Nasubiri CCM tutangaziwe tarehe ya kuchukua na kurudisha fomu kama walivyofanya CHADEMA

afsa

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
1,983
1,574
Dirisha la nafasi ya kugombea urais ndani ya CHADEMA limefunguliwa rasmi Leo. CHADEMA safari hii wameamua kuzuia waviziaji kama mamvi.

Ni raha sana kwa Democrasia ndani ya CHADEMA. Ukitaka uenyekiti ndani ya chama nafasi zinawekwa wazi, zinatangazwa, wenye uwezo mnaomba, kura zinapigwa na washindi wanatangazwa.

Sasa wametangaza kwa uwazi kabisa nafasi nyeti, nafasi ya URAIS wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania. Tunasubiri watanzania wapenda maendeleo, wapenda Demokrasia wajitokeze kupitia CHADEMA.

Tangu nimezaliwa hadi leo sijawahi kushuhudia nafasi ya uenyekiti ikigombaniwa ndani ya CCM. Ndani ya CCM hakuna Democrasia. Hazijawahi kupigwa kura ki Demokrasia kumtafuta mwenyekiti wa chama.

Kwa sasa naambiwa hata nafasi ya Uraisi hakuna Demokrasia. Hakuna kutangaza nafasi ya urais kugombaniwa ndani ya CCM. Hakuna kumpigia kura mgombea wa urais. Ni udikteta.

Tumuombe Mungu atusaidie kutuondolea CCM madarakani huku na sisi tukipigania kuikataa kwa nguvu zote kwa sanduku la kura.

Mungu imulike CCM ianze kuiamini Demokrasia ili waweze kuitumia ndani ya chama chao.

Mungu Ibariki CHADEMA, Mungu Ibariki Tanzania.
 
Hizo fomu Chadema ni sinema tu, kuna watu walichokuwa fomu jimbo la Pwani wakapewa majina ya ajabu na kuitwa ni mapandikizi ya CCM.
 
Katika muda ambao presha ya Jiwe iko juu Ni mwezi huu ,maana hata betri lake linaweza kuishiwa chaji Hana amani kabisa mwezi huu,anaweza dai kwa presha.
 
Dirisha la nafasi ya kugombea urais ndani ya CHADEMA limefunguliwa rasmi Leo. CHADEMA safari hii wameamua kuzuia waviziaji kama mamvi.

Ni raha sana kwa Democrasia ndani ya CHADEMA. Ukitaka uenyekiti ndani ya chama nafasi zinawekwa wazi, zinatangazwa, wenye uwezo mnaomba, kura zinapigwa na washindi wanatangazwa.

Sasa wametangaza kwa uwazi kabisa nafasi nyeti, nafasi ya URAIS wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania. Tunasubiri watanzania wapenda maendeleo, wapenda Demokrasia wajitokeze kupitia CHADEMA.

Tangu nimezaliwa hadi leo sijawahi kushuhudia nafasi ya uenyekiti ikigombaniwa ndani ya CCM. Ndani ya CCM hakuna Democrasia. Hazijawahi kupigwa kura ki Demokrasia kumtafuta mwenyekiti wa chama.

Kwa sasa naambiwa hata nafasi ya Uraisi hakuna Demokrasia. Hakuna kutangaza nafasi ya urais kugombaniwa ndani ya CCM. Hakuna kumpigia kura mgombea wa urais. Ni udikteta.

Tumuombe Mungu atusaidie kutuondolea CCM madarakani huku na sisi tukipigania kuikataa kwa nguvu zote kwa sanduku la kura.

Mungu imulike CCM ianze kuiamini Demokrasia ili waweze kuitumia ndani ya chama chao.

Mungu Ibariki CHADEMA, Mungu Ibariki Tanzania.
Viva CHADEMA... Viva 4Ever... Chama la wana
tapatalk_1590166850924.jpg

Jr
 
Back
Top Bottom