Natafuta msichana wa kuwa katika mahusiano naye, mahusiano thabiti yenye mlengo wa kudumu

Daniel Adrian

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
311
322
Habari za saa hizi wakuu.

Upweke si kitu chema, nilikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na msichana fulani ila mambo yakaenda kombo. Alipata mwingine. Ikanikera sana ikaniumiza sana na ikasababisha nisitake mahusiano yoyote.
Lakini upweke si kitu chema.
Nimekuja hapa kueleza nia yangu ya dhati ya kuhitaji mke, mwanamke ambaye atakubali kuwa katika mahusiano nami mahusiano ambayo tuyajenge kwa lengo moja tu, NDOA.

-Nahitaji ambae ana angalau elimu ya form 4.
-Dini/kabila lolote lile.
-ila sipendi mwanamke mfupi sana.
-awe mweupe au mweusi yote sawa tu haina shida, ila napenda sana super blac, rangi ya lami.
-Umri wangu ni chini ya miaka 30. Ila nahitaji mwanamke ambae hatazidi miaka 25.
-Sihitaji mwanamke mwenye mtoto, niwe muwazi. Na nimepanga kuwa watoto wawili tu katika maisha yangu.

Nime edit: Baada ya kushauriwa na watu kadhaa kwa nia njema tu nime edit moja ya vigezo. Niko tayari tuwe na mpaka watoto wawili.
 
Mtoto mmoja are you serious ? mwanamke gani atakubali huo ujinga ? Hivi unajua raha ya kabebii wewe ? Muoga utafikiri wewe ndio unaingia leba.

Sent using Jamii Forums mobile app

Asante kwa kutoa maoni yako dada angu.

Majukumu ndo yananifanya niwe ivyo. mimi ni mtoto wa kwanza kwetu, hapa unaponiona nna wadogo zangu kadhaa nalea.
 
Asante kwa kutoa maoni yako dada angu.

Majukumu ndo yananifanya niwe ivyo. mimi ni mtoto wa kwanza kwetu, hapa unaponiona nna wadogo zangu kadhaa nalea.
Majukumu hayaishi mdogo wangu..

Mimi kwetu ndio wa kwanza baba yangu wakati anafariki aliniachia wadogo zangu watatu .. wote wakiwa bado wadogo kabisa na kipindi hiko ndio ninaanza kazi kwa mara ya kwanza.

Nimesomesha wote na hivi sasa amebaki mmoja tu ambaye amemaliza kidato cha nne mwaka jana na matoke yake sio mazuri.

Mimi mwenyewe nina watoto watatu wa ndoa na mmoja wa mchepuko ila maisha yanaenda poa tu.

Usiwaze sana maisha ndio haya haya zaa angalau watoto wawili au watatu ,mmoja ni uoga wa maisha uliokithiri.

Asante sana kaka kwa kunishauri.

Wakati mwingine income panel ndo inanifanya nijaribu kuji-limit. Maisha yanatufunza vingi sana na niwe muwazi tu mshahara wangu unapotoka huwa unaishia kwenye majukumu woote kiasi cha kwamba nna kiwanja ila sijaweka hata msingi tu. Sasa nikapiga moyo konde kwenye swala la maisha ya mahusiano na familia ila nikisema ntazaa mtoto zaidi ya mmoja ntakuwa siendani na uhalisia wangu na kipato.

Ila nikupongeze sana kwa ujasiri ulio nao kaka. Maana wadogo zako plus watoto watatu hiyo inahitaji ubongo uchemke kweli kweli ili kutimiza mahitaji.
 
Mtoto mmoja are you serious ? mwanamke gani atakubali huo ujinga ? Hivi unajua raha ya kabebii wewe ? Muoga utafikiri wewe ndio unaingia leba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mwaka fulani nilikua makambi ya wakimbizi wenye asili ya kutoka kwa Kabila. Sasa kuna kesi niliikuta asubuhi ustawi wa jamii. Mama wa kibembe analalamika mumewe hataki kumpa mimna, tulimuuliza kwani una watoto wangapi? She replied 6 kids. Nikajisemea bora mzee baba ampe tu cuz ration yenyewe bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nnavowish kuwa na watoto 5, nimeshangaa eti mtoto 1 duh, hapana aisee. Kwanza elimu bure ,nothing to fear hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa kuchangia.

Hali ya maisha na income panel ndo inafanya mipango ya familia iwe ya namna gani. Napenda mtazamo wako kuhusu mipango ya familia.

Lakini jambo la msingi sio tu mipango au kuwa na watoto ila je, watapata mahitaji yao yote vizuri ?
-Kusoma shule nzuri.
-kula vizuri.
-kuvaa nguo nzuri. (Hujawai skia mtaani wanasema, mtoto wa nani yule kavaa nguo zimeisha vile ?)
-kulala mahali pazuri.
 
Back
Top Bottom