Natafuta "Konki" wa Idara hii

Mimi nimesoma Biblia na Quran huu mwaka mmoja uliopita, huwezi kuamini nimelipata hilo jicho la kuona nyuzi 360, kuna mambo mengine nimeoneshwa mpaka kwenye ndoto na nikija kwenye uhalisia nayaona ni kweli kabisa. Mganga Mungu tu mkuu achana na hao matapeli kwenye ulimwengu wa shetani, atakuambia ya ukweli matatu na matatu ya uongo, mwisho wa siku inakuwa uharibifu kwako kwasababu kazi ya shetani ni kumuharibu mwanadamu na kumpoteza.
 
Ila huwa mnamkuza shetani bila kujua.
 

Yakobo 1:27 BHN​

Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
mkuu upo sawa hasa hapo mwishoni mwa hiyo yakobo..NA KUJILINDA MWENYEWE NA ULIMWENGU. me nakutakia kheri na ukifanikiwa si vibaya kutuludia kutupa ushuhuda nasi tujisaidie mana vgagula wanatutesa hakuna mfano!
 
Wakati MUNGU wa Israeli akitafuta watu wake mwenyewe, akituma watumishi wake kila mahali kuazia kugonga milangoni kwako uwafungie mlango, barabarani uvae earphones usiwasike, kwenye radio na TV ubadilishe channel, mitandaoni tena buure ufanye tu kuiginore (ukiombwa pesa kimbia),
tena kawaandikia na neno lake kwa lugha yako mwenye, tunajua MUNGU wetu anawaza nini, anapanga nini, atafanya nini, yani tuna ramani ya miaka 6000 kiganjani tumemulikiwa mwanga hatuko gizani hatudanganyiki hatupeperushwi na ulimwengu huu, tunajua tulipotoka na tunapoenda,

Huku mungu wa ulimwengu huu hapatikani meeen, ni mwendo wa konekshen tu, you have to know someone who knows someone, hapo upigwepigwe na matapeli weee ndo uje ukapande gari ushuke uchukue bajaji ushuke upande bodaboda, ushuke upande punda, ushuke utembee upande milima na mabonde, halafu mkitoka huko hata hatujui nini huwa kinatokea ni kimya kimya tu, hatupati ushuhuda, kwamba ushuda unakuwa wako kibinafsi ghafla tu unaona tunaanza kukukubali na kukupenda na kuvutiwa na wewe blaza hata kama ni jitu la hovyo kabisa tutapigwa upofu, hata kama ulikuwa fundi mahiri wa simiens unataka tuvutiwe tu wakati umepitwa na muda sahivi tuna smatifoni badala upewe akili u upgrade unapewe mvuto tu watu waendelee kununua simiens ili tuje kwako,

Lakini shetani!

Post in thread 'Kabla wamisionari hawajaja Afrika na kufundisha kuhusu mbinguni na kuzimu wazee wetu walikuwa wanaenda wapi?' Kabla wamisionari hawajaja Afrika na kufundisha kuhusu mbinguni na kuzimu wazee wetu walikuwa wanaenda wapi?
 
Mmh mmh
 
Mnamfanya ionekane shetani kama ana nguvu sawa na Mungu isipokuwa tu yeye shetani nguvu zake mbaya, kila jambo baya mnalifanya kuwa ni nguvu ya shetani. Huyo shetani kwa imani ya waislamu huamini kuwa anafungiwa mwezi wa ramadhani lakini ukiangalia bado watu huwa wanafanya maovu kama kawaida.
 
"Mganga mkuu ni Mungu",hapa sasa umenichanganya,mganga mkuu ni nani sasa kati ya Allah na Jehovah maana umesema biblia na Quran zimekupa jicho la kuona 360
 
Kitu wasichokijua watu ni kwamba kupata mganga sahihi kwa tatizo lako husika si kitu rahisi.
 
