natafuta barafu kwa ajili ya sherehe-DSM

trplmike

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
701
775
wana JF ninategemea kuwa na sherehr ndogo nyumban tarehe 1 January.
ni wapi nitapata barafu kwa ajili ya kupooza vinywaji?
msaada tafadhali
 
Nenda ferry kwenye soko la samaki huko utapata ice blocks
 
Kuna jamaa wanaitwa Tanz Ice wako opposite na Efatha Bank Mwenge. Namba zao ni 0652-206862. Mfuko mmoja wa kilo 5 nafikiri wanauza Tsh 1000. Leta mrejesho kwa manufaa ya wadau wengine.
 
wana JF ninategemea kuwa na sherehr ndogo nyumban tarehe 1 January.
ni wapi nitapata barafu kwa ajili ya kupooza vinywaji?
msaada tafadhali
Kuna mtu nilimsikia akisema yanapatikana maeneo ya keko...pale furniture..
 
Vichekesho vingene bhana, kama umeme hauna, friji hauna unatafuta mambo makubwa ya nini, wape vya moto hivyo hivyo, sana sana ukivinunua tumbukiza kwenye ndoo ya maji ya kawaida vitapoa tu.
 
Vichekesho vingene bhana, kama umeme hauna, friji hauna unatafuta mambo makubwa ya nini, wape vya moto hivyo hivyo, sana sana ukivinunua tumbukiza kwenye ndoo ya maji ya kawaida vitapoa tu.
lol... nina vinywaji vingi.. havitaenea kwenye fridge.. ila umeme ninayo na fridge ninayopia
 
Kuna jamaa wanaitwa Tanz Ice wako opposite na Efatha Bank Mwenge. Namba zao ni 0652-206862. Mfuko mmoja wa kilo 5 nafikiri wanauza Tsh 1000. Leta mrejesho kwa manufaa ya wadau wengine.
shukuran mkuu. nimewapigia wamesema wanayo. ila tarehe 1 hawatafungua.. thanks again
 
shukuran mkuu. nimewapigia wamesema wanayo. ila tarehe 1 hawatafungua.. thanks again
Pamoja sana mkuu. Hapo ndio tunapokosea wabantu,tarehe 1 ilipaswa wafungue maana ndio siku ya mahitaji ya hiyo bidhaa. Other option Kama una deep freezer unaweza kununua a day before ukaziweka kwenye freezer kwa matumizi ya tarehe 1 Jan.
 
Mrejesho..
kama mlivyonishauri niliamka mapema nikawa ferry. kufika tuu wakati natafuta parking madalali wakaniwahi. nikawaaambia natafuta barafu.. wakati ninapark vizuri jamaaa wakawa wamefika na barafu ya kilo 50 hvi. nikawaambia sh ngapi? wakaniambia elfu 35. machale yakanicheza. wakat bado naendelea kushangaa shangaa pale. wakawa wanabishana wenyewe kwa wenyewe. nikawaacha nikaenda mwenyew kwenye contena wanalouza barafu. kuuliza bei naambiwa elfu 10.
nikalipia barafu kurud kwenye gar nakuta jamaa wsmeshaingia mitini
note.:kuwen makin sana na madalali.. hawana huruma hata kidogo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom