Natafuta Kazi: Nina Masters ya Education Management and Administration

Out of point: Binafsi sioni umuhimu was kusoma masters degree wakati huna direction baada ya kumaliza itakuwaje hata kama mtu akiwa ameajiriwa

Mi nadhani msoto wa masters (msuli wa coursework, assignments, U.E , research + stress za malecture )+ gharama bora utumie katika kupambania bachelor yako mtaan.

Masters hutakiwi kusoma na stress za ajira / pesa za kujikimu etc

That's ukitembelea block za masters students unakuta wamapeki mikoko yaani hawana stress za za pesa za nyanya

All in all pambana na usichague hata ukipata shule ww piga pindi
Ni kweli apunguze pia uchaguzi
 
Hujanielewa Tajiri,

"Masters" ni hatua katika kisomo cha elimu, lakini sio uthibitisho wa uwezo wa mwenye masters katika utendaji wa fani husika.

Masters ni bure ikiwa utendaji wa mwenye hiyo masters ni sawa na mtu mwenye "Bachelor".

Nikujuze tu, waajiri wengi wanategemea kama una "masters" basi pia una experience ya masters hiyo but sio mtupu ndio unaenda kujifunza kazi.

Hivyo waajiri wanaajiri mtu mwenye 'uwezo', "masters" ni hatua tu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbona wengine masters ndio zimewapa ajira tena bila experience. Acha kukatisha watu tamaa kwa sasa degree ni kama form6 tu. Sasa jichanganye kwenye interview ukutane na mtu mwenye gamba la masters uone kama utasalimika.
 
Mbona wengine masters ndio zimewapa ajira tena bila experience. Acha kukatisha watu tamaa kwa sasa degree ni kama form6 tu. Sasa jichanganye kwenye interview ukutane na mtu mwenye gamba la masters uone kama utasalimika.
Bure kabisa wewe.

Kwa hiyo kwenye usaili "gamba la masters" ndilo huwa kichocheo kwa mtainiwa kufanya vizuri?

Wacha uwongo kabisa.

Ikiwa nafasi ya kazi inataka mtu mwenye degree moja ikiwa utatokea na digrii zako mbili unapigwa chini. Usikatishe tamaa wenye digrii moja.

Kila hatua na cheti husika kina nafasi yake kwenye soko la ajira. Hata kidato cha nne, darasa la saba pia wanaajirika katika nafasi zenye uhitaji huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona wengine masters ndio zimewapa ajira tena bila experience. Acha kukatisha watu tamaa kwa sasa degree ni kama form6 tu. Sasa jichanganye kwenye interview ukutane na mtu mwenye gamba la masters uone kama utasalimika.
Hizi zote ni stress za kukosa ajira. Pambana na hali na hiyo masters yako
 
kwani yeye research alizokua anafanya ali base kwenye nini ili azitumie hizo hizo kutatua matatizo ya ukosefu wa ajira unao mkabili.
 
Ngoja nikuelezee kasimulizi kangu kafupi mwalimu mwenzangu unaweza kupata chochote

Nikiwa npo kidato cha tatu shule ya boarding mkoani dar es salaam (private and islamic school) kuna jamaa alkuwa na undugu ya manager wa shule akatokea kuwa jamaa saana mpaka leo hii jamaa ndo kawa mentor wangu.

Huyu jamaa nikiwa kidato cha tatu alkuja shule akiwa analia na kusaga meno..mm nikiwa namfanyia solving dada m1 hivi ambae wana undugu na huyu jamaa akanitonya na kuniambia jamaa analia kwa sababu ameferi mtihani wa kidato cha nne..mimi nikatoa pole nikampotezea coz jamaa alkuwa anaile kujifanya mkubwa nini na kutuchapa chapa sie wadgo.

Jamaa alienda kusoma certificate ya ualimu. Katika chuo flani cha kishamba tu, yaani jamaa alipomaliza na chuo kikafungiwa na serikali kwa kukosa vigezo.

Mm niliendelea nikamaliza form 4 na division 1 yangu then six na division 1 yangu..nikaenda ualimu chemistry and bio (kiukweli ualimu ulikuwa umenikaa koooni kweli kweli..yaani nilikuwa nauenda ualimu kiasi kwamba nilianza kufundisha since nlipomaliza form 4)

Nilipomaliza chuo nikaajiriwa katika shule niliyomaliza form 4..yule yamaa yangu akawa anakuja mara kwa mara na ananikuta mie pale napiga chaki kama sina akili nzuri. Ila mimi nikimchek naona jamaa ana kigari kidgodogo na maisha kimtindo flan kama yanamuendea fresh.

Basi akija pale ananitania tania na kukumbushana maisha flani ya kiskul alipokuwa anatuchapa chapa..mara akijisifu kwa staff wenzangu kuwa mimi ni mwanafunzi wake. Mimi nikawa namchukulia poa ila nkavutiwa na maendeleo yake kiuchumi na pia alikuwa hafanyi kazi kwenye taasisi ninayofanya kazi mie japo ni ya kaka yake.

Basi siku moja nikaamua kuongea nae jamaa akasema mimi sitak niongee na wewe kwa maneno naomba weekend nkutembeze kwenye miradi yangu..jumapili nikamchek jamaa akanitembeza, mawazo yangu nilijua labda jamaa ana maduka au namna gani kumbe jamaa ana SHULE MOJA primary na nusury schools km sita hivi.

