Natafuta partner katika biashara ya kusambaza maji maeneo yenye uhaba wa maji

smanyonyi

Member
Nov 22, 2013
16
14
Naomba kuwashirikisha hii fursa, kwangu nina kisima kirefu chenye maji mazuri sana yaani yamepoa hayana test ya chumvi kabisa. Nimeona kuna fursa kubwa kwenye biashara ya kuuza maji, kama yupo mtu mwenye uwezo wa kuwekeza kwenye biashara hii naomba aje inbox.
Nini kinaitajika:
1.Kujengea mnara wa kuweka tank la maji lisilopungua lita 5,000
2.Kutandaza bomba la kufikisha maji kwenye tank.
3.Kununua tank la maji lisilopungua lita 5,000
4.Kununua gari la kusambazia maji ( Toyota canter) yenye uwezo wa kubeba lita 3,000 za maji
5. Kununua matank matatu ya lita 1,000 kila moja
6.Water pump itakayotumika kusambazia maji kwa wateja
Namengineyo yatakayojitokeza hili kukamilisha mradi huu. Mahitaji haya ni kutokana na uelewa wangu wa mwanzo, lakini akipatikana muwekezaji tutakaa na kufanya tathimini kwa kukusanya taharifa zaidi.
Mara baada ya mradi kuanza , Tutagawa mapato asilimia 50% kama return on investment kutoka kwenye mapato ya kila siku/mwezi baada ya kutoa gharama za uendeshaji kama vile umeme, mafuta na salary ya dereva, mpaka pesa yote iliyowekezwa itakapokuwa imerudi , baada ya hapo tutaendelea kushare profit kulingana na makubaliano
Hii biashara inalipa na ina risk ndogo sana, tutaweka mkataba kabla ujaanza kuwekeza pesa yako.
AMBAYE ATAKUWA TAYARI AJE INBOX.
NIPO DAR-ES-SALAAM, WILAYA YA ILALA, KATA YA KIVULE
 
nakumbuka mwaka 2015 nililetewa dili kama hilo jikumu langu ilikua kununua generator kubwa kama m20 hivi,kweli nilinunua hela yangu mpka leo sijawai kuiona,wenye mradi nao waliyatekeleza mabomba yao huko huko,mradi ulikua singida...matarajio na uhalisia kwenye hii miradi ni tofauti kabisa..!!
 
nakumbuka mwaka 2015 nililetewa dili kama hilo jikumu langu ilikua kununua generator kubwa kama m20 hivi,kweli nilinunua hela yangu mpka leo sijawai kuiona,wenye mradi nao waliyatekeleza mabomba yao huko huko,mradi ulikua singida...matarajio na uhalisia kwenye hii miradi ni tofauti kabisa..!!
Huu ni tofauti na huo unaosema biashara hii hapa Dar kama ujabahatika kukutana na magari yamebeba matank ya maji basi tembelea maeneo ya mbezi, kimara, kibamba, mbezi salasala utakutana nayo, huu sio mradi wa kusambaza mabomba bali unasambaza maji kwa kutumia gari kwenye maeneo yenye shida ya maji, utapata tabu mwanzo kutengeneza base ya wateja baada ya hapo ndio utaona wepesi wake
 
Back
Top Bottom