GE2025 Nassibu Kitabu: Samia ni lulu, msitishike na kitu chochote dola ipo, mkapige Kura

GE2025 Nassibu Kitabu: Samia ni lulu, msitishike na kitu chochote dola ipo, mkapige Kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Mgombea Udiwani wa Kata ya Jangwani, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nassibu Hassan Kitabu, ametoa wito kwa wananchi wa kata hiyo kutoogopa vitisho vinavyoenezwa na baadhi ya watu wanaopanga kuzuia Uchaguzi Mkuu kupitia maandamano.

Akizungumza katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika Oktoba 16, 2025, Hassan amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamilifu zoezi la upigaji kura linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Aidha, amewasihi wananchi kumpigia kura Mgombea Urais, Mbunge pamoja na Diwani wa CCM ili kuendeleza juhudi za maendeleo katika kata hiyo na taifa kwa ujumla.

Hassan alimalizia kwa kusema kuwa yeye na chama chake wapo tayari kushirikiana na wananchi katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo endapo watapewa ridhaa ya kuongoza.

 
Back
Top Bottom