Fika bunju mtaa wa Basihaya mtafute mtu anaitwa Abubakar Katwila almaarufu Q CHILLA nadhani anaweza kukusaidia maana washirikina wengi wamemsifia mizimu ya nchi kuwa imetia nanga kwake kwasasa

Akishindwa panda gari elekea mkoa wa rukwa ukifika Namanyere ulizia gari au pikipiki za kufika kata moja inaitwa KiRANDO ukifika hapo mtafute diwani wa zamani wa kata hiyo bwana KESSY mueleze shida yako nina hakika atakupeleka kwa mganga mzuri mno yupo kisiwa fulani kipo karibu na kata hiyo utasaidiwa

Ukifeli huko basi panda gari mpaka Songea mkoani ruvuma ukifika huko ulizia kambi ya jeshi inaitwa CHABRUMA hakuna sheria kuingia ,ukishaingia omba yeyote hasa raia wanaokatiza humo kuwa unahitaji kifika kwa mganga Sameje huko Mpitimbi watakatisha humo humo mpaka mpitimbi utasaidiwa.

Ukifeli huko basi panda gari mpaka mkoa wa Kagera ukifika bukoba mjini ulizia kwa bodaboda kuwa unahitaji kwenda kwa mganga wa kienyeji anitwa BISHANGA yupo nje ya mji sehemu inaitwa KAGONDO KAIFO utatibiwa na utakuwa sawa .

Najua unaweza usiwe na bahati kote huko basi njoo mbeya ukifika mbeya mjini ,nenda mpaka mji md9go wa mbalizi ulizia stendi za umalila ukifika stendi hiyo panda gari zinazoenda Isuto ukifika isuto muulize bodaboda yeyote kuwa unaenda kwa mganga anaitwa NAMBALI ,ukifika kwa huyo mama mwambie umeagizwa na nyoka ,basi hata maji ya kuoga utapewa ukitibiwa rudi hapa kunishukuru .

Basi umefeli kabisa nauli huna ,baki hapo Dar ila nenda wilaya ya temeke ,uliza kata ya keko ukifika keko ulizia keko machungwa ilipo nenda mpaka lilipo gereza la keko muulize hata mpita njia kuwa unapatafuta kwa mama kyembe ,ukimpata huyo mama mwambie nyoka amesema nikuulizie alipo mganga basi utasaidiwa kwa kupelekwa kwa mganga .

Ukibahatisha hela na bado ukawa haujapona basi rudi Mwanza mpaka mwanza mjini panda gari za kwenda kisesa ,ukifika kisesa ulizia ulipokuwa mji wa mzee Limbe ,wakikuonesha hapo ni ruksa kumuuliza mtu yeyote kwa mganga konki watakutajia wengi wa pale ila mmoja atatajwa kwa jina gumu la kisukuma ni huyo huyo nenda haraka.


Ukifeli basi panda meli sijui siku ya jumanne uende tena bukoba mjini ukifika panda gari za kwenda mpakani huko MUTUKULA ukifika mutukula tafuta kwa wauza mchele maarufu au myafute bwana mmoja anitwa FAUDHI ,mwambie nyoka amesema unifikishe kwa mtaalamu utafikishwq ni mtaa wa pili utatibiwa ukipona nenda hata Uganda kidogo ukawaone akina Atwoki .

Ukifeli na huko utarudi mbeya mpaka Tunduma mkoa wa songwe uende mpaka mpemba ,umdake mpiga debe yeoyote nwambie mambo hayaendi akupe mtaalamu hayupo mtaalamu utayepewa zqidi ya mmoja ,herufi yake itaanzq na F .

Nadhani kwa kuzunguka hivyo utakuwa umepata tiba yako ila ikifeli basi nitakupeleka ARUSHA ,CHUNYA ,IRINGA ,NJOMBE ,KAHAMA NA SIMIYU mimi mwenyewe ukifeli hapo nitakuomba ukubali jambo lako ni la Mungu mwenyewe .

Ahsante na pole kwa kuugua .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…