Nashindwa Kuelewa Vijana mnafanya nini mjini!!

Nashindwa Kuelewa Vijana mnafanya nini mjini!!

belak

Senior Member
Joined
Jul 23, 2016
Posts
179
Reaction score
377
Hello comrades
Kwa faida ya kizazi cha vijana wetu! Takribani miezi 2 nimekuwa kibiashara mikoa ya iringa, mbeya na rukwa! Kilichonishangaza ni fursa zilizoko mikoa hiyo hasa vijijini. Nikajiuliza hivi vijana wanafanya nini DSM? Wengi hawana ajira lkn kuna fursa nyingi kuanzia ufugaji, kilimo, biashara, na maarifa mengi sana!

Mfano kuna wanaviji wengi wana Ardhi, mazao, na rasilimali mbalimbali lkn hawana kiunganishi kati yao na wanunuzi, pili Huduma nyingi hazipatikani vijijini na zinafuatwa mbali mijini lkn ni rahisi kuanzisha na zinalipa mfano maduka,Mashine za kusaga, migahawa mizuri, huwezi kuamini watu wa vijijini wanapenda kuspend hasa kukiwa na vitu wavitakavyo!fursa ni nyingi mno vijana unahitaji kuja na mtaji mdogo tu angalau laki 4 kuanza kufanya mambo makubwa!

Mijini kunalemaza vijana nakuendelea kutengeneza taifa lenye lawama sana! Ninahakika kijana akiamua hawezi kukosa mtaji huo!

Pendekezo; uwepo mfuko wa kumotivate vijana wanaomaliza vyuo na wanataka kurudi kuendeleza vijiji na kutengeneza ajira huko
 
Mkuu umeandika vizuri na kutoa ushauri mzuri sana,lkn umegeneralise sana,sio vijana wote unaowaona mjini hawana cha kufanya,pia wewe mwenyewe umebakia kijiji gani?
Mimi nacheza kotekote mjini na kijijini lkn pia nimemaanisha vijijini kuna fursa hata kama mjini unakazi unaweza kuendelea kutengeneza pesa zaidi vijijini
 
Labda kwa nafasi ya kipekee fursa nyingi nimeziona mkoa wa iringa! Kuhusu fursa a b c nk inahitaji nini kifanyike ni vzr mhusika sense akafanye kautafiti kdg ili anapowekeza afanye kitu anaweza
 
Mimi nacheza kotekote mjini na kijijini lkn pia nimemaanisha vijijini kuna fursa hata kama mjini unakazi unaweza kuendelea kutengeneza pesa zaidi vijijini
Vijana wa dar hawawezi kukuelewa,huwa hauwaoni ikitokea wamekuja kuzika labda wamefiwa na jirani ambaye kwao ni mkoani?
huwa wanakuwa mzigo kiasi unashangaa sijui walikuja kufanya nini,stori zao utasikia huku hakuna mademu kabisa,daah huku porini sana,utafikiri kule dar wana la maana lolote zaidi ya kulundikana kwenye nyumba za urithi,hii nchi ina watu mizigo sana..
 
Nadhani kama vyombo vya fedha vingewezesha walio tiyari kwenye miji midogo midogo ka kule Nzega, B'mulo, Kahama etc hakika wengi wangeweza kurudisha hiyo mikopo.
Sijasema wapewe bure bali wakopeshwe. Lakini kwa tra hii ya mwendo kasi, unalipa kodi kabla hujaanza mradi, nadhani wengi watajikatia tamaa
 
Tukijazana wote vijijini hizo fursa zitatutosha sasa???
 
Mtoa mada manunuzi na kufunga mashine yataka mtaji ndugu sio kwa laki NNE. Laki nne ni kufungua duka na kuwa mfanyabiashara au kulimisha eka mbili
 
Back
Top Bottom