Nassari aambiwa aache Kucopy na Kupaste

Nassari aambiwa aache Kucopy na Kupaste

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Posts
899
Reaction score
1,108
Wanajf.
Nimeamua kuja hapa kuweka mambo haya sawa, Kijana wetu na mdogo wetu Nassari alionekanika ni kijana machachari mbele mwa jamii pale anapokuwa jukwaani na sehemu nyinginezo hili halina ubishi kabisa.

Jana na Juzi kulikuwa na mikutano ya CDM Moshi na Mwanza ambayo Dogo janja alihudhuria na kupewa nafasi ya kuhutubia kama mbunge, Naomba niongelee hili la Mwanza maana la Moshi sikuwepo zaidi ya kusikiliza kwenye Redio.

Nassari inabidi uwe wewe kama wewe acha kucopy na kupaste maana unapocopy ni lazima utaje nukuu ya mtu fulani ila wewe unasema kama wewe ndiyo umefanya hicho kitendo wakati siyo wewe, Mfano Unapenda kuongelea ishu ya Magereza wakati hujawahi kwenda, Jana kwenye mkutano wa hapa Mwanza ulizungumzia kuhusu mateso ya wafungwa walivyokuwa wanakueleza jinsi walivyofungwa kwa kusingiziwa wakati siyokweli kwamba wewe ndiyo ulikuwa magereza bali Alikuwa ni Lema! kwanini unashindwa kusema Na Nukuu kutoka kwa Lema? kama ambavyo Lema Anapenda kunukuu Wanaharakati mbalimbali kama steve Biko, Martin Luther nk.. ni Lazima ubadilike utafute mkakati mwingine wa jukwaani wewe ni kiongozi sasa unaongoza jimbo wananchi wako wangependa kukusikia Nassari na siyo Lema.

Najua waweza kwazika ila huwo ndiyo ukweli kuwa wewe kama wewe Level uliyofikia siyo ya kuwa hivyo, Badilika Tunakupenda ndiyo maana tunakuambia ukweli urudi kwenye mstari maana watu makini hukushusha na kusema umebebwa na upepo.... Natumaini salamu hizi zitakufikia na utazisikia.... jiulize kwanini kamanda Mawazo hakopy na kupaste? Samahani lakini..
 
Kwani kuelezea matatizo yaliyopo gerezani ni kukopi, ama ni lazima ufungwe? Kwani chanzo cha taarifa cha mateso ya gerezani ni Lema tu? Hapa hujaeleweka. Nasari kama mbunge ananafasi ya kufatilia kwa undani matatizo mbalimbali kwenye jamii na kuyashughulikia either pamoja na wananchi, kuweka msukumo kwa wahusika ama kulifikisha Bungeni.
 
We usirudie siku nyingine kukosoa viongozi wako hadharani sio desturi ya chama chenu! Ikibidi mtu wa kukosolewa hadharani ni Zitto kabwe pekee maana hata ukipatikana na hatia uwezekano wa kupewa karipi ni mkubwa badala ya kufukuzwa!
 
Una hakika kuwa Nassari hajawahi kutembelea magereza? Mbona kuna tatifi nyingi zinaonesha matatizo ya magereza au nazo wame-cpoy & paste toka kwa Lema?
 
Kwani kuelezea matatizo yaliyopo gerezani ni kukopi, ama ni lazima ufungwe? Kwani chanzo cha taarifa cha mateso ya gerezani ni Lema tu? Hapa hujaeleweka. Nasari kama mbunge ananafasi ya kufatilia kwa undani matatizo mbalimbali kwenye jamii na kuyashughulikia either pamoja na wananchi, kuweka msukumo kwa wahusika ama kulifikisha Bungeni.

hahaha unatetea kisa ni mtu wa chama cha zone yenu sio
 
Maccm bana mh kazi mnayo

ma çcm wapi hamna jipya nyie wabunge wenu wanapenda umàrufu wakati hawajui mambo we kama huyo nasari ati alimkataza JK kufikaàrumeru chadema ni kichaka cha wevi
 
sasa toka akatazwe kakanyaga, c anapaogopa sana meru, maccm bwana!
 
Ndugu yangu hebu acha hoja dhaifu kama hizi, hebu jaribu kutofautisha kati ya fb na Jf na usirudie tena makosa kama haya.
 
mmmmh puuuuuuuuuumbaaaaaaaaaa ingekua una nia ya kumwambia ungem pm
 
Wanajf.
Nimeamua kuja hapa kuweka mambo haya sawa, Kijana wetu na mdogo wetu Nassari alionekanika ni kijana machachari mbele mwa jamii pale anapokuwa jukwaani na sehemu nyinginezo hili halina ubishi kabisa.

Jana na Juzi kulikuwa na mikutano ya CDM Moshi na Mwanza ambayo Dogo janja alihudhuria na kupewa nafasi ya kuhutubia kama mbunge, Naomba niongelee hili la Mwanza maana la Moshi sikuwepo zaidi ya kusikiliza kwenye Redio.

Nassari inabidi uwe wewe kama wewe acha kucopy na kupaste maana unapocopy ni lazima utaje nukuu ya mtu fulani ila wewe unasema kama wewe ndiyo umefanya hicho kitendo wakati siyo wewe, Mfano Unapenda kuongelea ishu ya Magereza wakati hujawahi kwenda, Jana kwenye mkutano wa hapa Mwanza ulizungumzia kuhusu mateso ya wafungwa walivyokuwa wanakueleza jinsi walivyofungwa kwa kusingiziwa wakati siyokweli kwamba wewe ndiyo ulikuwa magereza bali Alikuwa ni Lema! kwanini unashindwa kusema Na Nukuu kutoka kwa Lema? kama ambavyo Lema Anapenda kunukuu Wanaharakati mbalimbali kama steve Biko, Martin Luther nk.. ni Lazima ubadilike utafute mkakati mwingine wa jukwaani wewe ni kiongozi sasa unaongoza jimbo wananchi wako wangependa kukusikia Nassari na siyo Lema.

Najua waweza kwazika ila huwo ndiyo ukweli kuwa wewe kama wewe Level uliyofikia siyo ya kuwa hivyo, Badilika Tunakupenda ndiyo maana tunakuambia ukweli urudi kwenye mstari maana watu makini hukushusha na kusema umebebwa na upepo.... Natumaini salamu hizi zitakufikia na utazisikia.... jiulize kwanini kamanda Mawazo hakopy na kupaste? Samahani lakini..

yamkin usingizi ni tatizo kwako.
 
Kuna mijitu miwili humu inaboa leo.Mhh ni ya kiume lakini inaonekana imeolewa na mbaya zaidi inapumuliwa kisogoni.
 
Back
Top Bottom