CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,781
- 6,065
Kwanza nimshukuru Mungu kwa uzima na uhai ambao anatupa kila siku, kama alivyotuahidi mheshimiwa Rais kuwa "hatatuangusha" wafanyakazi na watanzania kwa ujumla ninaamini hotuba yake hii itakuwa majibu kwa wafanyakazi kote nchini.
Yapo mambo ambayo binafsi nasubiri kwa hamu kubwa kusikia ufafanuzi kutoka kwa mheshimiwa rais.
1. Ni muda gani haswa ulipangwa kwa ajili ya zoezi la uhakiki? mwezi mmoja, mwezi mmoja na nusu au miwili au mwaka mzima? kutokana na waraka ule ule wa juni 13, 2016 zoezi lilikadiriwa kutozidi miezi miwili lakini tunaambiwa jana tar 28 ndo raisi amepewa ripoti!
2. Bodi ya mishahara, mwaka jana mwishoni, waziri wa utumishi akihojiwa na kituo cha ITV kwenye dakika 45, aligusia swala la bodi ya mishahara akidai kuwa wanasubiri uchaguzi wa tucta ili wapate baadhi ya wajumbe, natumaini mheshimwa raisi ataolea ufafanuzi hili.
3. Nyongeza ya mishahara kwa mwaka huu unaoisha, ni wazi kuwa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi imeweka sawa suala la nyongeza kuwa itakuwa kila mwaka tar 1 julai, sasa kutokana na sakata la uhakiki hakuna nyongeza iliyotolewa, na kwa kuwa watumishi halali wapo na wanafanya kazi kwa bidii ni nini hatma ya nyongeza yao kwa miezi hii 10, naamini raisi pia hatakaa kimya katika hili.
4. Waliopanda madaraja na kupandishwa vyeo kisha wakarudishwa nyuma, wapo wafanyakazi ambao walikumbwa na kadhia hii na hadi leo wanaendelea kusota naamini raisi atatoa ufafanuzi ikiwemo kuamrisha walipwe haraka arrears zao.
5. Suala la uhamisho, ingawa juzi hapa waziri simbachawene aliruhusu uhamisho kwa watumishi ambao wanafuata wenzi wao lakini bado huku katika halmashauri zetu suala hili bado halijawekwa wazi.
6. Matarajio mapya ya wafanyakazi kwa mwaka 2017-2018, asilimia kubwa ya wafanyakazi matarajio yao sasa yapo kwako mheshimiwa raisi, tumeishi kwa tabu kwa mwaka huu na tumeonyesha uzalendo wa hali ya juu na wewe mheshimiwa raisi unalijua hili! ni wakati wako sasa kufanya kile ulichokusudia...tunakusubiri kwa hamu!!
Ubarikwe sana.