Kama wewe unashindwa kujizuia,sijui kwa nini ujiite Senior Member.
Kama unashindwa kujizuia,what you have to remember ila binadamu ana roho ya Mungu,ambayo ni zawadi yake kutoka kwa Mungu,ambayo ni integral part of himself,of every human being, kumsaidia katika maisha yake ya kila siku,ili aweze kufanya maamuzi ya hekima.
Hii ni roho ya Mwenyezi Mungu ambayo anakuwa nayo from a very early age,4,5,or 6 years of age,wakati anapoanza kuzungumza maneno coherent.
Hilo ni jambo la kwanza. Jambo la pili,katika Dini ye Yesu Kristu,tunafundishwa kwamba baada ya Yesu kufundisha Duniani,na baada ya kuondoka,Yesu amewazawadia watu wote,siyo Wakristu wote,siyo wafuasi wake wote,isipokuwa watu wote,Roho ya Kweli,Roho ya kuwaongoza katika ukweli wote,siyo ukweli wa Dini tu.
Kwa hiyo kwanza kuna roho,ruhani kutoka kwa Mwenyezi Mungu,ambaye anafanya kazi kwa ubia,emphasis kwenye neno ubia,kwa sababu ina maana kwamba binadamu pia ana wajibu wa kufanya kazi,labda 90% na ruhani wake 10%,kwa hiyo emphasis kwenye neno ubia.
Halafu ipo Roho ya Kweli iliyoshuka wakati wa Pentecoste,again,siyo kwa Wakristu tu,isipokuwa kwa watu wote Duniani.
Au unaweza kusoma vinaya kama huna self control. Zipo sheria pale katika vinaya,kwa wanaume na kwa wanawake;vinaya pamoja na dharma vinaweza kukusaidia.
Kwa hiyo natamani kwamba fundisho kuhusu roho wa Mungu na Roho wa Kweli,ingekuwa ndio somo la kwanza la Dini,kwamba ndio ahadi yetu kwamba binadamu wote ni ndugu,na Mungu ni Baba yetu.
Ingekuwa ndio ajenda ya kwanza kabisa katika siasa zetu,kumueleza kila mtu aliyeshika maksai,au anayesukuma mkokoteni;kwa tufanye kazi kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu kulijenga Taifa letu.