Kanyagio taratibu tu usiwe na wasi humu kuna watu waliobobea kwenye mambo hayo utashindwa wewe tu. Labda nikuulize kidogo unapanga kulima nini zaidi ya mitiki maana kila mkoa una hali ya hewa na mahitaji tofauti na mwingine. Ukishajua hilo ndipo inakuwa rahisi kukadilia bei ya shamba kutokana na eneo unalopendekeza.
......................................
Amani yetu inatumiwa vibaya
Mitiki inasitawi vizuri Mheza tanga! Kwa vile kuna shamba la serikali la mitiki huku upatikanaji wa vipando ni rahisi na pia kama utahitaji ushauri wa kitaalamu kuna watalaamu wapo huko!
Pia kilimo cha mpunga kinalipa sana, tafuta mashamba Morogoro hasa wilaya ya Ifakara kwenye bonde la mto rufiji!
Wakuu natafuta sana ushauri maana nataka kupanda ile miti ya muda mfupi, say 4-5 years nivune; ni ya aina gani na ardhi ipi inafaa?
Je alizeti inastawi mkuranga?
Mitiki inasitawi vizuri Mheza tanga! Kwa vile kuna shamba la serikali la mitiki huku upatikanaji wa vipando ni rahisi na pia kama utahitaji ushauri wa kitaalamu kuna watalaamu wapo huko!
Pia kilimo cha mpunga kinalipa sana, tafuta mashamba Morogoro hasa wilaya ya Ifakara kwenye bonde la mto rufiji!
nani anafahamu jina la kitalamu la mitiki ili niweze kutafuta taarifa zake hapa kwenye GoogleKimsingi miti ya kuvuna ndani ya miaka hiyo unayosema kwa Tz haipo,labda milonge,au kama unataka kupanda mitiki/milingoti(saligna au grandis) ili uvune kama boriti unaweza, itabidi utafute ardhi yenye maji mengi. Lakini kama unakusudia kuvuna kama mbao,hiyo miti haipo.
Kuna taasisi moja ya Uingereza inafanya mipango ya kuleta pines za miaka 5 kule Kilolo inaitwa NEW FOREST,lakini mbegu hizo ni za maabara,na ni mahsusi kwa ajili ya pulp. Je ukikosa mnunuzi wa pulp utafanyaje mkuu? Kwa sasa mbegu hiyo ya Pulp ipo,ila kuwa makini.
Aliozeti zinamea sehemu kubwa ya Mkuranga,tatizo ukame mkuu wangu. Ila kata ya Talawanda kule Bagamoyo kuna ardhi nzuri kwa alizeti.
Je kilindi ni kilimo aina gani kinakubali? aidha, nimesikia baadhi ya members wanaongelea samaki wa kufuga,... naomba msaada wenu kupata maelezo zaidi katika hili..
Kilindi kuna kilimo cha nafaka na matunda. Kama unataka mambo ya samaki fuatilia thread ya bwawa la samaki,kuna mjumbe alijitolea kutusaidia ili tumpate mtalaamu husika. soma hiyo thread.
nani anafahamu jina la kitalamu la mitiki ili niweze kutafuta taarifa zake hapa kwenye Google
kama nnataka mali mtaipata shambani