Nashauri NIDA wasiweke "signature" ya mwenye kitambulisho wazi

Wickama

JF-Expert Member
Mar 8, 2009
1,466
1,195
Wadau,
Kitambulisho cha uraia ni kitu nyeti. Hususan ukizingatia hali ya nchi zinazotuzunguka. Kumekuwa na hili tatizo la kwamba vitambulisho vya NIDA havina sahihi ya mmiliki kama vile vya wapiga kura. Binafsi nadhani kwa unyeti wa kitambulisho cha uraia ni bora sahihi ya mmiliki ikabaki kwenye "CHIP" ya kitambulisho kama alivyojulisha hivi karibuni bosi mmoja wa NIDA kuliko kuiweka hadharani. Kuificha ndani ya chip ni rahisi na salama zaidi kumbaini mwizi au mnunuzi wa kitambulisho kinyume na sheria kwa vile mara nyingi hatakua anajua sahihi ya mmliki wa awali kuliko kuiweka hadharani ambapo anapata muda wa kujifunza kuighushi. Labda kuna mawazo mbadala tuyasikie.
 
...hili nalo linahitaji mjadala!?...hilo ni 'tatizo' kwa wasioelewa!
.....wajielimishe!
 
Hapo mtoa mada umenena. Hakuna haja ya kitambulisho cha Uraia kuwa na sahihi, ili ibaki kuwa mojawapo ya "security features' kwani hiki ni kitu nyeti.

Naona wanataka kuweka sahihi ili kumfurahisha mkuu wa kaya lakini akieleweshwa mbona ataelewa tu...
 
Sioni kama ni sawa kwa sababu kama huyo mtu ataweza kufoji saini lakini sidhani kama ataweza kufoji na picha lakini pia kwa kuwa kile kitambulisho kinasomwa kupitia kifaa maalum ambacho kitatoa taarifa zako kwa kirefu ni rahisi kumtega mtu anayetiliwa shaka kwa kumuuliza swali la kushtukiza kama jina la mama yake au mahali alipozaliwa huyo mzazi au kitu chochote ambacho hakipo wazi kwenye kile kitambulisho
 
Vya mwanzo vyote viko hivyo na mkuu wa Kaya anajua, hii ya kuiweka hadharani naipinga sana
 
Back
Top Bottom