Natafuta partner wa kufanya naye biashara ya ufuta

konabar

Member
Apr 18, 2018
25
19
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, naishi Rufiji Bungu, ni eneo linalojishughulisha sana na shughuli za kilimo hasa mihogo, ufuta na korosho. kipindi hiki ni kipindi ambacho ufuta unavunwa kwahiyo wakulima wanauza ufuta kwa watu wenye mitaji kwa tsh 2000/= kwa kilo na Serikali inatarajia kununua kwa 3500 kwa kilo. Nakaribisha mtu yeyote mwenye cash na kutaka kutengeneza faida ya 1500 kwenye kila 2000/=. na prefer kwa waliokaribu hasa maeneo ya Dar.

Ili uweze kuona nini kinanunuliwa at list kila week na kuepusha lawama na kukiona kinachonunuliwa bila kusahau lile zao jingine la mwezi wa 9 tunaweza shirikiana na kuliuza bila shida...... kwa yeyote atakaependezewa anicheki inbox. Kuna watu tumezungukwa na fursa lakini hatuna mtaji na kuna watu mna mitaji lakini hamna fursa au mnabanwa na kazi za kuajiriwa, tushirikiane kujikwamua kiuchumi, amina.
 
Bungu ni kibiti kiongozi sio Rufiji... Nilishituka nikadhani upo Rufiji tupige kazi... Karibu Nyamwage Muhoro Miwaga...
 
kama kichwa cha uzi kinavyojieleza. naishi rufiji bungu, ni eneo linalo jishughulisha sana na shughuli za kilimo hasa mihogo, ufuta na korosho. kipindi hiki nikipindi ambacho ufuta unavunwa kwahiyo wakulima wanauza ufuta kwa watu wenye mitaji kwa tsh 2000/= kwa kilo na serikali inatarajia kununua kwa 3500 kwa kilo. nakaribisha mtu yeyote mwenye cash nakutaka kutengeneza faida ya 1500 kwenye kila 2000/=. na prefer kwa waliokaribu hasa maeneo ya dar. ili uweze kuona nini kina nunuliwa at list kila week na kuepusha lawama nakukiona kinachonunuliwa bila kusahau lile zao jingine la mwezi wa 9 tunaweza shirikiana na kuliuza bila shida......kwa yeyote atakae pendezewa anicheki inbox. kuna watu tumezungukwa na fulsa lakin hatuna mtaji na kuna watu mnamitaji lakn amna fulsa au mnabanwa na kazi za kuajiliwa tushirikiane kujikwamua kiuchumi amina
Duh! Huko kwenu ufuta haupo under control ya vyama vya ushirika? Maana nanusa harufu ya kangomba hapa
 
Serikali ya nchi gani inakuja kununua ufuta na ni lini? Acha kudanganya watu wewe.

Tarehe 1/June >Waziri akiri mkanganyiko soko la ufuta. WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga, amekiri kuwapo mkanganyiko katika ununuzi wa zao la ufuta kwenye maeneo mbalimbali nchini na kuagiza utumike mfumo wa zamani badala ya soko la bidhaa. Mfumo huo wa zamani unamruhusu mtu yeyote kwenda kununua maadam afuate taratibu zilizowekwa.
 
Bungu ni kibiti kiongozi sio Rufiji... Nilishituka nikazani upo Rufiji tupige kazi... Karibu Nyamwage Muhoro Miwaga...
Naam kuweni makini, dalili zinaonesha kwa mara nyingine tena mkulima wa ufuta atalia kilio cha mbwa koko. Tatizo ni Magufuli na serekali yake!. serekali ina migogoro ya kodi na wanunuzi wakubwa. Ina athiri vipi mkulima nitaeleza baadaye.
 
Back
Top Bottom