Nashindwa kuelewa ana maana gani kunipa zawadi ya kondomu

joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,623
5,039
Habari wana MMU,

Ni kwamba juzi nilimwambia mpenzi wangu kuwa nina ziara ya kwenda Dodoma kikazi kama wiki moja hivi. Hivyo basi jana asubuhi alikuja tukashinda wote na mpaka leo asubuhi naondoka amenisindikiza kidogo tu akarudi.

Sasa wakati anarudi akaniambia kuwa kwenye begi nimekuekea zawadi yako ila hakutaka kusema ni aina gani ya zawadi. Nikajaribu kumuuliza kwa lugha ya upole ile aweze niambia ni zawadi ila akawa mgumu kusema basi nikwambia ahsante kwa zawadi natumai itakuwa nzuri queen wangu.

Baada ya kupiga hatua kidogo nikafungua zawadi hiyo iliyowekwa kwenye bahasha ya kaki ndogo hivi. Zawadi yenyewe ni Condom pakiti mbili. Kiukweli imesababisha nikacheka sana na kuhisi kuchoka.

Hakika nimeshindwa kumuelewa sio siri ndugu zangu.Je haniamni au imekuwaje mpaka amepata ujasiri wa kufanya hivo?Nikimuuliza kamaanisha nini au kwanini kafanya hivo anabaki cheka tu.

Je hiki kitendo kimekaaje wana MMU?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom