Natafuta mume jamani mbona sipati

Natafuta mume jamani mbona sipati

Komaa na Bwana Yesu utapata.Usilazimishe.Ila nakushauri utafute Mkristo,sio Mkristu.Mkristu atakusumbua.Sijui kama unanielewa.
Awe mweupe au maji ya kunde
mrefu
alie ajiriwa au mfanya biashara
umri 30 kuendelea
awe mcha mungu mkristu
 
Wewe sema unataka mume atakae kupenda kwa dhati na mcha Mungu nichek pm
 
Mazingira unayoishi kuanzia shuleni, chuoni, kazini na mitaani kwa ujumla ndio yatakufanya upate mume bora. Kuna kipindi ukikichezea basi tena huwezi kumpata aliye bora. Jiangalia kampani yako ikoje huko mitaani kwako, unamcha Mungu? Mavazi yako na tabia kwa ujumla ukoje? Una majivuno au kiburi? Umeshaachwa na wanamume wangapi na kwa sababu gani? Kama umeshachezea ujana wako umeshaomba toba ya kweli kwa Mungu wako na kutaka kufunguliwa?
Asante kwa ushauri
 
Humapti kwasababu bado uko kwenye stage ya kubagua wanaume. Ukiwa unahitaji ndoa kweli hutajali rangi yake. Endelea kusubiri maji ya kunde watakuja tu...
 
Wenzio tulikalia sifa tukaja kuolewa watu wenye sifa tofauti na tunaishi mpaka tuna wajukuu. Maji ya kunde au mweupu ukipata mkorogo wa kicongo je utajua? Akiachishwa kazi baada ya harusi tu utafanyaje? Akija mkristu au kama mwingine alivyosema mkristo whatever, halafu akaja na tabia za kukucontror unakoenda, unakopita, mshahara wako, ndugu zako je utaona sawa sababu ni maji ya kunde, mkristu/o, ameajiriwa/mfanyabiashara na umri huo?Fafakari kabla ya kuamua. Unaweza pata mzee au kijana kuliko wewe halafu mweusi kama Sokoine lakini ukawa na raha na amani kuliko hizo sifa zako zote ulizoweka.
 
Humapti kwasababu bado uko kwenye stage ya kubagua wanaume. Ukiwa unahitaji ndoa kweli hutajali rangi yake. Endelea kusubiri maji ya kunde watakuja tu...
Kabisaa ndo nimemwambia asiweke expensive wakat wanaume tuko simple
 
If you are serious pm your number
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom