PostGE2025 THRDC: Iundwe Tume ya Ukweli, Uwajibikaji na Upatanishi

PostGE2025 THRDC: Iundwe Tume ya Ukweli, Uwajibikaji na Upatanishi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,095
Reaction score
7,116
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetaka kuundwa kwa Tume ya Ukweli, Uwajibikaji na Upatanishi akisema ndiyo njia pekee ya kulivusha taifa kutoka katika mgawanyiko mkubwa na majeraha ya kijamii yaliyosababishwa na matukio ya wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Mratibu wa Kitaifa wa mtandao huo Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuwa jitihada za maridhiano zilizofanyika kabla ya uchaguzi hazitoshi tena kurejesha mshikamano, kwani hali ya taifa baada ya Oktoba 29 imekuwa tofauti kabisa na mazingira yaliyokuwepo katika kipindi cha kuelekea uchaguzi.

Amesema kabla ya uchaguzi, maridhiano yalihusu changamoto za kawaida kama mazingira ya uchaguzi lakini machafuko ya wakati na baada ya Oktoba yamezua maumivu mapya, vifo, kupotea kwa watu na hofu ya kitaifa ambayo haiwezi kutatuliwa kwa mbinu zile zile za awali.
 
hawezi kuelewa. Mpaka muda huu yeye yuko busy kutafuta chanzo cha tatizo nje! Yaani anataka kuwaangushia wengine jumba bovu lake! Huku akiwa hajui kama yeye mwenyewe na chama chake ndiyo chanzo kikuu cha matatizo yote nchini.
 
Back
Top Bottom