Hawa watu wa Arumeru bila kujali ni CCM au Chadema nimependa sana misimamo yao
Wote kwa pamoja wanakubaliana na suala moja, huyu Kijana Nassari waliyempandisha daraja kutoka utotoni na kumpa hadhi ya Ubunge kwa ''jasho na damu'' ni msaliti mkubwa. Wamekubaliana hawafai kwa kishindo.
Nassari asubiri ukurugenzi au U-DC wa kuteuliwa tu. Biashara ya kuuza jimbo kwa kutohudhuria vikao vya Bunge imeisha. Of course usaliti wake haukuwa bura, alilipwa sana, lakini sasa ndio mwisho wa siasa za kuchaguliwa.
Maisha yake yatakuwa ya siasa za kuteuliwa na kutenguliwa.
Haya ni matokeo mazuri sana na Wana Arumeru washukuriwe kwa kumtosa mburukenge wahedi
'