Serikali ya awamu ya tano imekuwa inajinadi kuwa si ya kisiasa bali ni ya kiutendaji zaidi. Na President amekuwa akisema yeye ni msema kweli na anaamini kuwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Kwa dhana hiyo tu niliipa imani yangu na kuitetea mbele ya watu wanayoipinga. Hata pale ahadi ya serikali ya kushughulikia wafanyakazi hewa kwa miezi miwili ilipofeli niliyaelewa maelezo ya serikali kuwa tatizo ni kubwa kuliko walivyodhani.
Tulio na imani na serikali tulijipa mda wa kutosha kuwa atleast January 2017 italipa stahiki zilizosimamishwa ikiwa imeshamaliza uhakiki, HAIKUWA.
Tukasema tusubiri bunge la Feb tupate maelezo rasmi ya serikali kupitia kwa wawakilishi wetu, serikali ikakiri kumaliza uhakiki. Tukatumaini kwa kuchelewa basi April italipa, Holla.!!
Tukabashiri Serikali inajipanga kufanya fresh start ktk bajet mpya ya 2017/2018 ili July kieleweke, HAIKUWA
Serikali ikatoa maelezo bayana kuwa kilichokuwa kinatatiza ni rufaa za vyeti na kwamba hatma yake ilikuwa 30,Sept na kwamba tayari serikali ilikuwa imetenga fedha kwa ajiri ya increament na madaraja ambayo yangelipwa baada ya Septemba 30.
Hivyo mimi na watumishi wenzangu wenye nasaba kama zangu tnasubiri Oktoba hii.
Lakini kwa hii 'verse' mpya ya Mkuchika naanza kuwa na wasiwasi iwapo serikali hii ni ya 'wasemakweli' na 'watendaji' watatekeleza Octoba hii.
Baada ya Oktoba kupita bila increament na madaraja yaliyosimamishwa kurejeshwa, mtazamo wangu na wenzangu juu ya serikali hii utakuwa tofauti kabisa (hata kama malipo hayo yatafanyika April kabla ya Mei Mosi ambayo ni kejeli kabisa) nitajua tu kuwa sasa wafanyakazi tutakuwa tumegeuzwa punching bag ya serikali dhidi ya raia jambo ambalo ni unafiki, na tutafanya kazi kinafiki kweli..
KUTOKA NDO HATUTOKIII..!!!
UPDATE..

Postponed to November
Ok let's make it November, hata si mbali mbona