Bradha
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 8,787
- 45,248
Pole sana Abbitto .Natumaini mu wazima hata kama sio mia kwa mia lkn pumzi ipo.Mwenzenu nina shida hasa inayonikosesha furaha ya maisha maana nimeolewa mwaka Wa tatu sasa sijafanikiwa kupata mtoto,sijawahi kutoa mimba ila nimekunywa dawa nyingi za mitishamba bila mafanikio.Mwaka Jana mwishoni nilienda hospitali wakagundua nilikuwa na fungus kwenye kizazi na mirija yote ilikuwa imeziba,walinipa dawa za kutibu iyo fangas na niliona mabadiliko na pia walinizibua mirija nayo pia niliona mabadiliko.Sasa ni miezi mitano imepita bado sijashika mimba,sasa bas najua humu kuna madoctor au wahanga ambao waliwahi kupitia hali kama yangu Kwa kweli naomba msaada wenu.natanguliza shukrani zangu za dhati
Sent using Jamii Forums mobile app
Miezi mitano bado ni michache kwa wewe kupata wasiwasi hata kama umepona.Hivyo endelea kusubiria.Wataalamu wanasemaga mtoto atakuja tuu akitaka kuja, hivyo usipanick wala kuwa na mawazo sana utapata mwanao.Hakikisha mnafanya yale mambo kila unapoweza usisubirie hadi pale unapohisi wewe(au kuona) kuwa upo kwenye siku za hatari.Usimpimie
Pili, muombe na mmeo apime, na muende wote kupima.Ikiwezekana wewe ndiye uamue mnaenda kupima wapi;Nadhani umenielewa kwanini nimeshauri wewe ndiye uamue wapi pa kuchukulia vipimo...
La msingi usistress; ndugu/majirani/marafiki wanaweza wakawa wanauliza sana kuhusu mtoto na pengine wengine wanatoa kauli zisizo sahihi ila cha msingi usiwaze sana wanasema nini, furahia maisha, relax Abbitto .
I pray that mfanikiwe, mjaliwe hata mapacha.Sisi tunasubiria mrejesho hapa.Ukileta mrejesho utaniambia unaitwa mama nani.