Nashauri Rais aunde Tume ya Upatanishi

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,486
86,002
Kwa trend inayoendelea sasa, kimya kimya, wazi wazi na pengine kwa sauti zaidi kila kona ya nchi ni dhahiri kuwa kuna watu wana maumivu na vidonda vikubwa sana vilivyotokana na utawala wa Magufuli.

Ni ngumu kusahau Mara moja ila ili kuleta umoja wa Kitaifa NASHAURI iundwe tume au Kamati ya Usuluhishi na Upatanisho kama Taifa.

Tuanze upya kama Taiga, tuanze upya kama ndugu na zaidi tusahau tulipojikwaa, tuangalie mbele zaidi.

Watuhumiwa wanaoweza kuitwa na hata kukutanishwa na familia za Waathirika, waombe msamaha tufungue ukurasa mpya.

Siasa za visasi ni mbaya sana, Rais ajitahidi kufuta hiki kitu, kama tutalazimika hata kurudi tena kwenye uchaguzi Mkuu basi na ikawe hivyo. Tutachangia uchaguzi kama Burundi walivyofanya.

Ni muhimu as a Nation kufanya damage control maana ni wazi kabisa UTAWALA ule ulituumiza, hatuhitaji kubaki hapo kwenye kuumizwa BALI tunahitaji kuendelea na safari tukiwa pamoja.

Mungu Ibariki Tanzania
 
“Unafiki ni jambo baya katika Maisha yetu wote na kama Viongozi wetu wakiwa Wanafiki wasipokuwa wakweli hawatomsaidia Mama Samia, wale wa CHADEMA wakiwa Wanafiki kwangu hawatoisaidia CHADEMA, tujenge Taifa la wanaoheshimu ukweli, ukweli utatuweka huru”———MBOWE
#MillardAyoUPDATES https://t.co/SWGG4SjZIg
 
Njia pekee ya kuleta maridhiano ni kuwafidia wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na utawala uliopita.
Ni sahihi pia ni option nyingine nzuri! Na ikiibuka kuwa kuna ambao walidhulumiwa uhai?
 
Kuna sehemu nimesema wana siasa pekee? Una bahati nimestaafu siku hizi
Nafikiri hukumuelewa! Ana maana kwamba utengano unaousema kwamba iundwe Kamati ya upatanishi - ni wana siasa wanao tengana au kuendeleza huo utengano na visasi! Siyo wananchi wote au watanzania wote, ndiyo maana yake. Na jamii ya Wanasiasa wa kihivyo, ni sehemu ndogo sana ya watanzania wote - kuundiwa Kamati!
 
Hahahaha hahahahaha hahahahaha haya! Wana siasa sio sehemu ya jamii kumbe? Siasa sio sehemu ya jamii?
 
Wanasiasa wote naona mnatuchanganya tu,hamna huruma dhidi ya watu maskini,mnajali matumbo yenu na maslahi yenu,hamjawahi kumtumikia mwananchi wa kipato cha chini,hii nchi sio ya kwenu ni ya wote mmepewa dhamana na hawa masikini,mkipata vyeo mnajisahau na mnawategea mgongo hao waliowapa,nyie ni wapuuzi sana msitusumbue,saa hizi kila mtu anafungua domo lake kuongea anachokitaka zamani mlikuwa wapi kama sio unafiki ni nn? Acheni upumbavu na unafiki!
 
Wewe ungeweza kufungua mdomo akiwa hai? At least hata mimi nilikua naongea
 
Kuna watu ni wapumbavu sana, na mleta mada ni miongoni mwao; hiyo tume unataka iwapatanishe akina nani? Mshaigeuza hii nchi na watu wake ni ya kutimizia matakwa yenu bunafsi. Hao unaoona sanapiga kelele sio kwamba wana machungu na nchi ila wanachumia matumbo yao kama huamini subiri wapate madaraka uone kama watasema tena. Grow up kijana usiwaamini wanasiasa na usiwategemee kwa mambo yako binafsi watakuangusha. Acha kila mtu apambanie maisha yake anayeona anaonewa aache siasa afanye mengine.
 
Wanasiasa wote naona mnatuchanganya tu,hamna huruma dhidi ya watu maskini,mnajali matumbo yenu na maslahi yenu,hamjawahi kumtumikia mwananchi wa kipato cha chini,hii nchi sio ya kwenu ni ya wote mmepewa dhamana na hawa masikini,mkipata vyeo mnajisahau na mnawategea mgongo hao waliowapa,nyie ni wapuuzi sana msitusumbue,saa hizi kila mtu anafungua domo lake kuongea anachokitaka zamani mlikuwa wapi kama sio unafiki ni nn? Acheni upumbavu na unafiki!
Kula like .
 
Kwa trend inayoendelea sasa, kimya kimya, wazi wazi na pengine kwa sauti zaidi kila kona ya nchi ni dhahiri kuwa kuna watu wana maumivu na vidonda vikubwa sana vilivyotokana na utawala wa Magufuli.

Ni ngumu kusahau Mara moja ila ili kuleta umoja wa Kitaifa NASHAURI iundwe tume au Kamati ya Usuluhishi na Upatanisho kama Taifa.

Tuanze upya kama Taiga, tuanze upya kama ndugu na zaidi tusahau tulipojikwaa, tuangalie mbele zaidi.

Watuhumiwa wanaoweza kuitwa na hata kukutanishwa na familia za Waathirika, waombe msamaha tufungue ukurasa mpya.

Siasa za visasi ni mbaya sana, Rais ajitahidi kufuta hiki kitu, kama tutalazimika hata kurudi tena kwenye uchaguzi Mkuu basi na ikawe hivyo. Tutachangia uchaguzi kama Burundi walivyofanya.

Ni muhimu as a Nation kufanya damage control maana ni wazi kabisa UTAWALA ule ulituumiza, hatuhitaji kubaki hapo kwenye kuumizwa BALI tunahitaji kuendelea na safari tukiwa pamoja.

Mungu Ibariki Tanzania
Japo kunawaliozoea kuongea kwa tungo tata nimegundua hawawezi kuacha
 
Back
Top Bottom