Mimi nikamwambia "aah kaka yake amekupa hii shule uiendeshe?" Jamaa akasema "NO yeye alinipa maarifa tu ya namna ya kuanzisha shule hata kama huna pesa nying kivile"
Nikamuuliza teena "unaweza kuiendesha shule kubwa kama hii pamoja na nursury 6 ukizingatia elimu yako"
Jibu ndogo tu akanipa "nmeajiri watu"

Nikambeleza saana jamaa anifungue ubongo, ukizingatia jamaa ana certificate ya ualimu na hata hvyo hyo certificate haitambuliki na serikali, mimi na digree yangu ya ualimu ya upper second kutoka chuo kinachotambulika.

Basi jamaa akazingatia ukaribu wangu mie na yeye na pia uchu wangu wa mafanikio. Akaanza kunipa darsa kama ifuatavyo

  1. Mbinu za kutafuta vituo vya kielimu (nursury, shule)
  2. Utaratibu wa kuandaa mkataba na aina za mkataba.
  3. Utaratibu wa kuingia mkataba na mmiliki wa shule.
  4. namna ya kuanza kuendesha shule ukiwa una mtaji mdgo.
  5. Njia za kupata wanafunzi (bila ya kuzingatia matokeo ya shule, hata miundo mbinu)
  6. Mikakati ya ufaulishaji.
  7. Kujitanua.
Kiukweli ilinichukua miezi 6 nikiwa na dhamira ya dhati kabisa kuwa nitaanzisha hichi kitu lazimaaaaaaaaa.

Mpaka sasa nimeanzisha na nina nursury 8 japo sijawah hata kufundisha nursury school ila nmeajiri walimu 16 na wasimamizi wa hizo nursury 2 mie npitia pitia tu kwa mwezi mara 2 au 3.

Utahoji kuhusu mtaji, binafsi nilianza na mtaji wa 500,000 ambao ulikuwa ni sehem ya mshahara wangu. Na nilianza na vituo viwili tu ila namna nilivyoviweka, kuna wamiliku walikuwa wananifuata wao wenyewe niingie nao mkataba.

Kwa sasa baada ya kutoa matumizi na mishahara sikosi japo 3mil ya kuendeshea maisha yangu na mda huo kazi zangu nyingne zinaenda.( ila kwa hii corona tunasulubika wote kwa sasa 😅😅😅😅)

Mipango yangu ya baadae niingie mkataba na primary school ili wanafunzi watokao kwenye nursury zangu niweze kuwaingiza kwenye shule yangu sio kuwauza kwa shule nyingne kama nifanyavyo sasa. Pia mwakani nifunge mkataba wa uendeshaji wa secondary coz huko ndo nina uzoefu wa kutosha wa uendeshaji.

Kwahyo mr mwenye masterz ya kinini sijui jaaribu kuangalie nje ya box, tafuta waliofanikiwa nje ya mfumo rasmi wa elimu waombe mjadala. Halafu kimtindo flani hzo sifa zako za kujinadi una master ungekausha kwanza. Kwasababu unafanya watu wadharau tasnia ya elimu kwa kuona mastez holida anazagaa mtaani.

Yaani wewe ukikutana na huyu jamaa alienifunua ubongo na kuutia kidole ili uamke....daaaaahhh ndugu yangu anaweza kukushangaa na akatukana mfumo mzima wa elimu yetu.
 
Ndugu,

Mimi ni kijana wa Kitanzania na mwenzenu humu kwa miaka mingi kidogo nina masters ya Education Management and Admistration natafuta kazi wakuu associated na fani yangu husika hasa katika maswala ya utawala, rasilimali watu na mipango kama kuna mkuu yeyote yupo sehemu wanauhitaji huu au anaweza nisaidia natanguliza shukrani nyingi kwenu.
Mmmh kwani kwenu Apo akuna Kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Humu utaambulia kejeli za "masikini wenye hela".
Take your time kuwasiliana na ma HR wa Taasisi zinazohusiana na kazi unazotaka, wasiliana na watu uliosoma nao wajulishe challenge yako na uwaombe ushauri(usione aibu), rudi hata pale chuo onana na wakuu wa department kuomba ushauri(narudia,usione aibu).Sambaza CVs katika recruitment portals mbalimbali.
Humu utakutana na wajuaji ambao wanaandika kitajiri wakati hapo nyuma kidogo baba wa baba zao walikuwa wachunga mbuzi na wakulima wa jembe la mkono😃.
 
Humu utaambulia kejeli za "masikini wenye hela".
Take your time kuwasiliana na ma HR wa Taasisi zinazohusiana na kazi unazotaka, wasiliana na watu uliosoma nao wajulishe challenge yako na uwaombe ushauri(usione aibu), rudi hata pale chuo onana na wakuu wa department kuomba ushauri(narudia,usione aibu).Sambaza CVs katika recruitment portals mbalimbali.
Humu utakutana na wajuaji ambao wanaandika kitajiri wakati hapo nyuma kidogo baba wa baba zao walikuwa wachunga mbuzi na wakulima wa jembe la mkono😃.
asante mkuu umeongea hoja nzur mno
 
Back
Top Bottom