Nasikia kelele masikioni na kichwani

Nasikia kelele masikioni na kichwani

Edylux

Member
Joined
Mar 30, 2009
Posts
48
Reaction score
10
Salaams wana JF,

Ninasumbuliwa na kelele zinazovuma ndani ya masikio yangu na kichwani kwa ujumla. Usiku sauti inakuwa kubwa zaidi.

Hospitali nimeambiwa itaisha yenyewe, lakini ni zaidi ya mwezi sasa na miluzi inaongezeka sauti.

Msaada tafadhalini.

Edylux
 
kuna rafiki yangu amepata tatizo hilohilo imepelekea kuacha kazi kabisa mpaka sasa kajaribu vipimo wapi matibabu wapi maombi wapi ameamua kurudi kwao tabora akaonane na ghost wake ,so jitahidi kuwahi hospitali
 
Baadhi ya dawa e.g. Quinine zinasababisha hali hiyo. Na uzuri ni kwamba hali hiyo huisha yenyewe ingawaje kwa wengine inaweza isiishe. waone ENT surgeons au Neurologist kwa ushauri wa uhakika
 
Ulikuwa unafanya kazi ya aina gani mpaka ikakuletea hiyo shida au ulitumia dawa(mfano mzuri ni quinine) au imeanza yenyewe tu? nieleze ili nikupe uzoefu mimi nina tatizo hilo kwa miaka 11 sasa,no cure ila unaweza kupunguza hiyo hali, ingawa inategemea chanzo ni kitu gani.
 
Pole sana mkuu! Hiyo hali inaweza kawa sababishi kutokana na mazingira uliyo au unayo ishi, je? Unafanya kazi kiwandani, au kariako, au fundi geti
 
Baadhi ya dawa e.g. Quinine zinasababisha hali hiyo. Na uzuri ni kwamba hali hiyo huisha yenyewe ingawaje kwa wengine inaweza isiishe. waone ENT surgeons au Neurologist kwa ushauri wa uhakika

Ahsante kwa shauri
 
Ulikuwa unafanya kazi ya aina gani mpaka ikakuletea hiyo shida au ulitumia dawa(mfano mzuri ni quinine) au imeanza yenyewe tu? nieleze ili nikupe uzoefu mimi nina tatizo hilo kwa miaka 11 sasa,no cure ila unaweza kupunguza hiyo hali, ingawa inategemea chanzo ni kitu gani.

Kikazi mimi ni mhasibu. Nadhani itakuwa imeanza yenyewe. Nishauri tafadhali
 
Jaribu kutumia mafuta ya samaki ( Cod Liver Oil, Omega 3 etc) ndani ya wiki 1 tatizo litakwisha kabisa
 
Kikazi mimi ni mhasibu. Nadhani itakuwa imeanza yenyewe. Nishauri tafadhali
Nenda Muhimbili ENT kitengo hiki kina madaktari bingwa watakusaidia,mimi nilikuwa nafanya kazi sehemu zenye makelele sana ikanisababishia hiyo hali,baada ya kufanyiwa vipimo vyote tena vya kisasa na kupewa madawa ikaonekana siwezi tena kupona ila ni kuepuka zaidi mazingira yanayoweza kuuongeza hiyo hali na so far ninatumia kifaa cha kuongeza usikivu.
 
Jaribu kutumia mafuta ya samaki ( Cod Liver Oil, Omega 3 etc) ndani ya wiki 1 tatizo litakwisha kabisa

Atumiaje mkuu maana wahanga tuko wengi humu!anatakiwa anywe au unaweka ndani ya masikio?
 
Habari ndugu naona tatizo nililo nalo ni kama la kwako ila mimi ni sikio la kulia linatoa milio usiku naona uzi wako ni wa muda vipi ummeshapona au bado lina kusumbua na kama umepona ulitumia dawa gani?
 
Pole sana; daktari aulikuambia una tatizo gani?

Tatizo lina muda gani? Kuna dalili nyingine zinazoambatana na tatizo hili? ni vigumu kukusaidia kwa maelezo hayo mafupi uliyotoa kwani ugonjwa sio dalili moja bali.

mkusanyiko wa dalili. kwa hiyo basi kulingana na dalili nyingine ulizonazo Yawezekana ukawa na tatizo
linaloitwa Tinnitus ambapo ENT specialist watakusaidia

Au kwa upande mwingine yawezekana ikawa auditory hallucinations ambapo Psychiatrist au Clinical Psychologists wanaweza kukusaidia!
Wataalamu hawa wote wanapatikana muhimbili
 
Kuna rafiki yangu ana hili tatizo, watu wengine huwa hawaamini, nami nilikuwaga mbishi kidogo. Yeye rafiki yangu ana imani kabisa kwamba ana mapepo kichwani!
 
Pole ndugu,
kuna ndugu yangu alikuwa anasumbuliwa na tatizo kama hilo bahati nzuri tulipata suluhu.
Wasiliana nami nikushauri jinsi ya kupata msaada. 0716 299 399
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom