bimkubwa bado kuna maswali mengi hapo yanayotakiwa kujibiwa kabla mtu hafanya conclusion.

Jambo moja ninaloliona mimi kuwa mara nyingi familia nyingi za kipato cha kati na juu kidogo huwa bajeti zake zinalenga zaidi katika suala la mahitaji ya chakula ambayo mtu anaweza ku-justfy matumizi yake hata kabla hajaenda dukani au sokoni. Hapa nina maana kuwa mwanamke anaweza kudai pesa kwa ajili ya kilo kadhaa za mchele, maharage, sukari, mafuta ya kula au kupikia??? (nisaidieni kunyoosha kiswahili hapa)na mambo mengine kiasi kwmba mwanaume akaridhika na kutoa hiyo pesa. Hata hivyo lazima ieleweke kuwa pesa inayotolewa hata kama ni kwa chakula tu haiwezi kuwa sawa kutoka mwezi mmoja hadi mwingine...sababu iko wazi bei za vitu hu-fluctuate kila wakati tena baya zaidi fluctuation hiyo ni ya kupanda..POINT # 1

Kuna mahitaji mengine ya msingi bila kujali idadi ya watu katika familia kama vile mavazi,matibabu,usafiri,kama binadamu dharura mbali mbali zinazoweza kujitokeza nje ya bajeti iliyoandaliwa achilia mbali starehe na burudani nyingine za kawaida kabisa zisizohitaji effort kubwa kuzifanya e.g kupata lager angalau kwa wiki mara moja kutegemea ana nguvu yako kiuchumi. Haya yote yana-relation sana na kipato cha mtu. Sasa suala la mkeo kudai 200,000 haitoshi inawezekana kweli ana sababu ya msing kufanya hivyo na kama walivyoshauri wengine kuna haja ya wewe na mkeo kukaa chini pamoja kuzungumza kirefu juu mambo niliyotaja hapo juu na nina imani mtapata ufumbuzi. Nadhani si vyema kuamini kuwa malezi uliyopata wewe toka kwa wazazi wako unzaweza ku-apply katika maisha ya sasa ni ngumu sana sana utaishia kusononeka may be na kukwaruzana na mkeo kila wakati.

Alternatively, jaribu kufanya itafiti katika matumizi ya msingi anayofanya mkeo uone kama yanaendana na pesa unayompa. Unajua tatizo siku hizi baadhi ya akina mama wamekuwa si wawazi sana katika financial matters hata kama utaamua kumpatia yeye fungu lake kama mother house ili ajiweke soap soap wanafikiria mambo mengine makubwa ambayo si priority at particular time e.g God chain za gram 10 na kuendelea, sijui nywele za kimasai pale mwenge msuko mmoja 40,000 hujaweka madiko diko mengine ya kupaka mwilini, mavazi sitaki kusema usipokuwa makini mnaweza hata kuharibu hiyo bajeti ya nyumba yenu kama hutakuwa firm katika ku-handle haya mambo.

So ndugu you need time kufanya hayo yote and ikibi give her a hand katika kupanga once ukibaini she has genuine arguments kwani nyie ndio wa kupanga future ya familia yenu na si vinginevyo usije kuingia mkenge ukaona kero uka-opt small house you'll die my brother!!!

Pia kumbuka kusimama kidete katika mambo ya msingi ili hiyo pesa mnayopata ifanye yaliyomo katika priorities zenu...
 
Naona wale wadau wote mliokuwa mnatafuta wenza kupitia baraza hili mmekaa kimya, pasi na shaka mmeshawapata wale mliokuwa mnawatafuta.
Invisible ushapata?
Kila la kheri

As one of them, tujulushe mmefikia wapi? I mean, tutakula wali lini? All the best.
 
Naona wale wadau wote mliokuwa mnatafuta wenza kupitia baraza hili mmekaa kimya, pasi na shaka mmeshawapata wale mliokuwa mnawatafuta.
Invisible ushapata?
Kila la kheri

Dah!
Mshkaji nilipata ndo maana kwenye hiki kibaraza nilipotea kwa muda ila yaliyonikuta hayafai kusimulia kabisa!

So, that is to say bado naendelea kutafuta manake sikupata kile ninachokitaka ila ni utumbo na uozo mtupu tu ndo niloambulia!

Wat about you IDIMI?
 
What about you IDIMI?

Pole sana Kaka 'Pasko'
Mie nilishampata na tunaendelea na mawasiliano kama kawaida, kila kitu chenda vema kabisa.
Lakini usikate tamaa kabisa, kwani hujui lini mambo yatakuwa poa. Wasanii wapo kibao sana hapa mahali, kwa hiyo sishangai unaposema ulikutana na 'Mambo makubwa' kunako chemba kwako.
Tuendelee na mjadala.
 
Mzee naona unaweka mitego hapo mwanangu ila usihofu utawanasa tuu. Kama ni rafiki wa kushauriana naye pia wakubwa zaidi ya 30yrs wanaweza kukupa constructive ideas bila shaka. Au sio ushauri wa kawaida? Nakutakia kila la kheri mwana.

kwiki kwi kwi !!! huu uchokozi !!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom