kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,255
- 16,185
- Thread starter
- #121
Muda unvyoendelea, ndivyo kosa lako linavyokuwa kubwa. Yaani kila shemeji yako anapotoka na rafiki yako mwenye kucheat, nawe unashirikishwa kiasi fulani jambo hilo. Haisaidii wewe kukaa kimya tu. Dunia huharibiwa si na wale watendao maovu tu, bali pia wanaoona maovu na hawafanyi lolote.
Jitwike ujasiri. Kwanza waepe kabisa wapenzi wawili wanaoharibu mambo. Hao si marafiki wazuri. Huyo mwanaume anaweza kukulia hata wewe kama hujui. Tafuta namba ya simu ya siri au unda moja ya kwenye mtandao. Kisha mpelekee ujumbe rafiki yako ananymously kwamba kuna randezvous mahali fulani. Yeye akashuhudie yeye mwenyewe. Itakuwa vibaya kama jamaa atajua kwamba ulijua muda mrefu na hukufanya lolote. Kwa upande mwingine mambo yakija julikana kwamba ni wewe ulitoa siri, own it. Kubali. Kama ni urafiki wa kweli utabaki. Lakini urafiki wa kinafiki haufai.
Siku moja nilikuwa ninampima mwenye mke kwa kumfake (yard stick) na hadithi ya kutunga kuhusu rafiki yangu mwingine huko kazini anayetembea na mke wa rafiki yake wakati mimi nafahamu jambo hilo, nikamuomba anipe ushauri nifanye nini kuhusu hilo, he, yeye alinionya ninyamaze kimya kabisa maana kitakachotokea juu yao nitakuwa ninahusika nacho, akasema "mimi nikijua kuwa rafiki yangu anakula mke wangu nayonga kabisa kwa mikono yangu" he, nilivyosikia vile nikaufyata kabisa mkia nikanyamaza kimya nina mwaka sasa.