Nashukuru kwa zawadi hii ya maisha

Nashukuru kwa zawadi hii ya maisha

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Posts
13,402
Reaction score
12,792
IKIWA LEO NI MAPENZI YA MUNGU KUTIMIZA MWAKA ZAIDI NICHUKUE FURSA HII KUWAKUMBUKA WAFUATAO​
Kwa dada zangu Jul na Ritha
'si mnakumbuka tulivyokuwa wadogo, tulicheza pamoja, tulikaa pamoja katika shida na raha…tulipigana pale tulipoudhiana,ila tulisameheana kwa vile tulifundishwa upendo..mara zote tuliamini kwamba japo tulizaliwa katika hali ya umasikini ila hatutakufa masikini,kwa vile si lengo la Mungu watu wake wataabike katika dhiki..nawapenda sana dada zangu'

Kwa watoto yatima wote na wale waishio katika mazingira magumu;


..Nawapenda sana na daima nakuwa na amani sana kuwaona mkitabasamu na kufurahi,bila kujali matatizo mliyonayo maishani..sio lengo la Mungu mteseke kwa kuwakosa wazazi ama ndugu mliowapenda na kuwategemea kwa namna moja ama nyingine..Mungu si mwanadamu hata tuseme anakosea kufanya maamuzi..ishini mkimtegemea Mwenyezi Mungu,baba wa mbinguni na hakika ipo siku majonzi yenu yatageuka kuwa Furaha..hamtanung'unika tena..nawapenda sana!


N
ichukue fursa ya awali kumshukuru Mungu baba wa mbinguni kwa kunifanya moja kati ya viumbe alivyoviumba chini ya jua ..ni kwa neema yake tu kuwepo kwangu hadi leo hii kwani sina haki kuliko wale wote waliotangulia mbele ya haki.Namshukuru zaidi kwa kunipa ufahamu wa kuelewa mambo..asante Mungu kwa kunijaalia karama hii..naomba uniwezeshe kuitumia vizuri kwa wengine!

Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru wazazi wangu kwa kunileta duniani..nawapenda sana na daima napenda kuona mnaishi maisha ya ujana,yenye kila aina ya furaha..narudia kusema nawapenda sana!


S
hukrani za kipekee ziwafikie walimu wangu wa Pre Unity hadi wakufunzi wa chuo kwa juhudi zao walizofanya za kunifuta ujinga..hakina singalikuwa nilipo intellectually kama si jitihada zenu! Mungu akujaalieni kheri!


Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisiposhukuru wanajumuiya wangu wa JF kwa kuwa mentor, influencer na watu mlioni-jengea hekima ya hali ya juu! Niwaombe radhi wale tuliocharuana kwa sababu moja ama nyingine pale tulipopishana hoja!

Nimshukuru Kipekee Mzee Mwanakijiji kwa kuwa role model wangu kujiunga JF, madam Michelle popote ulipo shukrani zikufikie kwa kuchangamsha sana jukwaa enzi zako,ni wewe uliyenifundisha kuneutralize stress za siasa kwa kuchungulia MMU!


lara 1 Mungu akujaalie miaka 372 bila kujali uliyonayo sasa ili nikucheke makunyazi yatakapoanza kuibambia sura yako! Heaven on earth pamoja sana bi dada bila kumsahau kaka mkubwa MziziMkavu kwa kukubali kuchimbwa dawa kila mara!

Hawa ni wachache tu ila JF ni kisima cha mambo,nawapenda wooooooote! mia
 
Last edited by a moderator:
Kila la heri na Baraka Mkuu, ubarikiwe sana.
 
Mkuu kaamua kumshukuru Muumba wetu na watu mbali mbali akianzia Wazazi wake dada zake wawili, na watu mbali mbali hapa jamvini wakiwemo Mkjj, Michelle na wengineo na jamvi lote la JF habari ndiyo hiyo Best.

best embu nipe muhtsari nini kinaendelea au kilijiri
naona kichinachina tu
 
best embu nipe muhtsari nini kinaendelea au kilijiri
naona kichinachina tu
Mkuu amu tarehe kama ya leo miaka mingi iliyopita nilizaliwa, nimetumia fursa hii kuwaza na kutafakari na kugundua sikuwa peke yangu kwenye zoezi zima la kukua kimwili ndiyo maana nikamkumbuka mkuu sana Mungu,na wengine walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kunilea kiakili,kiroho and likely...
 
Last edited by a moderator:
Kushukuru n Roadmap ya kubarikiwa, mungu akuongoze katika busara na matemdo yako mkuu(Horseshoe Arch)
 
Mkuu sana MziziMkavu napenda sana watu wanaofikirisha ama kutoa cheche za fikra zinazosababisha wasio wavivu kufikiri ndiyo maana ni aghalabu sana kutoapreciate watu watu wa aina ya Mzee Mwanakijiji wanaotazama mambo katika 3D!

Kwa wenzangu na mimi ambao tulikuwa tumekariri kwamba kupenda ni kanuni na kanuni zenyewe ni mathalan A B C tumekuja kufunguliwa macho na watoto waliozaliwa wanasema, bi lara 1 akiwa kiranja na nikiri tu kwamba kwa mafunzo haya niliyopata wakati wa Mungu ukifika nitakuwa responsible husband kwa forthcoming wife wangu wa ukwee eeh..Si mafunzo ya muadhama wala sheikh yanayoweza kunikomaza kama darasa huru nililolipata hapa!

Nakumbuka kipindi bwana boss mambo yake yalienda mrama,sikuwa na shaka kwamba weekends ningetokaje kwa kuwa niliamini nikiingia chaka na kuchimbua hadithi za kaka Mtambuzi bas nakuwa na moments nzuri kuliko ambao mifuko ilikuwa imetuna!

Mkuu BAK nimekuwa kaimu baba/mume kwa muda mrefu kwa maana kila penye kustahili kutoa funzo kwa hawa vijana macho juu ambao ndoa zilikuwa zinawachezea kidali po nilivaa u Sr mume ili nishauri na kweli ushauri ulifanya kazi. Leo hii nichukue fursa hii pia kukualikeni kwenye shughuli yangu ya kufunga mkataba wa maisha na rafiki yangu wa siku nyiiingi bi dada. Itakuwa 27/09/2015 karibuni nyote,mje na wake zenu/waume zenu kututia joto!
 
Last edited by a moderator:
Kushukuru n Roadmap ya kubarikiwa, mungu akuongoze katika busara na matemdo yako mkuu(Horseshoe Arch)
Mkuu General8 saluti kwa mikono yote miwili...
 
Last edited by a moderator:
Lizzy pamoja sana mamaangu mdogo...kuna toy langu Abunwasi kaninunulia niliogopa kuja nalo Unga LTD kwa kuhofia manjeree wasijenirukia shingo...si unajua unga ltd hakulimwi mahindi mtu wangu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom