Nashauri wasio kwenye ndoa wasichangie mada za ndoa

Muwe na jukwaa lenu kama hamtaki michango yetu.
Mkiwa na jukwaa lenu itatusaidia kujua wakaka wazuri wazuri walio single.

Tofauti na hapo msituchoshe maana hata padre hajaoa ila anafungisha ndoa.

Mkija hospital tunawatibu hata kama mko kwenye ndoa zenu

Mkija mahakamani tunatatua migogoro yenu ya ndoa.

Mkija kanisani tunawaombea wote.bila kujali ndoa zenu.

In short sisi ambao bado, hatukwepeki, some times bila sisi nyinyi mnapwaya.😂😂😂😂
Hoja zoote hapo zinaonesha hujaelewa mada inayo jadiliwa; ingekuwa ni mtihani yaani ulisha pata Zero; Pole!
 
Yaan we unahisi kufahamu umbea umbea wa maisha ya ndoa ya flani ndo kufahamu maisha ya ndoa?
Huo umbea ndio mwanzo wa kujenga au kubomoa ndoa, watu wa nje wanaweza kumjua mtu vizuri tofauti na wanaoishi nao ndani mana nje atajiona yuko huru tofauti na akiwa ndani.
 
Huo umbea ndio mwanzo wa kujenga au kubomoa ndoa, watu wa nje wanaweza kumjua mtu vizuri tofauti na wanaoishi nao ndani mana nje atajiona yuko huru tofauti na akiwa ndani.
Kumjua mtu ndo kuijua ndoa? Navojua ndoa zenye misukosuko, hazifanani iyo misukosuko, ndoa zenye amani hazina formula moja yenye kuleta amani......ni kutumia akili na busara za kiutu uzima kuelewana humo ndani
 
Hoja zoote hapo zinaonesha hujaelewa mada inayo jadiliwa; ingekuwa ni mtihani yaani ulisha pata Zero; Pole!
Labda ingekuwa mtihani wa hesabu ila ile mitihani mingine inayotaka
....discuss
....explain
....with examples
....list, define
....etc ndo ungejua kwa nini mahakimu wamesoma sheria moja ila hukumu zinakuwa tofauti, au mawakili walofunzwa na mwl mmoja sheria ile ile ila wanazozana bila muafaka. Au dr kutoa dawa tofauti wakati ugonjwa ni ule ule.
 
Ata wajinga na wapumbavu nao wanao na kuolewa vile vile.
Kuna ambae hayupo kwenye ndoa ila ana busara na hekima za kumshauri aliekwenye ndoa kuliko unavyo fikiria.
 
Ata wajinga na wapumbavu nao wanao na kuolewa vile vile.
Kuna ambae hayupo kwenye ndoa ila ana busara na hekima za kumshauri aliekwenye ndoa kuliko unavyo fikiria.
kwa kuwa wengi wa Serengeti boys approximately 90% wamekosa sifa, hata hiyo 5 to 10% tumeona ipumzike kwa sasa. Huwa hakuna maamuzi duniani yanayoweza kufavor watu wote; hivyo wala usiumize Kichwa.
Generally Serengeti boys wameonesha kuwa na mawazo mabovu kabisa ( hata kwa kusuluhisha isue ndogo ndogo tu zakifamilia) hivyo wamekosa sifa ya kumshauri mtu anayepitia changamoto ya Ndoa. Atakaye jichanganya kuwasikiliza; ataacha Mume wake/mke wake na ndani ya Mwezi tayari anataka warudiane
 
😀 Ila bana kuna saa unaeza ona mtu anashauri kitu kuhusu ndoa mpaka unajisemea moyoni hivi huyu anaijua ndoa vizuri au ndo anaisikia sikia tu.

Pia niseme hiyo ya kusema wasichangie ni ngumu kwani hili ni jukwaa huru kikubwa ni wewe mshauriwa unapoleta jambo lako kuhusu ndoa ujue kuchambua pumba na mchele.
 
Back
Top Bottom