kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,788
- 5,027
Mwaka 2017, mimi na familia yangu tulihamia Canada kwa matumaini ya maisha bora na ya utulivu. Hata hivyo, baada ya kufika, tulikumbana na changamoto kubwa kutoka kwa baadhi ya Wakongo wenzetu tuliowakuta hapa. Walitusambaratisha kupitia fitna na chuki walizozusha baada ya kuona familia yetu ni kubwa, yenye watoto wengi wa kiume. Walihisi tukiwa na mshikamano, tungeweza kufanikiwa haraka kuliko wao.
Kwa bahati mbaya, walifanikiwa kuchonganisha wazazi wetu hadi baba akaondoka, akatuacha tukiwa bado wageni katika mazingira tusiyoyafahamu. Serikali ilisitisha misaada yote ya kijamii kwa sababu ya hali hiyo ya kifamilia. Wakati huo, mimi nikiwa na umri wa miaka 17 na bado shuleni, nililazimika kuacha masomo ili nianze kufanya kazi na kusaidia mama pamoja na wadogo zangu.
Kwa neema ya Mungu, mama mmoja Mzungu ambaye mtoto wake alikuwa rafiki wa dada yangu, alikuja kutuonyesha upendo na msaada mkubwa. Hapo ndipo tulianza kujisimamia tena taratibu.
Leo, baada ya miaka mingi, baba amerudi akiwa hana makazi, hana kazi, na hana msaada. Alienda kuishi na mwanamke mwingine ambaye baadaye alimfukuza. Mama naye tayari ana maisha mapya na mume mwingine. Mdogo wangu alimkataa kabisa alipomwendea.
Kwa huruma, nimempa hifadhi nyumbani kwangu, ila mke wangu hajaridhika kabisa na hali hiyo.
Nimejipata nikiwa katika wakati mgumu sana—kati ya huruma kwa baba yangu na wajibu wangu wa kulinda amani na heshima ya ndoa yangu. Sipendi kumwona baba akiendelea kuteseka, lakini pia sitaki kuvunja msingi wa familia niliyojenga kwa taabu.
Nimefanya uchunguzi wangu ana madeni kibao hawezi kupata nyumba kwasababu ya credit yake mbaya ya kutolipa madeni nashindwa kumsaidia na kwa Canada mtu hawezi kukodi nyumba mbili kwa wakati mmoja yaani situation yake ni ngumu mno kutatua