Nashindwa kukusamehe nashindwa kukuacha

mwenye shamba

JF-Expert Member
May 31, 2015
978
1,766
Nilianza kukutongoza miaka miwili iliyopita tukiwa collage na hatimaye ukanikubalia tukaanza mahusiano yetutena kwa furaha ya ajabu.

Tangu niwe na wewe nilikuwa sijui uchungu wakutendwa tulipendana zaidi ya kawaida nilipokukosea moyo haukutulia hadi ulipo nisamehe nawe ulifanya hivyo hivyo.

Siku zilipita tukiwa wenye furaha sana sana sana mpenzi wangu nayaandika haya nikiwa na maumivu makali sana moyoni hata nashindwa nifanye nini kwa nini baby unisaliti?kwa nini? ni kipi nilichokukosea?cAu tatizo ni mimi kuwa mbali na wewe?

Umenisaliti mbaya zaidi we ndo umenieleza kuwa umesaliti na unahitaji msamaha wangu eti roho inakuuma nakupenda sana sana sana natamani nikusamehe lakini roho inasita na natamani tuachane lakini moyo unakataa kata kata.

Jamani wanaJf nifanye nini?Mbona nahisi uchungu kiasi hiki?

Naombeni mawazo yenu jamani
 
pole sana! mwenzio nilipenda mwanaume nikamuamini asilimia 100% kilichonikuta cna hamu nacho kumuamini mtu asilimia 100 akija kukusaliti unapata maumivu makali,
 
Kushindwa kumsamehe mtu ni kujiadhibu na kujiharibu mwili, akili na roho yako.

Msamehe, muombe mungu wako akusaidie umsamehe. Kama huwezi kumuacha ni kwa sababu bado unampenda. Muulize sababu ya kukusaliti na uifanyie kazi kiroho safi. Akirudia tena kukusaliti ujue huyo ndio alivyo. Na utabakia na alternatived 2, umuache aende zake ama umchukulie kuwa ndio cha wote ila wewe una majority shares.
 
katka mahusiano, Usipende sana kupitiliza coz cku ukichukia utachukia the same way kama ulivyo penda.. kama newton alivyosema "evry action has equal and oposite reaction" me nakushauri mpe nafasi.. mtu anaposaliti na akakiri na kuomba msamaha kujutia makosa yake ni kwamba hata ye anaumia. mpe nafasi.. but this time be carefull.. penda kwa step na kwa akili.. me ninauz mrefu nkipataga mda ntashare na nyinyi... ni long story.
 
nilianza kukutongoza miaka miwili iliyopita tukiwa collage na hatimaye ukanikubalia.tukaanza mahusiano yetu.tena kwa furaha ya ajabu. tangu niwe na wewe nilikuwa sijui uchungu wa kutendwa.tulipendana zaidi ya kawaida. nilipokukosea moyo haukutulia hadi ulipo nisamehe.nawe ulifanya hivyo hivyo. siku zilipita tukiwa wenye furaha sana sana sana...mpenzi wangu nayaandika haya nikiwa na maumivu makali sana moyoni.hata nashindwa nifanye nini. kwa nini baby unisaliti?kwa nini? ni kipi nilichokukosea?au tatizo ni mimi kuwa mbali na wewe?umenisaliti mbaya zaidi we ndo umenieleza kuwa umesaliti na unahitaji msamaha wangu eti roho inakuuma. nakupenda sana sana sana.natamani nikusamehe lakini roho inasita na natamani tuachane lakini moyo unakataa kata kata.jamani wanajf nifanye nini?mbona nahisi uchungu kiasi hiki?naombeni mawazo yenu jamani

Usipende 100& penda 50, afu 50 unaweka mfukoni
 
Jipe mda wa kutulia na kuongea na moyo wako wa ndani then utapata jibu zuri la Kafanya.
Hakuna kitu cha kupoteza ktk dunia hii vitu vyote hutokea kwa lengo maarum inaweza kuwa ni kujifunza au kutuonyesha upendo au hisia zetu kwa watu tuwapendao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom