Natafuta mume

Mwajey123

Member
Mar 23, 2017
20
23
Wapendwa
Najitokeza tena kwenye jukwaa hili, kuchukua hii fursa ya kujitafutia mwenza aliyeko tayari kuanza maisha;
sifa zangu;

  1. Nina umri wa miaka 39
  2. Sijawahi kuolewa wala sina mtoto
  3. Naishi Dar na ninajitegemea
  4. Ni mjasiriamali mdogo
  5. Nimelelewa kwenye familia ya Kiislam
  6. Elimu yangu ni kidato cha nne
  7. Nina mwili wa kawaida, rangi ya maji ya kunde/mweusi
Napendelea Mume ninaye muhitaji awe na sifa hizi;
  • Awe na umri wa 45 na kuendelea (Sifa za umri na dini ni Muhimu kwangu)
  • Akiwa na mtoto ni sawa; nipo tayari kumlea kama mwanangu
  • Asiwe kwenye Ndoa ila kama alisha wahi kuoa haina tatizo
  • Awe na kipato (mjasiriamali au ameajiriwa)
  • Awe tayari kuoa na sio kuchezeana au kupotezeana muda
Kwa aliye tayari karibu pm tuchati
Kama huna sifa au unatafuta mtu wa kujitimizia haja ya mwili wako naomba ukae pembeni/Usi pm!
 

Attachments

  • 1569069838471.png
    1569069838471.png
    432 bytes · Views: 33
Samahani imekuwaje umekaa umri wote huo hujawahi kuolewa..!?
Ilihali elimu yako ni kidato cha nne..!?

Siku zoote taarifa zina sema kuwa; wanawake ni wengi kuliko wanaume
Hivyo ni lazima tukubali kuwa, sio wote wataolewa/wataolewa kwa wakati sawa

Naunga hoja ya waislamu kuoa mke zaidi ya mmoja pale mazingira yanapo ruhusu ili kufanya dada zetu wote waingie kwenye ndoa salama
 
Kwanini mnaweka kikwazo cha umri hata kama kijana wa miaka 20 kasha jipanga na yuko teyari anaweza kukuoa tu hivi huwa hamwoni mfano kwa Diamond na Zari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom