Natafuta Mtangazaji wa Michezo

Root root AE

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2018
Posts
212
Reaction score
370
Kwema wakuu.

Natafuta mtangazaji wa media yangu ya online. Media inahusu michezo, hivyo nahitaji mtu wa kunisadia kufanya mahojiano na mashabiki, preview za kabla na baada ya mechi, nk

Media yangu bado changa, lakini licha ya hivyo nitajitahidi mtangazaji asikose hata hela ya maji😎

Kama ni wewe au unamfahamu mtu anayesomea au aliyesomea utangazaji na anapenda michezo kinomanoma naomba tuwasiliane PM.

Asanteni sana!
 
Bwashee mbona kemia ni kama kumsukuma mlevi wa visungura tu, yani unachanganya changanya vodka na nyangi kutoa kitu tu
Wakati niko from four ilibaki kidogo sana niunguze Laboratory. Nilichanganya vitu zaidi ya kumi kwenye test tube 🤣
 
Hela ya maji ndiyo shilingi ngapi? Nyoosha maelezo. Kama huna hela ya kueleweka ya kumlipa huyo mtangazaji, fanya hilo jukumu wewe mwenyewe. Kwa maana bado hujafikia hatua ya kuitwa mwajiri.
 
Hela ya maji ndiyo shilingi ngapi? Nyoosha maelezo. Kama huna hela ya kueleweka ya kumlipa huyo mtangazaji, fanya hilo jukumu wewe mwenyewe. Kwa maana bado hujafikia hatua ya kuitwa mwajiri.
wataenda kugombana tu kama hana hela ,vifaa vyenyewe usikute ana laptop moja icore 7 na smartphone ya google pixel,anasema ana media
 
ofc zako ziko wapi ,dogo aje

hela ya chai ndio Nauli ya kuja na kuondoka. chai asubuhi ,lunch mchana na posho ya kazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…