mimi nina sifa zote unazotaka
Ni mkristo
umri miaka 32
Ni Mwana Chadema
Nimejiajiri (nina ofisi zangu zinazoniingizia kipato)
Ila tatizo moja tu elimu yangu darasa la 7.
sijui ntakufaa?
Absolutely.....
Lakini kwani kuna ubaya gani kumchunguza huyu nae kama ni walewale?
Unatafuta mchumba..go on,date nae kama hafai unamuweka pembeni tu.
Lakini trust me,naona kitu ndani ya huyu kaka....usimkatae.
Mimi pia ni mwanamke,na siwezi kukutumbukiza ktk shimo bovu,hebu fanya hivyo pls!!
Utakuja niambia,you'll never regret.
Labda uwe unatafuta mchumba msomi ambao wengi wamejaa majigambo na ujuaji mwingi na utajutia!
Hahahahaaaaa una hatari wewe?
Mwamke ninamashaka na imani yako?? Hivi ni nani amekuambia mume mwema anapatikana kwenye mitandao?? Kwa nini usisimame Katika nafasi yako na kumuomba Mungu akupe mume?? Kama ni mapenzi yako utampata huyo na hivyo vigezo vyako na mbele utakuja kulia na kusaga meno. Mkumbuke Mungu siku za ujana wako!
siwezi kukulaumu maana hicho ndicho unachoamini, kwani watu walioko mitandaoni sio watu wa Mungu? au ndio umekariri kuwa mwenza wako lazima umpate mahali fulani? mie sina mashaka na imani yangu and thats enough.
hahahaaaa! umenifanya nicheke aisee! unaonekana kuhadi mzuri sana.
ndio maana nimekuambia pale awali kuwa japo watu hutofautianaila hata yeye anaonekana ni mtu wa tambo sana, dont you see wht he wrote? read between the lines sisy
Kweli tena kamanda..wewe mbona sioni kama unatafuta..
Kamanda mimi nimeolewa na MABADILIKO.
uliwapiga vibuti vijana wenzako wakati unasoma kila wakikufuata uliwaona malofa kwa sababu hawakuwa na ajira wala pesa ukawaona ni nguruwe wasumbufu ukamegwa na vibabu vyenye wake zake bila kuzingatia future yako sasa uzee unakunyemelea mvi mpaka kwenye kwapa na kusikojulikana kwa wengi ndiyo unakuja unalialia hapa na kuanza kuweka vigezo kama wanaume unaumba wewe. watu wanatoa vigezo vyao humu unaleta shobo mwanamke mwenzio anakupa direction unajifanya unajua mioyo ya watu ?habari wana jf, kichwa cha habari chajieleza;
mimi ni binti mwenye umri wa miaka 28, mkristu,mweusi kwa rangi(chocolate), elimu yangu ni ya ngazi ya shahada, ni muajiriwa serikalini.
ninatafuta mchumba(mwanaume) mwenye umri wa kuanzia miaka 30 - 35, mcha Mungu,mkristu, elimu kuanzia shahada kwenda juu, aliyejiajiri au kuajiriwa,muelewa, muaminifu,muwazi na mkweli.
aliye na uhitaji kama mimi na aliye serious pekee ani-pm, tafadhali kama hauko serious just spare me with the trouble please.
akiacha kukusikiliza kwa ushauri huu atakuwa hataki mume anatania tu kupotezea muda watu.mimi sio kuwadi na sijawahi kuwa hivyo,nilijitahidi tu kadri ya uwezo wangu.
Moja kati ya sifa yangu kubwa ni nguvu ya ushawishi,kama huo ni ukuwadi basi sawa.
Yule kaka mimi nimemuelewa sana,wewe kama hujataka kila la kheri mamii...
Hii ndio jf bwana,bora anayefunguka hadharani kuliko magumegume yanayokuja huko pm kimyakimya.....sio waowaji!
Mwenyewe unaonekana mzoefu nadhani hili unalijua vyema,all the best.