Natafuta mwekezaji katika biashara au mtu atayekubali kuweka hela kwenye kila kazi na tutagawana faida

Mech

Member
Nov 13, 2017
96
210
Habari wakuu,

Nimerudi kwenu kwa mara nyingine tena. Mwaka juzi (2021), nilikuja hapa kwenye jukwaa na kutafuta business partner ambaye atakuwa tayari kuwekeza kwenye Machine shop. Hii kwa maana ya kwamba mimi nitawekeza kwenye Ujuzi & Marketing na yeye atawekeza kwenye ununuzi wa machines ambazo ndio zitakuwa nyezo za kufanyia kazi na gharama za mwanzo za kununulia materials pindi kazi zikipatikana. Machines hizo zilikuwa ni Lathe M/C, Milling M/C, Shaper M/C na Welding M/C.

Sikufanikiwa kupata Business partner kwa wakati ule, hii ni kwa sababu kwa wakati ule wazo langu lilikuwa ni too risk hasa kwa mtu ambaye hana ujuzi na mambo ya Machine shop kuwekeza hela yake. Baada ya kukosa mwekezaji, mwaka huo 2021 nikaanza kutafuta kazi (Ikumbukwe tayari nilikuwa nimeshasajiri kampuni ambayo ipo active na documents zilizokamilika). Nikawa nafanikiwa kupata kazi ndogo ndogo ambazo zilikuwa zinanisaidia kulipia Operational costs za kampuni. Pindi nikipata kazi, inanibidi niwe na Cash ya kununua material na pia ya kuwalipa mafundi ili waweze kukamilisha kazi. Nilikuwa siwezi kuchukua material kwa mkopo kwa sababu ya ugeni kwenye industry. Pia malipo ya kazi nilizokuwa nazifanya, Payment inaweza kuchukua siku 30-60days. Na supplier wa materials wanataka hela yao ndani ya 20days (Hii ni kama umechukua kwa mkopo).

Kwa sasa nina changamoto ya mtaji unaozunguka (Running Capital). Asilimia 90% ya running capital ipo mikononi kwa customer. Hii ni kutokana na kwamba kuna ucheleweshwaji wa malipo. Na kwa sasa nina potential ya kupata kazi, kazi ambazo siwezi kuzisponsor kwa sababu ya kutokuwa na fedha za kununua materials na kuwalipa mafundi. Hivyo ninakuja kwenu nahitaji mwekezaji ambaye atawekeza Milioni 5 as per makubaliano. Au ambaye atakuwa tayari kuwekeza kwa kila kazi inayopatikana na kugwana profit as per makubaliano. Kwa sasa nina kazi ya M3 na inahitahi Milioni moja kuweza kuikamilisha.

Natanguliza shukrani. Kwa maelezo zaidi PM yangu iko wazi
 
Ofisi iko mkoa gani?
Na mwekezaji akiwekeza iyo million 1 hapo anapata gawio kiasi gani?
Asante
 
Ofisi ipo Dar es Salaam.Swala la kugawana faida ni makubaliano tutakayoafiki baina ya pande mbili.
 
Hongera mkuu kwa hatua uliyofikia. Binafsi nipo kwenye situation ya kwako ambapo unahitajika mtaji wa kujiendesha yaani working capital. Nimejaribu kufanya options zifuatazo ili kupata working capital
1. Kusajili kampuni

2. Kuandaa business plan pamoja na blueprint ya operations

3. Kutafuta investors ambapo changamoto kubwa ni suala la investors kushindwa kuelewa wazo langu la biashara na pia sina network kubwa ya wafanyabiashara wanaoweza kunivet ili niaminike.

3. Kutafuta mtaji wa kujiendesha kwa njia mbadala mfano; kuomba mikopo isiyo na riba kupitia halmashauri japo changamoto zake ni kuwa ipo slow sana na huchukua miezi kadhaa ili upate fedha hizo kama umekidhi vigezo. Pia kuna taasisi kama PPRA ambazo zinatoa fedha kama mikopo kwa vijana na vikundi ila sijafuatilia kujua utaratibu ukoje.

