Natafuta kazi; Embroidery machine operator

Natafuta kazi; Embroidery machine operator

The Salt

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
391
Reaction score
1,038
Wakuu nimeona niwe specific kwenye kila eneo ninalolimudu,kuandika sana kunachosha watu kusoma neno kwa neno. Kama Kichwa cha habari kilivyojieleza hapo. Mimi ni mtaalam mzuri katika kuandaa na kudarizi nembo/logo mbalimbali kwenye mashati,tisheti,kofia, na nguo aina zote kwa kutumia mtambo wa kisasa katika kudarizi (Embroidery Machine),pia ni mtafutaji mzuri wa masoko katika upande huo huo wa Embroidery.

Naomba ajira/kibarua kwa yeyote mwenye mashine/ofisi inayojishughulisha na kutoa huduma hii ya Embroidery. Nipo tayari kufanya kazi katika Mkoa wowote Nchini (Preferably Mikoani)
Yawezekana una ofisi mpya inahitaji mtu wa aina hii,tuinuane.
Jinsia yangu ni ME
Umri; Above 30
Makazi; DSM
Mawasiliano; PM au nipigie 0788 947 354
Nitashukuru sana.
Terms and Conditions za Mwajiri nitazizingatia
 
Hiyo mashine inauzwa bei gani
Mashine hizi aghalabu zina bei.
Na mbei nzuri zipo kwa mashine za kichina na zinafanya vizuri sokoni pia
Kwa kuanzia mashine ya vichwa viwili tu inauzwa kuanzia shilingi za kitanzania milioni 16 hadi 18 kulingana na brand hadi inakufikia mlangoni na kuanza kazi. Sasa zipo mashine za Vichwa vinne,sita,nane,10,20 na kuendelea.
 
Zinaweza kuanzia bei gani, na soko la bidhaa zake zikoje
Soko lake lipo na demand ipo so ni wewe kuyatafuta masoko tu na kuangalia maeneo au mikoa ambayo hizo huduma ni adimu sana. Mikoa kama Dsm,Mwanza,Arusha na Dodoma hizi mashine wanazo sana ila mikoa ya Pembezoni kama Kigoma,Sumbawanga,Tabora,Shinyanga (Shinyanga zipo mbili tu,moja Shinyanga Town na nyingine Kahama) Katavi,huko Njombe nk. Mashule binafsi ya Mikoani mengi yanapeleka sare Kenya na Dar kwa ajili ya Embroidery kwa sababu walipo hakuna huduma. Na kama ujuavyo,wenye mawazo hatunaga hela na wenye hela wanaona kuwekeza kwenye wazo la maskini ni kupoteza hela.
Hadi uwe na interest
 
Mashine hizi aghalabu zina bei.
Na mbei nzuri zipo kwa mashine za kichina na zinafanya vizuri sokoni pia
Kwa kuanzia mashine ya vichwa viwili tu inauzwa kuanzia shilingi za kitanzania milioni 16 hadi 18 kulingana na brand hadi inakufikia mlangoni na kuanza kazi. Sasa zipo mashine za Vichwa vinne,sita,nane,10,20 na kuendelea.
Hapo parefu sana, inabidi kujipanga; ila kama soko ni la uhakika, ambalo linaweza kukuingizia angalau m 3 kwa mwezi, unaweza kujiripua kwa kuchukua mkopo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom