Natafuta partner tufungue mechanical workshop

SiliconValley

Member
Oct 17, 2018
56
59
Ndugu wanajamvi, mimi nimejiajiri ktk tasnia ya ufundi ( mechanical Engineer) nimefanya ktk tasnia hii kwa miaka 10 sasa, kwa sasa nataka kushea changamoto na mtu mwingine mwenye nia ya dhati katika biashara,

Maoni yangu nipate mtu ambae ana elimu ya ufundi katika kusimamia mafundi/ kazi au kufanya yeye mwenyewe ( put his hand into practical) au ku finance, japo sitilii kipaumbele kwa mtu wa ku finance sana kwa kuwa tasnia hii inahitaji sana "eye supervision" japo najua hela ni kila kitu.

Kwa sasa mimi nafanya ktk open workshop nawaza kufanya ktk closed door workshop. Na kuongeza facility zaidi.
nahitaji kuwalenga wateja wakubwa na wadogo, wa mbali na karibu.

Wateja ni wa aina 3.
1, mafundi
2, wamiliki wa magari
3, fabrication and metal working.

Majukumu ya partner ni kuwa kama mwekezaji mwenza, kwa 50 % lakini hii ni baada ya mjadala baina yetu. Au kulingana na vile atakavyoona inafaa kuwekeza.

Nakaribisha maoni, mjadala, mawazo au changamoto mpya

Naishi na kufanya shughuli zangu Tegeta ,Dar es Salaam
Simu yangu ni 0655 844 202
 
Back
Top Bottom