Nasikia madaktari wamegoma tena?

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,090
Niko kwenye kikao so sijui nini kinaendelea ila kuna mtu kapita hospitali ya mkoa niliko anasema madaktari wamegoma, hivi inatokea na maeneo mengine pia au?
 
Wala siwezi kubisha kitu hapo endapo madai halali ya Madaktari pengine yalichukuliwa tu kama 'Upepo wa Kupita' vile sasa unafikiri wenyewe hawana akili kujua wafanye nini zaidi hadi hapo?
 
BAdo hawajagoma lakini wanajiandaa kuhudhuria kwenye mkutano wao mkubwa sana kesho kupeana feedback ya usanii waliofanyiwa na serikali siku zote hizi tangu Mh.presidaa alivyoingilia kati mgomo wao..Maamuzi mazito yanaweza kutolewa!!
Labda hapo ulipoambiwa wamegoma walikuwa wameondoka kuja Dar!
 
BAdo hawajagoma lakini wanajiandaa kuhudhuria kwenye mkutano wao mkubwa sana kesho kupeana feedback ya usanii waliofanyiwa na serikali siku zote hizi tangu Mh.presidaa alivyoingilia kati mgomo wao..Maamuzi mazito yanaweza kutolewa!!
Labda hapo ulipoambiwa wamegoma walikuwa wameondoka kuja Dar!
Waambie wakitoka kwenye mkutano wao waje pale jangwani saa kumi kuja kusikiliza suluhisho la matatizo Yao mwaka 2015
 
Madai yao yaliishatimizwa, Mpona, Nkya, Nyoni na Mtasiwa hawapo tena wizarani. Na yule mchawi Maji Marefu kaenda kutibiwa India kwa hiyo hakuna haja ya kugoma tena kwa kuwa wagonjwa wao ni sisi walalahoi tu. Wanaonyima haki za madaktari hawatibiwi hapa hivyo mgomo hautawaathiri hata kidogo
 
Kugoma bongo? Dawa ya mgomo inapatikana magogoni,ni kikombe kimoja cha ghahawa na ukitoka hapo tu tayari pepo la mgomo lina kutoka.Waulza akina mkopi na akina ulimboka,wapi cdm na maandamano ya kupinga mswada wa katba.Walipopata ghahawa wakaibuka na majibu ya ndiyo mzee
 
Waondoke zao nao waache kulinga wafanye kazi,. Watu hawana msimamo tuliwaungs mkono kipindi kile wakalegeza msimamo,. Hatukubali waendelee kutesa watu tena
 
Ukitaka kufanikiwa Tanzania usigome kwa sababau maisha yamekubana na huna jinsi au kwa jazba kwa sababu umeona rafiki yako au mtu unaye mfahamu amekuwa tajiri ghafla. Ili migomo iwe na manufaa ni lazima kuwepo na determination and with that determination there should be a determined destiny of either getting what your fighting for or dying without, there should be no compromise. However, because of umaskini and not having a common determination and well defined reason for what your fighting for its easy to get apart and to that end you never get what you desired. Believe me what is happening in bongo land in the so called migomo it is a joke of the day, all participants they never have a common understanding.

Look on the recent arab spring revolution, it was a die or live commitment, it was a lose - win situation and not looking for compromises as its used to happen in Tanzania, so called peace loving country.In politics there is no such terminologies as win-win situation, there is only win-lose situation and we should learn it. So what is called mgomo in Tanzania is basically fighting for individual jealous
 
Kweli kama wana mpango wakugoma wacha wagome. ila ikifikia hapo utasikia baba RZ 1 anasafiri maana jamaa hawezi kabisa uongozi. sijui nani alimchagua????
 
Mimi sijui nisimame upande gani hapo maana madhara mengi ni kwetu walala hoi na siyo hao wanaosababisha huo uzembe maana hata wakati hali ikiwa shwari wanaenda india. Na upande mwingine bila hivyo vifaa havitanunuliwa na ni haki yetu. Du kazi kweli kweli Mungu tu atuepushe na hili balaa!
 
bado hawajagoma lakini wamepanga kukutana kwa tathmini ya utekelezeji wa makubaliano yao na serikali.inavyoonekana serikali imefanya usanii hivyo tusishangae kushuhudia mgomo mwingine
 
Niko kwenye kikao so sijui nini kinaendelea ila kuna mtu kapita hospitali ya mkoa niliko anasema madaktari wamegoma, hivi inatokea na maeneo mengine pia au?

yeah,ni kwel wauguz wa mkoa wa MARA wamegoma na wamesababisha vifo vya watoto wa3 na mtu mzima m1.
source ITV
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom