Natafuta fundi wa kuniwekea USB PORT kwenye music system

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,945
724
Heshima kwenu wakuu
Nina Music System aina ya Sony toleo la zamani ambazo hazina usb port ila inacheza tape za kawaida na dvd
Nauliza kama naweza kupata fundi wa kuimodify kwa kuiwekea usb port japo ya mp3 mimi nipo Mwanza.
 
Hiz ndio naunda mm, kuanzia mwanzo mpaka mwisho
 
Attachments

  • WP_20160324_006.jpg
    WP_20160324_006.jpg
    106.1 KB · Views: 51
Acha uongo, haiwezekani. Kwani kinachofanya redio isome USB ni port?
Binafsi sio fundi ila najua inawezekana kwa mafundi wajanja sasa bila usb port hiyo usb utaichomeka wapi mkuu nisichojua kama zipo zinazoweza kusoma mpk dvd files
 
inawezekana kama fundi mzoefu wa electronics, huwa inatumika universal DVD circuit (main PCB) . Kwa wasioijua universal DVD main pcb, ni ile machine kuu inayotumika kwenye deki za DVD -DVD player. Zipo zenye USB port na zipo zisizo na USB.

Sasa hapo inatakiwa utumie yenye USB port na unafanya modification kuifunga ndani, na redio yenyewe itatumika kama AMPLIFIER tu!. Cha muhimu ni kuweka switch ya kubadilisha kwenda kwenye hiyo system ya DVD na pia namna ya hiyo DVD board kupata power (umeme- voltage zinazohitajika) pia sometimes ikibidi unafunga na powersupply yake humo humo ndani ya redio. n a powersupply hiyo inaweza kuwa ni powesupply ya universal ya DVD player.

hata redio za gari zinafanyiwa modification siku hizi , unaweza kubadili redio ya gari ya MP3 na ikawa na uwezo hadi wa kuonesha VIDEO.

Vyote hivi ni kwa hisani ya CHINA.
 
Mkuu we ndo unafanya hii kazi au?
 
Heshima kwenu wakuu
Nina Music System aina ya Sony toleo la zamani ambazo hazina usb port ila inacheza tape za kawaida na dvd
Nauliza kama naweza kupata fundi wa kuimodify kwa kuiwekea usb port japo ya mp3 mimi nipo Mwanza.
Kama alivyotolea maelezo mkuu ymollel hapo juu,
Hilo linawezekana. Unaweza kuzitumia hizo universal USB circuit boards(ziko ready made). Unachohitaji kukifanya ni kutafuta 5volts kutoka kwenye circuit ya hiyo system yako. Kama hazipo basi ni suala la kufanya regulation kutoka kwa power supply(kumbuka, hizi USB circuits hutumia volt 5 tu na si zaidi). Lakini pia zipo usb circuit boards ambazo hufanya kazi kama transmitter, unachokifanya ni kuziingizia tu umeme(5volts DC.) Zenyewe hufanya kazi kwa kurusha (kuzi-transmitt hizo nyimbo ) kwenda kwa FM(utalazimika kuiseti radio yako kwenda kwa FM) na kuityuni ili kizipata frequency za hiyo USB circuit board,
Na hapo unakuwa, GOOD TO GO!...
PIA, zipo usb circuit boards zingine ambazo huwa na switches za inputs(modes), forward, backward, equalizer. You simply identify the vcc, ground, input and output signal terminals and supply them to it. And there again you are GOOD TO GO...
AHSANTE
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom