Natafuta Military Academy for Private Military Training

Prof

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,577
2,452
Wana board, Heshima kwenu!
wakati taifa likiwa kwenye msiba mkubwa, nami naungana na ndugu na jamaa katika majonzi na masikitiko ya kuondokewa na vijana wetu, Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awarehemu na kuwalaza mahala pema peponi. Amen!

Pia, kwa kuwa JF ni kisima cha fikra na maarifa ningependa kujuzwa kama kuna military academy nchini Tanzania or kwenye nchi jirani kwa ajili ya private military training. Natafuta chuo cha kijeshi kwa ajili ya first born wangu ambaye amemaliza chuo mwaka jana. sikutaka aanze kazi kwa sababu maalum...natanguliza shukrani.
 
Mpeleke jkt au apply US huko Kuna wabongo na Waafrika Wengi wanajiunga kwenye vitu hivyo
Mkuu Kuna usalama lkn asijebaadae kusumbua kutaka ajira kijeshi..
Asante sana mkuu. nitajaribu kuangalia option ya JKT ingawa kwa US fees zao ni kubwa sana. Ni salama kabisa, ingawa najaribu kumwandaa mapema ili aweze kuikabiri Dunia once am gone...
 
Kwanza eleza sababu za ww kutaka kitu hicho kwa maana mafuzo ya kijeshi yapo ya aina mbili
1 Mafunzo ya ukakamavu (military training)
2 Mafuzo ya Elimu ya kijeshi na utambuzi (Military intelligence)

Ww unataka yapi na pia kwa matumizi gani?
 
Huyu anataka military training.. just the basics...
 
Anataka kijana awe mkakamavu, aweze kukabili changamoto mbalimbali za maisha.
 
Huyu anataka military training.. just the basics...
Kama military training JKT wanafanya Scouts wanafanya Mgambo wanafanya huko kote mafunzo ya military na paramilitary training yanapatikana
Sidhani kama kuna umuhimu wa kutafuta chuo cha nje chuo kilichopo hapa ni kwa ajili ya maofisa wa kijeshi na usalama nje vipo vingi tu
 
Kwanza eleza sababu za ww kutaka kitu hicho kwa maana mafuzo ya kijeshi yapo ya aina mbili
1 Mafunzo ya ukakamavu (military training)
2 Mafuzo ya Elimu ya kijeshi na utambuzi (Military intelligence)

Ww unataka yapi na pia kwa matumizi gani?
mkuu, ningependa yote kama ulivyoanisha hapo juu. bahati mbaya sisi wakati tupo vijana hatukupata fursa kama hizi na siwezi laumu sana...kwa kuwa dogo umri unaruhusu, akipata mafunzo kama, Threat assessment and risk analysis, Firearms Training - Single operative (Pistol & Carbine), Land warfare: force-on-force with the use of FX Simunition and Advanced Firearms Training - Live Fire contatct Drills with VI na nyingine nyingi itapendeza. na ni kwa nia njema tu.
 
Jaribu kuangalia Sandhurst UK na West Point cha US, ingawa wanatoa mafunzo kwa askari kutoka nchi tofauti lakini kuna watu wanaenda kama private especially kutoka Middle East na nafahamu PKagame mwanae alimpeleka West Point ili akajifunze ukakamavu pia
 
Wana board, Heshima kwenu!
wakati taifa likiwa kwenye msiba mkubwa, nami naungana na ndugu na jamaa katika majonzi na masikitiko ya kuondokewa na vijana wetu, Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awarehemu na kuwalaza mahala pema peponi. Amen!

Pia, kwa kuwa JF ni kisima cha fikra na maarifa ningependa kujuzwa kama kuna military academy nchini Tanzania or kwenye nchi jirani kwa ajili ya private military training. Natafuta chuo cha kijeshi kwa ajili ya first born wangu ambaye amemaliza chuo mwaka jana. sikutaka aanze kazi kwa sababu maalum...natanguliza shukrani.

Si Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda wala Burundi ambako kuna Private Military Academies kama utakavyo Wewe. Nchi nyingi za Kiafrika Usalama wake ni mdogo hivyo Viongozi wengi ( namaanisha ) Marais wake huwa hawaruhusu ' Private Training ' kama hiyo kuwepo kwa hofu kubwa tu kwamba huenda siku moja hizo ' Njemba ' zilizofunzwa privately ' Medani ' za Kivita wanaweza ' wakawapindua '. Kwa wenzetu nchi zilizoendelea ( namaanisha Ulaya ) ambazo zimeshakomaa sana ' Kidemokrasia ' wao wanavyo hivi Vyuo binafsi na Watu huenda ' kujifunza '

Kwa kukusaidia tu na kukurahishia Kazi Mkuu nakuomba jitahidi umpeleke Mwanao huyo JKT kisha huko atafunzwa na kupikwa vizuri sana na si ajabu huenda Mwanao akionekana yupo vizuri Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) linaweza kumchukua ili aweze pia kulitumikia na kuilinda nchi yake nzuri ya Tanzania.

Hata hivyo nikushauri tu kwamba usimpeleke Mwanao huko kwa kumlazimisha kwani hutopata unachotaka Yeye akipate na utakuwa unapoteza rasilimali zako na muda wake isipokuwa kama huyo Mwanao kweli unaona ana mapenzi ya mambo ya Kijeshi basi wahi haraka sana ' kamtupe ' huko JKT ' Wanamume ' wamemtengeneze ili hata akirudi Kwako uweze kumsahau kidogo kisha uanze kujivunia kuwa sasa una Jembe la ' Kutukuka ' katika Familia yako.

Kila la kheri.
 
Hayo mafunzo yako ndo Yale ambayo TMA twaita
PT - physical training na AT - Academic Training ..?? Kama ni hivyo basi ajiunge na JKT baada ya kuhitimu wale madogo wa (OP Magu).

Kwanza eleza sababu za ww kutaka kitu hicho kwa maana mafuzo ya kijeshi yapo ya aina mbili
1 Mafunzo ya ukakamavu (military training)
2 Mafuzo ya Elimu ya kijeshi na utambuzi (Military intelligence)

Ww unataka yapi na pia kwa matumizi gani?
 
Jaribu kuangalia Sandhurst UK na West Point cha US, ingawa wanatoa mafunzo kwa askari kutoka nchi tofauti lakini kuna watu wanaenda kama private especially kutoka Middle East na nafahamu PKagame mwanae alimpeleka West Point ili akajifunze ukakamavu pia
asante sana mkuu, nitarifanyia kazi. ubarikiwe
 
mkuu, ningependa yote kama ulivyoanisha hapo juu. bahati mbaya sisi wakati tupo vijana hatukupata fursa kama hizi na siwezi laumu sana...kwa kuwa dogo umri unaruhusu, akipata mafunzo kama, Threat assessment and risk analysis, Firearms Training - Single operative (Pistol & Carbine), Land warfare: force-on-force with the use of FX Simunition and Advanced Firearms Training - Live Fire contatct Drills with VI na nyingine nyingi itapendeza. na ni kwa nia njema tu.
Kwa Tanganyika mafunzo hayo yanatolewa na Taasisi za Ulinzi na Usalama na ukipata mafunzo hayo ni lazima utakuwa ni mmoja wao tofauti na wenzetu ambao mafunzo ya kijeshi na ukakamavu ni sehemu ya mafunzo ya kawaida kabisa na kuna vyuo vinafundisha hasa vyuo vya VIP Protection College

Kama kijana wako unaweza mpeleka JKT au Scouts au Mafunzo ya Mgambo

Lakini mafunzo mengine uliyoyataja yanatolewa vyuoni (Military College) si kwenye military training grounds ambapo mara nying ni mafunzo ya ujasiri na ukakamavu na matumizi ya Silaha za Moto na Silaha za Baridi(Visu,kamba)

Nje kuna vyuo Lakini itakuwa ni ujinga kumpeleka mtu akasomee kitu ambacho hakitumii kwa manufaa ya kitaifa au kimapato au kiajira

Pia unaweza kumpeleka kwenye mafunzo ya mapigano wa miguu na mikono (Karate) Upanga nadhani kuna sehemu wanafundisha kule
 
unataka apate uzoefu gani kama vipi anze twishen ndogo ndogo kwa kuangali youtube namna mazoezi ya jeshi yalivyo pia kuna military flanks training(namna ya kukroo na movement in the squad)
 
Back
Top Bottom