Natafuta partner wa kufuga Samaki kwa Vizimba (Cage)

babilas25

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
471
332
Kutokana na uchache wa ajira uliopo nchi kwetu, nilitamani sana kupata partner ambae nitashirikiana nae kwenye ufugaji wa Samaki kwa kutumia vizimba, kitu pekee nlichonacho kama mtaji ni taluma ya ufugaji samaki.

Nahitaji mdau mwenye nia ya dhati asapoti kwenye utengenezaji wa vizimba na ununuzi wa vifaranga na chakula. Anayewiwa tukutane PM.

Au kwa mawasiliano +255764123459.

IMG-20201007-WA0002.jpg

Update

Nimekua nikipigiwa simu na watu wakitaka kujua hatua za kupitia ili kuweza kumiliki kizimba.
Leo nitakueleza hatua kwa hatua na ghalama zake.

UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA

•Hatua na mambo mhimu ya kuzingatia.

1.Vibali vya uendashaji wa shuguli za ukuzaji viumbe hai majini

I)Mhutasari wa kikao cha serikali ya kijiji au mtaa ambapo mradi utafanyika.

II)TAFIRI- Kufanya survey kwenye eneo ambapo vizimba vitawekwa, kupima kina cha maji, ubora wa maji, mkondo wa maji, ukubwa mawimbi n.k. galama ni Tsh. 2,700,000/=

III)NEMC-Kufanya Environmental Impact Assessment, galama yao n 4,200,000/=

IV)Bonde la Ziwa Victoria- Kutoa kibali cha matumizi ya maji

V)Barua ya Afsa uvuvi wa eneo husika

VI) Kibari kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi idara ya ukuzaji viumbe hai majini.

2.Kutengeneza kizimba na Kupanda vifaranga.
-Kizimba chenye urefu wa mita6, upana mita6 na kina cha mita6, kinaweza kubeba vifaranga 10,000.
-Galama za kutengeneza kizimba na kupanda vifaranga ni 6,500,00/=

3.Galama za vyakula
-Awamu ya kwanza 360kg(Starter) za chakula zitatumuka kwa miezi3.
-Awamu ya pili kilo 420kg(Glower) kwa mda wa miezi 2
-Awamu ya tatu ni kilo 300 kwa mda wa mwezi1
(Galama za chakula zinaweza kuongezeka au kupungua kutegemea na mwitikio wa ulaji wa samaki)

4.Galama ya usimamizi na ulinzi wa mradi (Ni makubaliano)

5.Mavuno; Kwenye kizimba cha ukubwa wa mita za eneo 36 kinaweza kubeba vifaranga mpaka 10,000, Matarajio ya kuvuna ni samaki 8500 mpaka 9000 ambao wanakadiliwa kuwa na uzito wa gram 400 mpaka 600
Wastani wa mavuno ni tani 2.5 kwa miezi 6.
 
Asanteni kwa mlionitafuta kwa kutaka ufafanuzi juu ya ufugaji samaki kwa vizimba, namna ya kupata vibari na mambo mengine ya mhimu kabla ya kuanza ufigaji.

Ukiwa na swali au maoni kuhusu ifugaji samaki kwa vizimba usisite kuuliza au kunitafuta kwa namba +255764123459.
 
Aisee nlikuwa nafanya feasibility study ya hii kitu nimekwama kwenye chakula gharama kubwa sana. Nlitaka nianze na cage moja yenye sato elf10 cage ya mita 6x6x4 nimepiga chakula tu ni almost 15tons hadi wanavunwa
Kufuga kwenye cage maana yake ni unawatenga hukohuko baharini au ziwani au naomba kujuzwa.
 
Aisee nlikuwa nafanya feasibility study ya hii kitu nimekwama kwenye chakula gharama kubwa sana. Nlitaka nianze na cage moja yenye sato elf10 cage ya mita 6x6x4 nimepiga chakula tu ni almost 15tons hadi wanavunwa
Msosi wa samaki sio mchezo.
 
Nimekua nikipigiwa simu na watu wakitaka kujua hatua za kupitia ili kuweza kumiliki kizimba.
Leo nitakueleza hatua kwa hatua na ghalama zake.

UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA

•Hatua na mambo mhimu ya kuzingatia.

1.Vibali vya uendashaji wa shuguli za ukuzaji viumbe hai majini

I)Mhutasari wa kikao cha serikali ya kijiji au mtaa ambapo mradi utafanyika.

II)TAFIRI- Kufanya survey kwenye eneo ambapo vizimba vitawekwa, kupima kina cha maji, ubora wa maji, mkondo wa maji, ukubwa mawimbi n.k. galama ni Tsh. 2,700,000/=

III)NEMC-Kufanya Environmental Impact Assessment, galama yao n 4,200,000/=

IV)Bonde la Ziwa Victoria- Kutoa kibali cha matumizi ya maji

V)Barua ya Afsa uvuvi wa eneo husika

VI) Kibari kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi idara ya ukuzaji viumbe hai majini.

2.Kutengeneza kizimba na Kupanda vifaranga.
-Kizimba chenye urefu wa mita6, upana mita6 na kina cha mita6, kinaweza kubeba vifaranga 10,000.
-Galama za kutengeneza kizimba na kupanda vifaranga ni 6,500,00/=

3.Galama za vyakula
-Awamu ya kwanza 360kg(Starter) za chakula zitatumuka kwa miezi3.
-Awamu ya pili kilo 420kg(Glower) kwa mda wa miezi 2
-Awamu ya tatu ni kilo 300 kwa mda wa mwezi1
(Galama za chakula zinaweza kuongezeka au kupungua kutegemea na mwitikio wa ulaji wa samaki)

4.Galama ya usimamizi na ulinzi wa mradi (Ni makubaliano)

5.Mavuno; Kwenye kizimba cha ukubwa wa mita za eneo 36 kinaweza kubeba vifaranga mpaka 10,000, Matarajio ya kuvuna ni samaki 8500 mpaka 9000 ambao wanakadiliwa kuwa na uzito wa gram 400 mpaka 600
Wastani wa mavuno ni tani 2.5 kwa miezi 6.
 
Asante kwa ufafanuzi ulioutoa hapo juu. Mosi, ningependa kujua upatikanani wa materials za kujengea hivyo vizimba. Hizo nyavu ni saizi gani na zinapatikana wapi?
Pili, wewe binafsi mtu akitaka akutumie kuelekeza elekeza mambo kwenye mradi huo, gharama zako zinakuwaje?
 
Materials kwa ajili ya kutengenezea vizimba kwa sasa yanapatikana hapa hapa nchini,
 
Nakupongeza sana kwa jitihada zako. kule ziwa victoria/Musoma walianza wajeshi wakafuga kwa vizimba na baadaye watu wengine na makampuni wakafuatia. Hata hivyo wasiwasi wangu umebaki kwenye ukuaji wa mbegu inayotumika hapa kwetu ya nile tilapia (Oreochromis niloticus). Kusema kweli hii mbegu haikui aiseee iwe kwenye cages, mabwawa ya kuchimba hata uongeze oxygen hata ufunnge aerators. Kwa sababu kwa mtizamo wa kibihashara mafanikio katika ufugaji wa samaki ni, low mortality rate, ukuaji wa haraka kwa maana ya kuongezeka uzito haraka na eventually matumizi kiasi ya chakula basi.
Kuna wafugaji wamepambana wakapata vibali vya wizara wakaleta mbegu ya Chitralada Tilapia kutoka Thailand lkn naona baaado kasi ya ukuaji ni ndogo. Kuna wengine wameleta tilapia toka Entebe ambayo wa Israel wamefanyia sorting kwa muda mrefu lkn bado ukuaji wake ni mdogo.

Kwa ufupi, to breakeven kwenye ufugaji wa samaki ni ngumu kidogo kwa species zetu hizi chache tulizo nazo.
Wachina kwao wanafuga zaidi ya spices za samaki 100 kwenye maji baridi tu wakati sisi tunafuga zaidi zaidi 2 tu. Pamoja na hayo wachina kama wachina hata wakija hapa kwetu wakaweka cages ziwani samaki wao watakua kwa haraka kwa sababu watawalisha ma hormones kibao wakue fast.

Kuna wakati nilijaribu kufanya campaign ya kuingiza species nyingine za samaki wanaofugwa kwa faida kama pangasius lkn zikagonga mwamba nikakata tamaa baada ya kupoteza zaidi ya 95m kwenye hekaheka hizo.
 
Unaposema Nile Tilapia hakui vizuri unamaanisha nini? Watu wanatoa gram 400 kwa miezi mitano wakitumia system ya RAS na mbegu ya dume tupu(YY) na mwingine kafuga YY kwenye bwawa la asili katoa gram 600 miezi 6. Unaposema hawakui sikuelewi. Maana kwa miezi 6 uvune samaki mmoja ana nusu kilo huwezi kupata hasara kamwe
 
Nakupongeza sana kwa jitihada zako. kule ziwa victoria/Musoma walianza wajeshi wakafuga kwa vizimba na baadaye watu wengine na makampuni wakafuatia. Hata hivyo wasiwasi wangu umebaki kwenye ukuaji wa mbegu inayotumika hapa kwetu ya nile tilapia (Oreochromis niloticus). Kusema kweli hii mbegu haikui aiseee iwe kwenye cages, mabwawa ya kuchimba hata uongeze oxygen hata ufunnge aerators. Kwa sababu kwa mtizamo wa kibihashara mafanikio katika ufugaji wa samaki ni, low mortality rate, ukuaji wa haraka kwa maana ya kuongezeka uzito haraka na eventually matumizi kiasi ya chakula basi.
Kuna wafugaji wamepambana wakapata vibali vya wizara wakaleta mbegu ya Chitralada Tilapia kutoka Thailand lkn naona baaado kasi ya ukuaji ni ndogo. Kuna wengine wameleta tilapia toka Entebe ambayo wa Israel wamefanyia sorting kwa muda mrefu lkn bado ukuaji wake ni mdogo.

Kwa ufupi, to breakeven kwenye ufugaji wa samaki ni ngumu kidogo kwa species zetu hizi chache tulizo nazo.
Wachina kwao wanafuga zaidi ya spices za samaki 100 kwenye maji baridi tu wakati sisi tunafuga zaidi zaidi 2 tu. Pamoja na hayo wachina kama wachina hata wakija hapa kwetu wakaweka cages ziwani samaki wao watakua kwa haraka kwa sababu watawalisha ma hormones kibao wakue fast.

Kuna wakati nilijaribu kufanya campaign ya kuingiza species nyingine za samaki wanaofugwa kwa faida kama pangasius lkn zikagonga mwamba nikakata tamaa baada ya kupoteza zaidi ya 95m kwenye hekaheka hizo.
Asante, Mkuu kwa ufafanuzi mzuri wa kitalaamu,
Nimekutana na changamoto hizo awali na nimezifanyia kazi mbegu zote hizo mbili kwa maana ya hiyo ya Thailand na ya Entebe, changamoto kubwa ni ya kimazingira na chakula.

Kwa sasa kunaimprovement kubwa sana watu wanafuga na samaki wanakua mpaka kufikia 600gm kwa miezi 6.
Karibu tushare experience na utembelee baazi ya mashamba wanayofuga uone wakiwa wanavuna.

Tuwasiliane kwa namba hii mkuu +255 764 123 459
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom