Nashindwa kukusamehe nashindwa kukuacha

nilianza kukutongoza miaka miwili iliyopita tukiwa collage na hatimaye ukanikubalia.tukaanza mahusiano yetu.tena kwa furaha ya ajabu. tangu niwe na wewe nilikuwa sijui uchungu wa kutendwa.tulipendana zaidi ya kawaida. nilipokukosea moyo haukutulia hadi ulipo nisamehe.nawe ulifanya hivyo hivyo. siku zilipita tukiwa wenye furaha sana sana sana...mpenzi wangu nayaandika haya nikiwa na maumivu makali sana moyoni.hata nashindwa nifanye nini. kwa nini baby unisaliti?kwa nini? ni kipi nilichokukosea?au tatizo ni mimi kuwa mbali na wewe?umenisaliti mbaya zaidi we ndo umenieleza kuwa umesaliti na unahitaji msamaha wangu eti roho inakuuma. nakupenda sana sana sana.natamani nikusamehe lakini roho inasita na natamani tuachane lakini moyo unakataa kata kata.jamani wanajf nifanye nini?mbona nahisi uchungu kiasi hiki?naombeni mawazo yenu jamani

kama amekuambia mwenyewe basi huyo amejutia na anataka msamaha wa dhati,mwingine angekaa kimya na wala usingegundua kamwe,msamehe maisha yaendelee coz nobody is perfect
 
Braza hiyo ni kama investment. Sometimes it never pays off as u expected. Ushauri wangu ni kwamba give it time. As they say " time heals wounds". I hope utamsamehe
 
Ulikosea sana ungechukua 50 na ukampa 50 so cha msingi fikiria mbele na utafakar unahitaji nin kutambua kama bado she has a gape or chance left
 
Watu wengine bana kujishebedua eti anakwambia amekusaliti ndo nini? Ili umuone anakupenda? Huyo dada ni mjinga kwani wewe ukimsalit uwa unamwambia? Ishiiiii
mwache mtu kujifanya mwema kiasi hicho? Liache kamata numberless.
 
Forgiving someone doesn't help him/her it helps you! So kazi kwako, kumsamehe ili uwe na amani au kuacha kumsamehe uendelee kuugulia maumivu.....!!!!!!
 
Yani kama yaliyonikuta mie sina hamu,ndo kilichonifanya nilete uzi wa "Ukitaka kuishi kwa amani ktk dunia usioe" humu.
 
Wacha ujinga wewe, huyo mwanamke anakupenda.... angekuwa hakupenda wala asingeekuambia.... Hakuna mwanamke mwaaminifu kama ilivyo kwa wawanaume pia.... tulia ndugu kugongewa ni suna yakhe alaaaaaaaaaa! na hiyo ndio chachadu ya penzi kama ujui ongeza mbwebwe ili usisalitiwe tena
 
katka mahusiano, Usipende sana kupitiliza coz cku ukichukia utachukia the same way kama ulivyo penda.. kama newton alivyosema "evry action has equal and oposite reaction" me nakushauri mpe nafasi.. mtu anaposaliti na akakiri na kuomba msamaha kujutia makosa yake ni kwamba hata ye anaumia. mpe nafasi.. but this time be carefull.. penda kwa step na kwa akili.. me ninauz mrefu nkipataga mda ntashare na nyinyi... ni long story.
kuna concept hapa
 
Mapenzi hayana formula ndugu mwandishi, hapo inakuuma amekusaliti na kakwambia, we ni mara ngapi unamsaliti na husemi, ebu vaa viatu vyake usikaze akili samehe, wanawake wenye future na akili ya kujitegemea ni wachache sana. Huyo ulonae "aliteleza" kulingana na mahusiano yenu kaamua kukueleza akiamini atapata amani ya moyo zaidi kwa sababu ni wewe pekee uwezae mvumilia kwa hali zote, shukuru hajawapa nafasi marafiki wamshauri kwanza. Mpende ndugu makosa yote yanasameheka kama anavyosamehe Mungu wetu tunaemwabudu.

Wa kwangu Yalipomkuta alilia sana na nilimuona kuwa anamaanisha (hua sishauriwi kwake najiamulia tu),very beautiful one na tangu nimekua nae (from college now tupo tunapambana) kafanyika baraka sana maishan mwangu.
Nishamsaliti mara nyingi tu japo hajawahi nikamata na anajivunia kuwa na mim, aliteleza kwa sababu sikuwa naona thaman yake japo mi nilikua naona kila kitu kipo sawa tu kwa wakati huo, sijui angekuwa anajua yote hayo kuhusu mm ingekuaje.

Mungu nilindie mchumba wangu na unilinde piah mimi maisha yangu, na tukajenge familia bora daima
 
Kweli duniani Kuna majaribu Yan mtu anakusaliti afu anakuchana ukweli.......bwana wee achana nae Mana atakusaliti na tena mwisho upate stroke
 
Back
Top Bottom