Nashukuru mungu Tanzania tuna kiongozi Membe ambaye ni serious, anaelewa mambo kwa undani, ana uzoefu wa ukweli, anaona mbali na anajua Tanzania inahitaji nini kujiendeleza. Kwenye dunia ya sasa ya technologia Tanzania inaweza kuendelea haraka sana kama ikipata kiongozi kama Membe ambaye anajua dunia inapoenda mfano sasa hivi kuna watu India wanafanya kazi za account za kampuni za Canada!, Bank ya marekani lakini customer service ipo Agentina. Kazi za miaka ijayo hazitatokana na kuchukia Wakenya na wahamiaji kwani mtu yeyote anaweza kufanya kazi sehemu yeyote duniani kama kuna mawasiliano na ujuzi wa uhakika. Gas yetu vilevile inahitaji mtu anayejua mambo kwa undani badala ya ushabiki wa wanasiasa wengi wa sasa. Tanzania inahitaji raisi mjuzi na anayejua mfumo wa uchumi, banking system ya kisasa, uhamiaji na solution za kisasa. Kwa mawazo yangu baaada ya kusikiliza na kuongea na vi0ongozi wengi akiwemo Sumaye, Lowasa, Kikwete, Sitta, magufuli, sefue, Nyalandu, Mbowe, Zitto na nikizingatia mambo yote Membe ndiyo naona anafaa kuwa raisi wa Tanzania kwa kipindi hiki na atakuwa raisi kwasababu Tanzania haitaweza kupita hii nafasi. Hana washabiki lakini ni kiongozi makini