Mbunge wa Arumeru Mashariki CHADEMA ambaye pia ni mbunge mdogo kuliko wote Tanzania amewataka wananchi wake kusimama kuchangia fedha za maabara kwenye shule za sekondari Kama fedha za Umma zilizoibiwa kupitia Escrow account na sagga ya IPTL hazitarudi kwa Umma. Aliyasema Hayo Juzi jumapili kwenye Ibada ya kuwasimika wachungaji wawili wa KKKT Dayosisi ya Meru. Kauli yake iliungwa mkono na maaskofu waliokuwamo akiwamo Dr. Akyoo.