Nashindwa kumwelewa kwakweli

Nashindwa kumwelewa kwakweli

Nimesoma kwa makini, nikakumbuka Mara nyingi hivi visa tunafanyiwaga wanawake, nikaumia, lakini ndugu yetu hapo mko wanaume zaidi ya Watatu, ila wewe ndio myoa matumizi ndio maana unabembelezwa akikukosea.

Yule mpuuzi Mme mwenzio yeye ndo anapendwa, ila ni Mario, handsome,+ upuuzi mwingine.
Binti anaogopa kukupoteza mtomatumizi, 😂😂😂😂

Mapenzi ni hisia, mteme.

Hivi wananzengo, ulishawahi mpenda mtu mpaka ukiskia SMS imeingia unajua ni yeye kumbe sio yeye maskini ni biko wanakukumbusha kucheza? Unafonzaaaa

Au unapiga simu hapokei unakuta yupo online dah😂
 
Miezi saba hujapiga!! What a fuk
Hivi mwanamke ambaye ni dem wangu inaishaje wiki sijamtafuna...atanambia nini?

Mi naona shida sio yeye, Shida ni wewe mleta mada.
 
Habari wana JF,poleni na harakati za kulijenga taifa.
Naombeni ushauri wenu kwa haya yanayonikuta sasa. Mimi nipo kwenye uhusiano na msichana ambaye kiukweli nampenda sana na nipo tayari kumuoa mda wowote, sina mwingine zaidi yake ila mambo anayonifanyia nashindwa kumuelewa. Mwanzoni tulikuwa tunapendana sana alikuwa hana tatizo ila amekuja kubadilika ghafla na mimi huwa nampa mahitaji yake yote anayohitaji hata ndugu zake huwa nawasaidia,na nimeshamtambulisha kwetu anajulikana na kwetu wanampenda sana ila visa vyake ni hivi;
1. Huwa nataka sana kufanya mpango wa kwenda kwao kujitambulisha rasmi lakini yeye anakataa,yaani hataki kabisa.
2. Huwa hataki kabisa niguse simu yake,nikigusa tu anakuwa mkali kama pilipili ila mimi huwa nipo muwazi kwake kwa kila kitu,mambo yangu ya maendeleo namuhusisha lakini haonyeshi interest, simu yangu huwa namuachia muda wowote akitaka.
3. Pia ana tabia ya uongo sana, yaani unaweza kumuuliza yupo wapi akakwambia yupo nyumbani ila nikimpigia simu dada yake kumuuliza naambiwa hayupo,ni mengi sana ameshanidanganya mimi,mengi sana,sio mkweli kabisa.
4. Ana tabia anatoka kazini anapitia sehemu zake huko anazojua anarudi nyumbani kwao usiku mida ya saa nne au saa tano usiku,kwao wenyewe wameshamchoka na tabia zake,wanamlalamikia sana(Anaishi na mama yake tu,amelelewa na single mother)
5. Nilikuwa nimeshafanya mpango kabisa wa kumvisha pete ya uchumba ila huwezi amini alikataa
7. Huwa nikimwambia tutoke out huwa anasema anakuja lakini hata haji(Mara nyingi tu ameshanifanyia hivyo)
8. Baada ya kuwa nae kwa miezi minne nikamgusia kuhusu suala la kufanya mapenzi,amekataa kabisaa anasema eti hadi aolewe ndio atafanya na sio kwamba ni bikra,sio bikra..amekataa kabisa.
9. Huwa sijawahi kuacha kumpa chochote anachohitaji,mm naona ni kama tu ananitumia ili mambo yake yaende sawa lakini hanipendi...maana kama ni kuhitisha pesa anahitisha sana
10. Nikiwa nachat nae,yaani text zinajibiwa polepole hadi kero,namtumia text inajibiwa baada ya madakika au lisaa,halafu yupo kabisa online
11. Yaani hayupo romantic kabisa,daahh yaaani huu uhusiano sioni nafaidika chochote,sifaidiki chochote kabisa hapa,naloose tu na kupata stress kila siku
12. Huwa ananiudhi sanaa na huwa ninapomwambia tuachane,huwa anakuwa mnyonge na kunibembeleza vya kutosha turudiane,atawatumia watu mbalimbali kuongea na mm,analia machozi na kuahidi kutorudia,sasa unakuta tu namsamehe na kurudiana nae lakini baada ya muda anarudia yaleyale tena.
8. Yaani ni mrahisi sana kuomba msamaha ila ni mrahisi sana kurudia kosa.
9. Halafu naamini sisi wanaume mwanamke ambaye una malengo nae huwezi kumruhusu avae hovyo,ila sasa yeye mavazi anayovaa hayana maadili ila nikimwambia ni mbishi kupindukia.
10. Halafu huwezi amini na kanisani huwa hakosi,anajua kusali sana na huwa anasoma biblia sana...huyu simuelewi kweli.
11. Halafu ni mtu ambaye hata status anazoweka Whatsapp hazina maadili kabisa,yaani hadi huwa namuuliza hivi wewe huna watu wa heshima huku,huna aibu lkn ni mbishi hasikii
12. Kiufupi ni mtu ambaye inaonyesha hana interest na mm.
13. Pia ni mtu wa hasira sana, yaani huwa anaongea na mimi kwa hasira lakini watu wengine anaongea nao kwa kucheka
14. Company yake ni ya wasichana walioshindikana, yaani ambao hawajiheshimu

Wakuu ni visa vingi huyu msichana amenifanyia,hivi ni baadhi tu. Ni miezi saba sasa tangu niwe nae ila kila siku ni visa, mimi nahisi atakuwa na wanaume wengine ila mimi atakuwa tu ananitumia kujinufaisha kiuchumi tu....sasa nataka niachane nae kabisa na hata nimblock kabisa ijapokuwa nampenda sana,wakuu naumia kwasababu nimekuwa muaminifu sana kwake,sijawahi kumcheat...kweli huyu dada atajuta sana,bado ana akili za kitoto,hajajua anachotaka huyu.
NISHAURINI TU,JE MWANAMKE KAMA HUYU UNAMCHUKULIAJE NA JE USHAKUWA NA MTU KAMA HUYU?View attachment 1185772
Pole sana mkuu piga chini, fanya kazi kwa bidii utampata anayeendana na wewe.
 
Pole sana mkuu, umependa usipopendwa! Ni dhahiri kabisa kuwa hakupendi ila unaendelea kumng’ang’ania! Jitahidi kumsahau uendelee na maisha yako.
 
Focus kwenye maisha yako kimaendeleo ni wazi unapoteza muda hapo...
 
Ndio ni mimi mkuu,ila tatizo nimependa hadi nashindwa kujielewa,sijui nini kimenitokea na mimi huwa sipo hivi,nahisi kuna kitu amenifanyia,niombeeni tu.
Yani ni sawa na kuuliza swali then ukajijibu mwenyewe
 
Nimesoma kwa makini, nikakumbuka Mara nyingi hivi visa tunafanyiwaga wanawake, nikaumia, lakini ndugu yetu hapo mko wanaume zaidi ya Watatu, ila wewe ndio myoa matumizi ndio maana unabembelezwa akikukosea.

Yule mpuuzi Mme mwenzio yeye ndo anapendwa, ila ni Mario, handsome,+ upuuzi mwingine.
Binti anaogopa kukupoteza mtomatumizi,

Mapenzi ni hisia, mteme.

Hivi wananzengo, ulishawahi mpenda mtu mpaka ukiskia SMS imeingia unajua ni yeye kumbe sio yeye maskini ni biko wanakukumbusha kucheza? Unafonzaaaa

Au unapiga simu hapokei unakuta yupo online dah
Hyo ni dharau ya kiwango cha juu kabisa
 
Ukisikia wale wenye roho za paka, huyu ndo mmoja wapo.
Hongera kwa uvumilivu huo
 
Yaan nimeshindwa kumalizia kusoma kwa malalamiko hayo mkuu.
Huyo dada hakupendi hata kidgo yeye shida yake ni huo msaada unaompatia. Na kama huamini sitisha huduma zote iwe ni kwake au kwa ndugu zake, uone sasa utakavyoachwa.
Huyo sio mwanamke wa kuoa ana mambo yake na dalili zote unakuonesha sema wewe tu ndio unampenda sana mpaka huoni hizo kasoro na tabia zake za ajabu.
Fanya maamuzi kwa sababu mwisho wa siku ni maisha yako. Unaweza kupewa ushauri wa kila aina hapa na watu lakini mfanya maamuzi ni wewe.
Mfano mzuri ni rafiki yangu wa kiume aliwahi kuwa na mwanamke wa namna hio mwisho wa siku alifanya maamuzi na huyo dada alikuja kujuta sana kwa sababu wale wanaume aliokuwa anawaona wa maana wote walimuacha akaanza kuomba kurudiana na rafiki yangu. So fanya maamuzi husije kuishi maisha ya majuto wanawake ni wengi na wana heshima katika mahusiano yao.
 
Kama dalili zote hizo bado hujaamini hupendwi ila unafanywa ATM bora ungeenda kuchota mafuta tu kwenye lori mkuu
 
Natamani uwe mdogo wangu, bikuzabe kofi la kichwa akili zikae sawa
 
Hivi Kuna mwanamke anaweza kunifanyia yote haya kweli???????
 
Back
Top Bottom