tamsana
JF-Expert Member
- Jan 13, 2012
- 3,354
- 7,306
Mithali 23:29-35Mkuu kuwa na hofu ya Mungu haimaanishi kuwa usinywe! Ndio maana ukisoma biblia utaona hata Yesu alibariki mvinyo.
Kikubwa ni kujua unakunywa kwa kiasi gani na kufuata kanuni zake.
Sitaki nivae joho la kuwa mlokole wakati najua fika kuwa sometimes huwa nakunywa. Nipo very clear katika hilo
29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
30 Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31 Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32 Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.
33 Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34 Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Waefeso 5:18-21
18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;
19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
20 na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
21 hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.