4. Kuingia ubia na makampuni au tasisi kwa ajili ya kutoa huduma. Hii inesaidia kwa namna fulani kuhakikisha maisha yanaenda pia some operatinal cost za kampuni zinakuwepo pamoja na kukuza portfolio.

Zaidi ya hapa nikutakie kila la kheri katika mapambano mkuu.
 
Hongera sana Mkuu,
Vipi ulifanikiwa kupata fedha kupitia Halmashauri au kupata mkopo usio na riba?. Kama ndio, vigezo na masharti ilikuwa ni nini?
 
Ofisi ipo Dar es Salaam.Swala la kugawana faida ni makubaliano tutakayoafiki baina ya pande mbili.

Oh okay sawa. Vp kuhusu kutatua changamoto y wateja wako kulipa kwa wakati ikiwa kama ss wanavyo chelewesha malipo kwa siku 30 mpk 60. Kuhusu hili umejipangaje?
 
Hii changamoto itatatuliwa kwa kuwa na running capital inayoweza kucover expenses zote ndani ya siku 90 hadi 100
 
Habari wakuu,

Nimerudi kwenu kwa mara nyingine tena. Mwaka juzi (2021), nilikuja hapa kwenye jukwaa na kutafuta business partner ambaye atakuwa tayari kuwekeza kwenye Machine shop. Hii kwa maana ya kwamba mimi nitawekeza kwenye Ujuzi & Marketing na yeye atawekeza kwenye ununuzi wa machines ambazo ndio zitakuwa nyezo za kufanyia kazi na gharama za mwanzo za kununulia materials pindi kazi zikipatikana. Machines hizo zilikuwa ni Lathe M/C, Milling M/C, Shaper M/C na Welding M/C.

Sikufanikiwa kupata Business partner kwa wakati ule, hii ni kwa sababu kwa wakati ule wazo langu lilikuwa ni too risk hasa kwa mtu ambaye hana ujuzi na mambo ya Machine shop kuwekeza hela yake. Baada ya kukosa mwekezaji, mwaka huo 2021 nikaanza kutafuta kazi (Ikumbukwe tayari nilikuwa nimeshasajiri kampuni ambayo ipo active na documents zilizokamilika). Nikawa nafanikiwa kupata kazi ndogo ndogo ambazo zilikuwa zinanisaidia kulipia Operational costs za kampuni. Pindi nikipata kazi, inanibidi niwe na Cash ya kununua material na pia ya kuwalipa mafundi ili waweze kukamilisha kazi. Nilikuwa siwezi kuchukua material kwa mkopo kwa sababu ya ugeni kwenye industry. Pia malipo ya kazi nilizokuwa nazifanya, Payment inaweza kuchukua siku 30-60days. Na supplier wa materials wanataka hela yao ndani ya 20days (Hii ni kama umechukua kwa mkopo).

Kwa sasa nina changamoto ya mtaji unaozunguka (Running Capital). Asilimia 90% ya running capital ipo mikononi kwa customer. Hii ni kutokana na kwamba kuna ucheleweshwaji wa malipo. Na kwa sasa nina potential ya kupata kazi, kazi ambazo siwezi kuzisponsor kwa sababu ya kutokuwa na fedha za kununua materials na kuwalipa mafundi. Hivyo ninakuja kwenu nahitaji mwekezaji ambaye atawekeza Milioni 5 as per makubaliano. Au ambaye atakuwa tayari kuwekeza kwa kila kazi inayopatikana na kugwana profit as per makubaliano. Kwa sasa nina kazi ya M3 na inahitahi Milioni moja kuweza kuikamilisha.

Natanguliza shukrani. Kwa maelezo zaidi PM yangu iko wazi
Wazo lako zuri nenda serikalini unana na sekta usika naamini utasikilizwa wakikuzingua nenda ofisi za chama Lumumba kulalamika ili wachukuliwe hatua.
 
Kwa nini niende kulalamika mkuu?

Nikalalamike kwa kosa gani walilofanya?
 
Back
Top Bottom