Natafuta mke mwema.

Tized

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
4,023
2,000
Mkuu endelea kuwa tu siriazi zaidi na ulokole wako, kwani hujawahi kukutana na hili andiko mahali? ''Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana mith 19.14'' Tena mithali 30:10 ikaandikwa ''Mke mwema ni nani awezaye kumuona?.........'' ''Au mkuu bado hujazoea mitaa ya huku galilaya?'

Huhusu Mume mwema, sijawahi kukutana na andiko linalohoji, so Wanaume wote nadhani watakuwa wema, wadada tu washindwe wenyewe kutufaidi, hahaaaaaa!! ni hayo tu mkuu wangu. kila la kheri.
 
Himawari

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
2,583
2,000
MIMI NI KIJANA WA KIKRISO MWENYE UMRI WA MIAKA 33, NAHITAJI MKE MWENYE SIFA ZIFUATAZO:*awe mkristu mwenye imani sana kwani mimi ni mlokole hasa.*awe na elimu isiyopungua form four .*awe na umri kati ya 20-27.*awe mrefu wa wastani na siyo pungufu ya 4.5 ft*awe mrembo,mweupe wa asili siyo mweusi na awe na umbo zuri hasa hips za ukweli.*awe tayari kupima na kuwa na mimi kimaisha.MIMI NI MREFU WA FT 6, MWEUSI KIASI, NA MWEMBAMBA KIASI,NI MLOKOLE HASA NA SINA MCHEZO NA MASWALA YA IMANI YANGU NAMI NAAMINI KATIKA WAEFESO 5:22-28(tafadhali soma).ALIYE TAYARI ANITAFUTE KWA NAMBA 0652- 750905.

Mhhh hapo kwenye ulokole haswa panatufukuza wengi!!
Kwani hata ambae si mloloke huwezi kumuokosha along the way?
 
MadameX

JF-Expert Member
Dec 27, 2009
7,812
2,000
Kumbe walokole wanabagua pia, lazima cheupeeeeeeeee. Haya ubarikiwe kwenye hili
 
BashiriOnline

Senior Member
Nov 5, 2012
127
195
Utatongoza hadi Jini..Mwanamke wa Mtandao sio Mzuri Man...Humjui tabia,ukishindwa kabisa,Nenda Suka Dar,au Kahumba Morogogoro..Pimbi wewe!Na hisi utakuwa Domo Zegeeeee
 
fered mbataa

JF-Expert Member
Feb 19, 2012
240
0
rudi brother ujipange, unaposali, unapoishi, unapofanyakazi na maeneo mengine hujaona huyo mwema? Mpe hii task mchungaji wako pengine huwezi kuongea. Note si vizuri kutafuta mchumba maeneo kama haya, mtu anaweza jifanya msafi kwa mda na kwakuwa wewe unatafuta mchumba wa mda mfupi then umuowe anaweza bugi brother.
 
Vituka

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
2,250
2,000
MIMI NI KIJANA WA KIKRISO MWENYE UMRI WA MIAKA 33, NAHITAJI MKE MWENYE SIFA ZIFUATAZO:*awe mkristu mwenye imani sana kwani mimi ni mlokole hasa.*awe na elimu isiyopungua form four .*awe na umri kati ya 20-27.*awe mrefu wa wastani na siyo pungufu ya 4.5 ft*awe mrembo,mweupe wa asili siyo mweusi na awe na umbo zuri hasa hips za ukweli.*awe tayari kupima na kuwa na mimi kimaisha.MIMI NI MREFU WA FT 6, MWEUSI KIASI, NA MWEMBAMBA KIASI,NI MLOKOLE HASA NA SINA MCHEZO NA MASWALA YA IMANI YANGU NAMI NAAMINI KATIKA WAEFESO 5:22-28(tafadhali soma).ALIYE TAYARI ANITAFUTE KWA NAMBA 0652- 750905.

Samahani sana ila mkuu hapa umechemsha mbaya!Kwanza walokole hasa kamwe hawawezi kuja humu kusaka wake/mke! Kifupi nina wasiwasi na huo ulokole wako hasa nikiangalia hapa chini:

Join Date : 3rd December 2012
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,863
2,000
Je wewe ni mume mwema au better than thou? Kila la heri. Mke mwema hutengenezwa na si kutafutwa ingawa kuna kunguru wasiofugika.
 
hanimimitu

Member
Dec 3, 2012
5
0
inawezekana kwani BWANA huangalia nia na sio chochote ukishasema hivyo ina maana tiyari unajua uelekeo sahihi, you are welcome!
 
hanimimitu

Member
Dec 3, 2012
5
0
Mhhh hapo kwenye ulokole haswa panatufukuza wengi!!
Kwani hata ambae si mloloke huwezi kumuokosha along the way?
inawezekana kwani usemapo hivyo inaonekana una fahamu uelekeo wenyewe yaani njia sahihi ambayo ni YESU unaijua tayari hio nia ndio inayo wafanyaga watu waokolewe na MUNGU si matendo yao kwani kila mtu kabla hajaokolewa alikutwa na dhambi na ndio maana akaokolewa -hivyo kama wote tulitenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa MUNGU basi tofauti ni NIA zaidi ;pale unapotenda lakini ukatamani usingetenda hiyo ni sababu itakayomfanya MUNGU akutazame na akupe uwezo huo wa KUTOTENDA ambao unautamani-YOU ARE WELCOME DADA!
 
steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
8,051
2,000
duu,hv we ni mlokole kweli au ni mloo wa 'k' tu,watu wote si ni sawa,iweje utake sifa zote hzo kama kweli we ni mtu wa MUNGU,umeambiwa JF ndo sehemu ya kuoa au kuolewa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom