NASIMAMA NA SPIKA NDUGAI.
Jana 14:15pm,07/06/2019.
Nianze kwa kusema Matamshi ya CAG kwenye vyombo vya habari yamekuwa yanaleta mkanganyiko sana,Huwa napata shida sana kumuelewa CAG,Wacha niendelee kula ugali labda nitamuelewa.
Msingi Mkuu ama naweza kusema Jukumu Kuu la Bunge letu ni Utunzi wa Sheria na Kuisimamia Serikali.Hapo kwenye kuisimamia Serikali CAG na yeye yumo,CAG anajumuika na Bunge katika kamati mbili anakuwa sehemu ya kuisimamia Serikali.
Kwa ambao mliishia kusoma Machapisho ya Lema,Zitto,Ole Mushi juu ya habari hii na kuanza kucomment bila kusikia clip ya CAG na Clip ya Spika akifanya Press, Nashauri mumsikilize Mhe Spika kama mimi kupitia Clip ya Video mtamuelewa vizuri sana Spika sio kama tulivyosoma machapisho awali akina Zitto Kabwe,Godbless Lema na Thadei Ole Mushi, Hoja ya Spika ina nguvu sana,hasa dharau aliyoonyesha CAG kwa Bunge na ukosefu wa Uzalendo aliouonyesha CAG kwa kwenda kuzungumza Marekani ,mambo ambayo angeweza kuyachukulia hatua akiwa katika kamati mbili za Bunge ambazo anaingia.
Matamshi ya CAG si dharau kwa bunge tu hata kwa Serikali pia..maana bungeni kuna baraza lote la Mawaziri ikiwemo na Waziri Mkuu hii ni ishara ya dharau na utovu wa nidhamu kwa Mamlaka husika..nadhani kuna haja ya nafasi CAG kuangaliwa upya kama bado anafaa kuendelea na hiyo nafasi ama la.
CAG kama sehemu ya Serikali angeweza kusema ofisi ya CAG imelifanyia kazi, na ni kazi ya Bunge kuhakikisha inapeleka Maazimio Serikalini si ilikuwa inatosha,ingeonyesha dhana ya umiliki ama Umoja katika hilo, kuna haja gani ya kusema bunge ni dhaifu? Ina maana yeye CAG na wataalam wake wanapoingia kwenye kamati za Bunge nao ni dhaifu sio!? Mara ya mwisho CAG alizua sintofahamu kubwa kuhusu 1.5T kwa matamshi ya namna inayofanana kwenye vyombo vya habari. Na kwanini asimwandikie Spika kama kuna mahali alihisi kuna lega lega, bado naamini aliyoyafanya ni utovu wa nidhamu..huwezi kusema mhimili mwingine wa nchi ni dhaifu.
Katiba na sheria ya kuanzishwa kwa ofisi yake inaruhusu kuondolewa kwa CAG kutoka kwenye ofisi, inaweza kutumika hiyo kama njia mbalada ya kuondoa tatizo.
-Kuchaguliwa ama kuondolewa kwa Spika.
7.The Controller and Auditor General may be removed from his office for reasons and procedures provided for under Article 144 of the Constitution.
8,-(1) Where the post of the Controller and Auditor-General becomes vacant,the President may appoint a person to that office within sixty days of the post becoming vacant.
Viongozi wa ofisi za Umma wanatakiwa kufanya kazi kwa manufaa ya nchi( national interest)..sasa sijui yeye anafanya kazi kwa manufaa ya nani!?
Kifungu hiki cha Katiba kinampa Mh Rais mamlaka ya kumuwajibisha na kumwondoa CAG,kwa misbehaving kama anavyofanya huyu CAG.
144.-(1) Without prejudice to the other provisions of this Article,the Controller and Auditor -General of the United Republic shall be obliged to vacate office upon attaining the age of sixty or any other age which shall be prescribed by a law enacted by Parliament.
(2) The Controller and Auditor -General may be removed from office only for inability to perform the functions of his office (either due to illness or to any other reason) or for misbehaviour,or for violating the provisions of the law concerning the ethics of public leaders and shall not be so removed except in accordance with the provisions of subarticle (4) of this Article.
(3) If the President considers that the question of the removal of the Controller and Auditor-General from office under the provisions of this Article needs to be investigated,then the procedure shall be as follows:
(a) the President shall appoint a Special Tribunal which shall consist of a Chairman and not less than two other members. The Chairman and at least half of the other members of that Special Tribunal shall be persons who are or have been Judges of the High Court.
Kifungu alichokitaja Lema,Zitto na Mushi kuwa kinampa immunity CAG ya kutohojiwa na chombo chochote, Kinapotoshwa. Ukweli ni kwamba hawezi kuhojiwa na chombo chochote wakati akiwa anatekeleza majukumu yake ya ukaguzi (Auditing).
Yaani ule ushibe upande ndege uende Marekani na kuichafua mihimili yetu kwa dharau ati usihojiwe? La hasha,tunaupeleka wapi Uzalendo kwa nchi yetu ,Tanzania!? Tumeamua kumuiga Tundu Lissu anavyoichafua nchi uko Ulaya au tumeamua kumuiga Mange Kimambi,au Ansbert Ngurumo au Evarist Chahali!?
Hivi ni busara CAG kwenda kuidhalilisha mihimili yetu nje ya Nchi huko kwa mabeberu? Huu ndio weledi!? Je ndo kazi iliyompeleka? Yaani CAG anageuka kuanza kufanya kazi za akina Tundu Lissu,Zitto Kabwe na Mbowe wanaokimbiliaga Ulaya kuisemea Tanzania, Hebu tuache mchezo kwenye Uzalendo na heshima ya Tanzania,Wapo Watanzania uko Ulaya wanaishi kwa heshima ya Tanzania ,lakini mtu anatoka huku anaenda huko kuichafua Tanzania.
Tukidai CAG anakinga kwa kila kitu ina maana CAG hata akiiba aachwe, akitukana watu aachwe, akiua aachwe kisa "hawezi kuhojiwa?" Yako wapi maadili aliyotufundisha Mwalimu Nyerere!? Viko wapi vyuo vya Maadili ya Uongozi,Hombolo pale Dodoma na Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere pale Kigamboni!?
Kila Kiongozi katika mihimili yote mitatu tukiyonayo wanapaswa kuishi kwa kulinda Sheria na Katiba na kuheshimu mihimili mingine.
Huwezi kuliita Bunge dhaifu, ni lugha ya kukera kutoka kwa mtu wa aina ya CAG hasa tunavyoona jinsi Bunge mara kadhaa linavyowawajibisha watendaji wa umma kwa sababu ya audit reports. Mara kadhaa Mawaziri wamewajibishwa na Bunge kwa sababu ya CAG, Watendaji wa Mikoa, Halmashauri, Mawaziri, Makatibu Wakuu wamekuwa wakibanwa kwa sababu ya Audit Report, inawezekana CAG alitamani mahali fulani katika Bunge paongeze nguvu, ana fursa sahihi zaidi ya kushauri, lakini sio kulitusi Bunge zima kuwa ni dhaifu.Je Wakurugenzi wenye hati chafu has a kuwa ni bingwa kwa kufutwa kazi!?
Ukitekeleza wajibu wako hautakumbana na mkono wa sheria, ukishindwa yatakukuta haya ya CAG kama ambavyo pia Mawaziri, Makatibu Wakuu na hata Wakuu wa Mikoa kadhaa ambavyo wameshafikishwa katika Kamati mbalimbali za Bunge kuitwa kutoa ufafanuzi ikiwemo hii ya Maadili.
Kuna watu wanasema eti Spika alikuwa anahangaika kutaja kosa la CAG. hakuweka wazi kwamba “amelidharau bunge” badala yake aliishia kusema ‘aende akeleze kuhusu maneno yake’ Hivi jamani kusema "Bunge ni dhaifu" bado hamjaona kosa!? CAG kaamua kuuvua nguo mhimili wa Bunge,Sasa lazima aende mbele ya Bunge akajieleze,na kwa nini alienda kusemea Marekani!?
Nimalizie kwa kusema,Kanuni za Bunge zinaipa mamlaka ya Bunge kumuita na kumuhoji mtu yeyote isipokuwa kama kuna shauri lolote dhidi ya mtu huyo lililopo Mahakamani,Mungu ibariki Tanzania.
Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.