Nasherehekea kuachwa na mchumba niliyemzalisha

Nasherehekea kuachwa na mchumba niliyemzalisha

Amoxlin

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Posts
3,781
Reaction score
4,118
Habari wapendwa wote. Leo nimependelea kuwashirikisha furaha kuu ninayoishi nayo mwaka wa pili sasa.

Ilikuwa hivi, Mwaka 2011 Nov nilianza mahusiano na bint mmoja wa Kikaguru akiwa kidato cha 3 kwenda cha nne 2012. Alimaliza kidato cha nne na kujiunga na mafunzo ya katika ngazi ya cheti.

Mwaka 2014 alipata ujauzito akiwa anamalizia masomo ya ngazi ya cheti, Wazazi wake walighafirika sana kwa kitendo hicho ila nikaongea na Wazee wangu wakawasiliana na kila kitu kikawa sawia. Baada ya kuhitimu alijifungua, Ndugu zangu walisafiri mpaka Dodoma wakamalizana ikiwa ni pamoja na kulipa tozo ya adhabu.

Sikutaka niwe sababu ya kumharibia maisha huyu bint. Niliahidi kumuoa na mwaka mmoja baadae nilienda kwao kulipa mahari. Siku hiyo walikuwepo ndugu zake wengi sana kukawa na tafrija na nikapewa jukumu la kumuendeleza kielimu (kumsomesha) kwani hayupo kwenye himaya yao tena, ni wakwangu.

Kipato changu kilikua cha tabu sana ila nililipokea hilo jukumu, nikapambana nilivyoweza, wazazi walinisaidia pia mpaka akamaliza diploma (zilinigharimu kama 4M) na nikamsaidia kuapply degree.

Tangu nianze nae mahusiano nilikuwa mwaminifu sana kwake, nilivumilia vitimbwi na visa vingi mno vya udanganyifu na usaliti alivyokua akinifanyia. Nimemfuma akicheat kwa simu karibu mara kumi na watu tofauti. Na ilikua tabia ya kujirudia kila mara.

Nilikua naumia ila nilijizuia nisimuache ili kukwepa lawama ya "umenizalisha na kuniacha" umeniharibia maisha yangu...

Niliisubiri kwa hamu sana siku ambayo angeniacha yeye na si mimi nimuache.

Hatimae mwaka 2018 Akiwa mwaka wa kwanza chuo kikuu alipata dalali mmoja wa magari pale taifa - temeke akamrubuni kwa fedha na outing za kutosha akaanza kunidharau to the maximum. Naamini huyu jamaa alikuwa nae tangu akiwa diploma ila penzi kikohozi lilikuja kumpalia mbeleni.

Siku moja akaniambia Jerry mi naona bora tuachane kuliko kuishi maisha ya kutokuelewana kila siku. Sikumjibu lolote mpaka yakapita masaa 24 ili nijiridhishe kama kamaanisha au atabadili kauli.

Siku iliyofuatia nilimtext na kumwambie nimeridhia ombi lake la kuachana akafurahi na kinipa option za kuhalalisha kuachana kwetu na nikazifuata tukaachana kihalali.

Haikupita miezi alirud kunisihi turudiane tumlee mtoto ila haikuwezekana, dalali aliyemrubuni alishamuacha na akaendelea kudanga na rafiki zake.

Nikisema nielezee kila kitu nitaandika kitabu maana ni visa na vituko vingi.

Leo nafanya tafrija ya kujipongeza kuachwa na mzazi mwenzangu kwa naishi maisha ya amani sana tangu aniache, sina stress kabisa tofauti na nlipokuwa nae.

Kama uliwahi kuachwa na ww jipongeze mkuu!
 
Karibu sasa rasmi kwenye chama chetu cha Mabaharia wa ardhini nchini. Kwa maelezo zaidi ya kuhusu ada, vikao na mikakati! tuwasiliane.

Mimi ni mlezi wao.
 
Heading yako uliyoweka nilitamani kukutukana kimoyomoyo kwani niliona umetenda ukatili...

Lakini maelezo uliyoweka yameniweka nuruni.

Pole sana kwa maswahibu.

Kisheria unapaswa kumshtaki akurudishie gharama zote ulizoingia kwa sababu tayari mliweka ahadi ya ndoa na ulishakamilisha taratibu za ndugu.

Hii ni kesi nzuri sana kwa wanasheria wabobezi wa sheria ya mahusiano na ndoa.

Analipa hata kwa kuuza mali za babake.
 
Ndipo nikasikia sauti ikisema mjinga we hujui kuwa amekuambukiza ngoma,nyanyuka uende hospitali uanze dozi,ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno
 
Hongera kwa uvumilivu na hongera kwa kuachwa. Wanawake wengine bana huwa ni pasua kichwa kweli. Ila kumbuka wewe ni baba wa mtoto wake/wenu hivyo hakikisha mwanao hawi sehemu ya kuachana kwenu.
 
Back
Top Bottom