Nassari: Watoto wa maskini msiogope, msikate tamaa, inawezekana

Emashilla

Senior Member
May 24, 2012
138
26
Hongera Mheshimiwa Joshua Nassari,(MB.Arumeru Mashriki)
Nakupongeza kwa mengi pamoja na hili la kuwatia moyo vijana na maskini wa Meru na popote duniani. Vijana na wananchi wa Tanzania kwa ujumla wao wamekata tamaa kiasi cha kubaki wakinung'unika tu. Wananchi msivujike moyo.Jipeni moyo mkuu, msaada wenu upo hapo mlipo lakini yupo azuiaye kwa sasa. Jitahidini na tujitahidi kwa pamoja katika kuleta mabadiliko ya kweli. Kwa wana Arumeru mpeni ushirikiano wa hali na mali kijana wetu,Joshua Nassari ili kuikomboa Meru na Taifa letu. Mipango yake ya kuanzisha taasisi ya maendeleo na mengine mengi aliyoyasema kupitia vyombo vya habari leo majira ya saa tatu usiku kwa saa za Afrika Ya Mashariki ni ubunifu mkubwa sana. Jipe moyo mkuu maana hili nalo linaweekana


SOURCE: RadioFive FM, Kipindi cha Maendeleo ya Jamii> 12.06.2012
 
Back
Top Bottom