Nassari na Lema: Tuna ushahidi wa madiwani waliohama wakipokea rushwa, tupo tayari kuwaonyesha TAKUKURU na DCI

Kwa hiyo CHADEMA mnamadiwani ambao wananunuliwa?
Ukiacha rushwa ni kitendo cha jinai, kuwa na kiongozi anayenunulika, hafai kabisa. Hao madiwani wa CHADEMA sasa ni dhahiri kwamba waliteuliwa na Chama kwa rushwa.

Katika msingi huo, ni jambo la kushangaza na aibu, kwa CHADEMA kulifanya kama mtaji wa kisiasa - make noises - ili jamii iwasikie na kuwahurumia.
 
Wanaunga mkono kitu gani hasa. Bombadi? wakati ni mbovu na ningine zinapigwa mnada? Makinikia wakati tumejua ni hoax ? Ni hiyo reli wakati haitaa ikamilike?
 
Nimependa hoja zao ila sijapenda representation (body language) kwani wapo kishikaji sana, nadhani wanalajujifunza toka kwa Freeman Mbowe kwenye ile press ya juzi.

Anyway ujumbe umefika, na Lema nimemkubali natumai Nasari naye ataricover soon.
 
Mbunge wa Arumeru Mashariki ,Joshua Nasary amesema kuwa anao ushahidi wa Watu waliohusika kupanga njama katika matukio ya uchomaji shule katika Mkoa wa Arusha ,sambamba na wahusika wa kununua madiwani wa chadema waliohamia ccm hivi karibuni.

Alisema wahusika wa matukio hao ni wateule wa serikali na walifanya hivyo kwa lengo la kupata vyeo .

Mbunge hiyo machachari amesisitiza kuwa tupo tayari kuachia ubunge wake iwapo atashindwa kuthibitisha madai hayo mbele ya vyombo vya dola .

Amesema yupo tayari kumkabidhi rais Magufuli majina ya wahusika wa matukio hayo baada ya kufanya uchunguzi wake kupitia vyombo vya kisasa vya kiuchunguzi alivyokuja navyo kutoka uingereza ambavyo vimenasa Picha za video wakati mipango ya njama ya kutekeleza matukio hayo ikifanywa na Watu hao.

076a18cafb2c64f519fd00e29930ede7.jpg
 
Tunaweza tukadhani tunawaabisha na kuwavunjia imani wananchi dhidi ya ccm, lkn ukweli ni kwamba chadema ndiyo tunapata madhara mara dufu. Tunapoteza imani kwa wananchi waliotupatia kura kumchagua diwani anayenunulika.

Wananchi wanajawa na hasira dhidi ya chadema. Na hivyo kukiona chama na wanachama kuwa wamekaa kidili dili tu.

Kama diwani ananunulika, mwanachama wa kawaida je? Huyu si ndiyo bure kabisa? Kama diwani aliyepitia hatua zote za mchujo hadi kufikia kupewa nafasi ya kugombea ananunulika, maana yake chama kinanunulika.

Pia taswira inayojengeka ni kwamba chadema siyo chama makini ktk kutafuta wagombea wake. Huwa kinafanya zoazoa. Hakitafuti mtu aliyemeza itikadi na kushiba Sera za chama na yuko tayari kufa kwa kukitetea chama.

Kutoa rushwa ni kosa, na kupokea rushwa ni kosa pia. Na kwakuwa ccm ndiyo chama dola na chadema inatafuta namna ya kuiondoa ccm madarakani basi kilipaswa kicheze mchezo salama na safi zaidi wa kisiasa wenye makosa kiduchu sana.

Ni makosa makubwa kujaribu kuwa sawa na ccm. Kwani wananchi wasipoiona tofauti yetu na ccm hawatakuwa na haja ya kuiacha ccm. Hili la madiwani kujitoa kwa kununuliwa tusilishadadie kana kwamba linatujengea heshima kwa wananchi. Linatuondolea utofauti na upekeee wetu dhidi ya ccm. Hivyo linatudidimiza.

Acha lisemwe na wao sisi tupige kimya. Kwasabb mahakama, polisi, takukuru vyote vyao. Wanaweza wakafanya lolote kutuangushia zigo tukabaki watupu mbele ya wananchi hata kama ushahidi tulionao ni wa dhahiri.

Ni maoni yangu tu .
 
Hivi anafikiria Arusha ni kama chato ?

Au arusha ni kule Dodoma wanapokula viwavi?

Arusha tena arusha mjini ? Hivi juzi tu amesahau uchaguzi wa Lema jinsi alivyoshinda in landslide votes?..

Arusha jinsi ilivyo hata kama yeye angetokaa ikulu kwenda kugombea udiwani kwa Sera mbovu za diwani wa wanyonge Mara tunaibiwa sana angeshindwa mapema sana .

Kama anabisha aende ajaribu ndio aelewe kwamba watu wamemchoka na wamechoshwa na ccm.
 
Back
Top Bottom