Pole mkuu pia hongera. Wenye hobby ya kutengeneza mitambo, hukutana na changamoto nyingi kwenye nchi zetu zinazoendelea. Kama issue ya upatikanaji wa motor imekuwa tight sana, anza kucheza na gear ratios. Tafuta gear box ambayo inatumia motor ya speed kubwa, lakini output yake ni the same na unayotaka kuendeshea machine yako. Nadhani upatikanaji wa gear box siyo issue sana tho sijawahi kuchakura soko. Pia unaweza hata jaribu diff ya gari. Ila the best solution ilikuwa ni kutumia VFD kama alivyosema mdau hapo juu. Unatumia motor yoyote, then unajipimia unachotaka. Lakini hiyo naona ni gharama hasa kwa project zetu hizi za kuelekea uchumi wa kati. Natumaini umenielewa mkuu na nitafurahi ukifanikiwa.