Nashindwa kuelewa alimanisha nini

Nashindwa kuelewa alimanisha nini

UWOGA=UMASKINI

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
2,400
Reaction score
1,017
Wapenzi wa jamii forum nakumbuka mwaka juzi rafiki yangu alinishirikisha ugomvi wake na mkewe walibahatika kupata watoto wawili aliponiambia amegombana na mkewe na baada ya ugomvi ule mkewe akamwambia watoto hawa kwanza si wako mkewe huyo aliyasema maneno hayo akiwa na hasira kali .na kwa kifupi watoto hao wamefanana sana na mama yao rangi na sura sasa mimi nilimpa moyo rafiki yangu huyo


Ila leo kaniuliza tena unakumbuka lile jambo aliloniambia shemeji yako mwaka juzi bado unaniambia nini kuhusu lile neno .mwanamke kaomba msamaha kwa machozi na kugaragara ila jamaa akamwambia sawa lakini bado analo moyoni

NIKAONA NIWASHIRIKISHE NANYI JE NI JAMBO LA KAWAIDA KWELI NA JE KUNA ALIYEKWISHA KUTWA NALO KUAMBIWA HIVYO
 
Wanasaikolojia wanasema ukitaka kumjua mtu na siri zake vizia akiwa amelewa, nahela, kaishiwa, anahasira n. k, hapo yaweza ikawa watoto siyo wa jamaa au huyo mama anamtu mwingine nje
 
Anaumiza kichwa good 3 yrs? mwambie kitanda hakizai haramu na asiweke mawazo hayo kama ni mkewe halali wa ndoa
basi watoto ni wake kwani wamepatikana ndani ya ndoa..
 
Hata hivyo mother ndio mwenye ushahidi wa mwisho kuwa watoto ni wa nani?na vile vile labda aliongea kwa hasira tu.
 
Dunia hii jamani.. Wanaume tunapita kwenye wakati mgumu sana..Kuepuka magonjwa nyemelezi ni kuachana na mapenzi na kuachana na mapenzi ni vigumu sana
 
hakuna maneno ya ukwel kama yanayotamkwa out of anger.... nahis mke alimaanisha alichkisema ila sasa ni kaz ya mume kuthibitsha
 
Hapo ni asilimia 49 za Mkemia. Inaweza ikawa ni hasira au ni kweli ila mwanamke akiwa na hasira hutumia maneno machungu ya kuumiza maana hana nguvu ya kupigana
Hasira hizo ni mbaya coz anampoteza mume huvi hivi
 
Yawezekana aliamua sema vile kwa hasira ku secure watoto ili abk na haki nao mi ndo navohs asubr hsra ziishe wakae wazungumze watafkia muafaka
 
Back
Top Bottom